Ijue Toyota Progres kwa ufupi

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
358
670
IFAHAM TOYOTA PROGRES- kwa ufupi

Na KIMOMWE MOTORS (T) LTD- Waagiza Magari

Utangulizi
Gari hii ndogo ya starehe ilizalishwa miaka ya 1998- 2007. Mshindani wake ni Lexus IS ingawa Progress inaelezewa kuundwa vizuri hivyo kutokua na mitetemo katika vumbi.

Injini na Mafuta
1JZ yenye Cc 2500- Vvti inatumia mafuta chini zaidi kiasi cha Km 12/L.

Utulivu na Uimara
Inaenda mpaka speed 180 ikiwa imara na katika vumbi ni tulivu sana

Vifaa
Vinapatikana kwa gharama za wastani.

Nyongeza
Airbags 6 badala ya 2 kama zilivyo Brevis, Verossa, Mark 2, Cresta au Crown. Viti vya ngozi, nakshi ya mbao, na GPS ya Sauti na Screen.

Maoni na Ushauri
Ikiwa unafikiria gari ndogo ya starehe yenye uwezo mzuri wa safari katika barabara zote na yenye usalama mzuri, hii pia sio ya kuacha kuifikiria.

Shukrani mkuu kwa makala hii, ninaisubiri kwa hamu makala ya Toyota Corolla Rumion, Rav4 (ile diesel engine toleo la uingereza) pamoja na Alphard
 
Na pia huko masokoni (Japan)hazipo kwa wingi ndo sababu kuu ukichanganya na ubugiaji wake wa mafuta imelifanya lisiwe popular kwetu ila ni gari nzuri kwa mbio na utulivu likiwa barabarani
Kwny wese sio inshu Sana,maana engine zilizoko kwny hio Gari ndio ziko kwny Brevis na Brevis mtaani zimejaa,khs uwepo wake sokoni huko Japan sijui maana hata huko Beforward/SBT Progress hua ni nyingi kuliko Brevis.

Labda umbo la Progress wabongo hawakuvutiwa nalo.
 
Kutakuwa na sababu inayofanya Progress isifanye vizuri kwenye soko.
 
Hivi wakuu ninajua Kuna magari yenye injini za VVTI Ila hasa sijui maana yake. Injini za VVTIkitaalam Zina nini?
 
Hivi wakuu ninajua Kuna magari yenye injini za VVTI Ila hasa sijui maana yake. Injini za VVTIkitaalam Zina nini?

Unaifahamu engine ya gari vizuri? Nikisema Camshaft na Crankshaft utakuwa unaelewa.ni vitu gani?

Kwa maana at least ndio ningeweza kukupa maelezo mazuri ya mfumo wa Vvti.
 
Back
Top Bottom