Ijue Sheria Mpya ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Sheria mpya ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za Kulevya ya mwaka 2015 (The Drugs Control and Enforcement Act, 2015)

Baadhi ya mambo muhimu ambayo yamezingatiwa kwenye sheria mpya ikilinganishwa na Sheria ya sasa ni kama ifuatavyo.

Mosi, pamoja na Sheria mpya kuendelea kutumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kama ilivyo kwenye sheria ya sasa na kwa kuzingatia kuwa Zanzibar ina chombo cha kudhibiti madawa ya kulevya, Sheria mpya imeainisha namna Serikali mbili zitakavyoshirikiana katika kukabiliana na kudhibiti tatizo la dawa za kulevya nchini.

Pili, Sheria ya Mpya imeanzisha Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya ambalo mwenyekiti ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lina wajumbe kutoka pande zote za Muungano. Jukumu la Baraza hili ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Tatu, ili kuiwezesha Mamlaka na Kamishna wa Mamlaka kutekeleza majukumu yake vyema, Sheria imeanzisha Kamati ya Ushauri ambayo majukumu yake makuu yatakuwa nikumshauri Kamishna Mkuu kuhusu masuala ya udhibiti wa dawa za kulevya.

Nne, Sheria iliyopo ina udhaifu wa adhabu, haitoi adhabu kulingana na ukubwa wa kosa kwenye baadhi ya makosa, hivyo kusababisha kukosekana kwa mizania ya haki. Sheria mpya imeweka kima cha kuanzia cha adhabu iwe ni faini au kifungo. Kwa mfano;

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria iliyopo, adhabu ya kujihusisha na kilimo cha mimea ya dawa za kulevya (mfano bangi) ni faini ya shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka 20. Sheria mpya imeweka adhabu ya faini isiyopungua milioni 50 na isiyozidi milioni 500 au kifungo kisichopungua miaka 7 na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja.
(b) Adhabu ya kosa la kufadhili biashara haramu ya dawa za kulevya katika sheria ya sasa ni faini ya shilingi milioni 10. Sheria mpya imeweka adhabu ya shilingi bilioni moja (1) au kifungo kisichopungua miaka 30 au vyote kwa pamoja mbali na kutaifishwa kwa mali za mfadhili.
(c) Kwa upande wa makosa ya kusafirisha na kufanya biashara ya dawa za kulevya, sheria ya sasa imetoa adhabu ya faini au kifungo cha maisha. Katika sheria mpya, adhabu iliyowekwa ni kifungo cha maisha peke yake. Lengo ni kuandoa uwezekano wa wahalifu kupewa adhabu ya faini pekee ambayo ni rahisi kuilipa.

Tano, Sheria ya sasa imeweka kigezo cha kutumia thamani ya dawa za kulevya katika kutoa dhamana na adhabu kwa baadhi ya makosa. Kwa vile dawa hizo zina bei kubwa sana, kuonyesha thamani kunachochea na kushawishi watu hususani vijana kujiingiza katika biashara hii haramu. Sheria mpya inaweka uzito kama kigezo cha dhamana na adhabu badala ya thamani kama ilivyo sasa.

Sita, Sheria iliyopo haijaharamisha baadhi ya vitendo vinavyohusiana na biashara ya dawa za kulevya, vikiwemo kumiliki mitambo au maabara kwa lengo la kutengeneza dawa hizi. Sheria mpya imeharamisha umiliki wa mitambo hii na kuweka adhabu kali kwa kosa hili ambayo ni kifungo cha maisha na faini isiyopungua shilingi Milioni 200.

Saba, Pamoja na kuwepo kwa ukamataji wa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya katika bahari kuu karibu na mipaka ya Tanzania, Sheria iliyopo haitoi mamlaka ya kushughulikia watuhumiwa wanaokamatwa katika maeneo hayo. Kwa sababu hiyo, dawa zinazokamatwa katika maeneo hayo hutoswa baharini na watuhumiwa huachiwa. Sheria inayopendekezwa imetoa mamlaka ya kushughulikia uhalifu wa dawa za kulevya nje ya mipaka ya Tanzania katika vyombo vya usafiri wa majini na angani pamoja na bahari kuu;

Nane, Sheria mpya imetoa adhabu ya faini au kifungo jela ili kuwadhibiti watendaji waliopo katika udhibiti wa dawa za kulevya wanaokiuka maadili ya kazi, jambo ambalo haliko katika sheria iliyopo.

Tisa, Sheria ya sasa haitoi adhabu kwa makampuni ambayo yanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya isipokuwa kwa menejimenti ya makampuni hayo tu. Jambo hili limezingatiwa Sheria mpya kwani inaweka adhabu kwa kampuni na menejimenti yoyote itakayojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kuifilisi.

Kumi, katika kukabiliana na malalamiko kwamba kesi za dawa za kulevya huchukua muda mrefu mahakamani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utaratibu wenye mlolongo mrefu wa uendeshaji wa mashtaka,Sheria mpya imeweka fomu maalum ambazo hazipo kwenye sheria inayotumika sasa. Fomu hizi zitaondoa ulazima wa kumtafuta shahidi ambaye wakati mwingine hawezi kupatikana kiurahisi, hivyo kuongeza kasi katika kuendesha mashtaka.

Kumi na Moja, Sheria mpya imeweka adhabu ya kifungo cha miaka isiyopungua 30 kwa watuhumiwa watakaowashawishi au kuwahusisha watoto kujiingiza kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya tofauti na Sheria ya sasa ambayo ipo kimya kuhusu suala hili zaidi.

Kumi na Mbili, Sheria mpya imeweka utaratibu na masharti kuhusu kufilisi mali zinazotokana na biashara ya dawa za kulevya kama inavyoonekana katika Sehemu ya Tano ya Sheria. Aidha, Sheria imeweka masharti kuhusu kutaifisha mali au kifaa kilichotumika katika kutenda kosa chini ya sheria hii. Masharti haya kuhusu ufilisi wa mali yanalenga kuhakikisha kuwa mhalifu hafanufaiki na biashara hiyo ya madawa ya kulevya. Hii itasaidia kuionesha jamii kuwa uhalifu haulipi.

Kumi na Tatu, Sheria mpya imeanzisha Mfuko wa kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya. Baadhi ya vyanzo vya mapato vya mfuko huo vitatokana na fedha itakayoidhinishwa na Bunge, mapato ya mali zinazotokana na biashara haramu ya dawa za kulevya zilizofilisiwa, misaada, mikopo na michango ya hiari.

Kumu na Nne, Sheria mpya imeainisha vyema masharti kwamba Serikali itakuwa na wajibu wa kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya ikiwemo uanzishaji wa vituo vya tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya. Matibabu hayo yatasaidia kupunguza utumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha kuimarika kwa afya ya watumiaji na kupungua kwa tabia hatarishi zinazoongeza maambukizi ya magonjwa mbalimbali kama UKIMWI, virusi vya homa ya ini na kifua kikuu. Aidha, matibabu kwa watumiaji hupunguza uhalifu mitaani.

Hatua nyingine zitakazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti dawa za kulevya ni pamoja na;
(a) Kuratibu shughuli zitakazofanywa na maafisa na na Taasisi chini ya Sheria hii;na
(b) Kusaidia Mamlaka katika nchi za nje na mataifa ya kimataifa kwa lengo la kuwezesha shughuli za uratibu ili kuwa na mikakati ya pamoja ya dawa za kulevya nakotiki na saikotropiki.

Ni muhimu kufahamu kuwa Sheria mpya imezingatia uwepo wa Mikataba ya kimataifa na Maazimio ya Kikanda yanayohusiana na udhibiti wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya na itafanya kazi sambamba na sheria nyingine na inaweka masharti ya Tanzania kushirikiana na nchi nyingine katika mapambano ya biashara na usafirishaji wa dawa za kulevya. Vilevile, itawezesha uwepo wa mfumo mzuri wenye kukidhi udhibiti wa dawa za kulevya, unaoendana na wakati kwa kuzingatia hali halisi ya ukubwa na ugumu wa tatizo hili kitaifa na kimataifa.

Wakati wa kutekeleza sheria hii zipo sheria ambazo zitatumika pamoja na sheria mpya. Sheria hizo ni pamoja na; The Tanzania Food, Drugs and Cosmetics Act, 2003; The Industrial and Consumer Chemicals (Management and Control) Act, 2003; Sheria ya Ushahidi (The Evidence Act [Cap 6]), Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (the Criminal Procedures Act [Cap 20]), Sheria ya Forodha (Customs (Management and Tariff) Act, [Cap 403], na Sheria ya Uhamiaji ya (Immagration Act).
 
Nyie mnaotajwa tajwa mjipange kisaikolojia maana siku mahakama ikijiridhisha mna hatia basis unaweza kuwa mwisho wa kuikamata fursa twendezetu..................
...wapi WAFU FM
 
Nyie mnaotajwa tajwa mjipange kisaikolojia maana siku mahakama ikijiridhisha mna hatia basis unaweza kuwa mwisho wa kuikamata fursa twendezetu..................
...wapi WAFU FM
Nakumbuka wakati hii sheria inapitishwa kulikuwa na mabishano makali sana Bungeni kati ya wabunge wa upinzani,wabunge wa CCM na AG na mjadala ulienda mpaka saa 2 usiku au saa 3 kama sikosei

kuna wabunge walikuwa wanataka sheria soft katika hii vita na kuna wengine walitaka tuwe na sheria ya kunyonga ili walizidiwa nguvu na waliowapinga.
 
Na CCM hawakutaka kuwasikiliza Wapinzani wakijua wahanga ni Wapinzani leo wenye kisu wanajikata na kisu chao wenyewe
 
Na CCM hawakutaka kuwasikiliza Wapinzani wakijua wahanga ni Wapinzani leo wenye kisu wanajikata na kisu chao wenyewe
Demokrasia ya wengi wape ni hasara kwa nchi zetu hizi maana wengi ni vilaza na wacheche ndio wenye kujitambua.
 
Back
Top Bottom