Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 3,910
- 6,707
Piston ni sehemu ama kifaa mojawapo katika engine ya gari ,ambacho hutumika kudhibiti hewa na mafuta ndani ya cylinder.
Pia kutoa nguvu itokanayo na kuungua kwa mafuta kupitia connect rod hadi kwenye crank shaft.
Piston hufanya kazi kwa ushirikiano katika engine na kusababisha kuizungusha crank shaft. Crank shaft inapozunguka hupeleka nguvu katika gear box hadi kwenye diff kupitia poropela na hatimaye tairi kutembea.
Piston inapopanda juu na kushuka chini
Hatua hii husababisha mapigo manne ndani ya chemba za cylinder.
1 Pigo la kwanza piston inashuka chini. Kitendo hiki huruhusu valve kuingiza hewa safi au hewa iliyochanganywa na fuel. (inategemeana na injini kati ya petrol au diesel)
2 Pigo la pili piston inapanda juu
Kitendo hicho kinasababisha ile hewa safi iliyo ingia kwenye chemba kukandamizwa kwa mgandamizo mkubwa sana na hewa hiyo kuwa na joto kubwa sana, kisha plug inatoa cheche au nozeli inanyunyiza mafuta (plug au nozel, hapa inategemeana na engine ya petrol au diesel.
3 Pigo la tatu
Baada ya ile hewa yenye joto kali kukutana na cheche kutoka kwenye plug au mafuta kutoka katika nozel husababisha mlipuko mkubwa uliosababishwa na kuchomwa au kuunguzwa kwa hewa hiyo.
Mlipuko huo husababisha piston kusukumwa kwa nguvu kubwa kushuka chini na chemba za cylinder kubaki wazi ikiwa na hewa chafu iliyochomwa.
4 Pigo la nne
Baada ya piston kushushwa chini,hupanda juu na valve hufunguka ili kutoa ile hewa chafu ndani ya chemba na kuitoa nje kupitia bomba la kutolea moshi.
Baada ya hapo piston hurudia mzunguko wake tena kuanzia pigo la kwanza had la nne.
Piston zinaposhirikiana katika kukamilisha mapigo haya ndio husababisha kuizungusha crank shaft na kusababisha mwendo wa gari.