Ijue piston: Elimu haina mwisho

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Piston ni sehemu ama kifaa mojawapo katika engine ya gari ,ambacho hutumika kudhibiti hewa na mafuta ndani ya cylinder.

Pia kutoa nguvu itokanayo na kuungua kwa mafuta kupitia connect rod hadi kwenye crank shaft.
Piston hufanya kazi kwa ushirikiano katika engine na kusababisha kuizungusha crank shaft. Crank shaft inapozunguka hupeleka nguvu katika gear box hadi kwenye diff kupitia poropela na hatimaye tairi kutembea.

Piston inapopanda juu na kushuka chini
Hatua hii husababisha mapigo manne ndani ya chemba za cylinder.
1 Pigo la kwanza piston inashuka chini. Kitendo hiki huruhusu valve kuingiza hewa safi au hewa iliyochanganywa na fuel. (inategemeana na injini kati ya petrol au diesel)

2 Pigo la pili piston inapanda juu
Kitendo hicho kinasababisha ile hewa safi iliyo ingia kwenye chemba kukandamizwa kwa mgandamizo mkubwa sana na hewa hiyo kuwa na joto kubwa sana, kisha plug inatoa cheche au nozeli inanyunyiza mafuta (plug au nozel, hapa inategemeana na engine ya petrol au diesel.

3 Pigo la tatu
Baada ya ile hewa yenye joto kali kukutana na cheche kutoka kwenye plug au mafuta kutoka katika nozel husababisha mlipuko mkubwa uliosababishwa na kuchomwa au kuunguzwa kwa hewa hiyo.
Mlipuko huo husababisha piston kusukumwa kwa nguvu kubwa kushuka chini na chemba za cylinder kubaki wazi ikiwa na hewa chafu iliyochomwa.

4 Pigo la nne
Baada ya piston kushushwa chini,hupanda juu na valve hufunguka ili kutoa ile hewa chafu ndani ya chemba na kuitoa nje kupitia bomba la kutolea moshi.

Baada ya hapo piston hurudia mzunguko wake tena kuanzia pigo la kwanza had la nne.
Piston zinaposhirikiana katika kukamilisha mapigo haya ndio husababisha kuizungusha crank shaft na kusababisha mwendo wa gari.

FB_IMG_1634069267737.jpg
 
Kwa engine za pikipiki zenye piston moja, mzunguko wa crankshaft unasababishwa na kitu gani? Ni sawa na baiskeli yenye pedal moja. Zenyewe zina mapigo manne vile vile?
 
Hiyo ni 4 stroke engine Ndio ina mapigo 4, ila kwa 2-stroke engine iwe ni diesel au petrol pigo la 1 na 2(kuvuta mafuta na kuchanganya na hewa safi) pigo 3 na 4 ( kuyachoma na kutoa hewa chafu). 2 stroke engine hivi vitendo hufanyika kwa wakati mmoja.

2-stroke ndio engine yenye nguvu, siku za karibuni zitapotea maana kwenye marine outboard engines za petrol watu wa mazingira wanasema zinachafua mazingira na kwenye pikipiki manufacturer wengi wanatumia 4- stroke wakiweka double overhead camshaft (2 inlet valve & 2 outlet valve) kuongeza ufanisi wa kuchoma mafuta na kutoa hewa chafu yote.
 
Kwa engine za pikipiki zenye piston moja, mzunguko wa crankshaft unasababishwa na kitu gani? Ni sawa na baiskeli yenye pedal moja. Zenyewe zina mapigo manne vile vile?
Unasababishwa na ufanyaji kazi wa piston baada ya mafuta kuchomwa na kupatikana nguvu ya kuzungusha crankshaft. Pikipiki zipo zenye mapigo manne (4-Stroke) kama hizi Boxer,TVS,Honda XL na zenye mapigo mawili (2-Stroke) kama Suzuki TS 125, Yamaha DT 125.

Crankshaft huwa inapozunguka kama baiskeli ukikanyaga pedal lakini kwenye injini ya pikipiki pembeni ya crankshaft Kuna kifaa kinaitwa flywheel hiki kina umbo la duara husaidia kutunza nishati na kumaintain ule mzunguko uwe vile vile wakati piston ikiwa kazini.
Kama isingekuwapo flywheel ingekuwa pikipiki inaenda kwa kusua sua( Nimekosa maneno sahihi ya kiswahili kuelezea Uzuri tusameheane mkuu).
 
Nimekuelewa zaidi ya maelezo mkuu. Na umetegua kitendawili changu. Nimekua nikijiuliza sana hili jambo, piston moja inafanyaje kazi? Kitu gani kinairudisha juu? Kumbe hilo gurudumu ndio linakua linahifadhi nguvu ya kuendeleza mzunguko, inamaana linachukua nafasi kama piston ya pili right?

Ahsante sana kwa maarifa ndugu yangu.
 
Unasababishwa na ufanyaji kazi wa piston baada ya mafuta kuchomwa na kupatikana nguvu ya kuzungusha crankshaft. Pikipiki zipo zenye mapigo manne (4-Stroke) kama hizi Boxer,TVS,Honda XL na zenye mapigo mawili (2-Stroke) kama Suzuki TS 125, Yamaha DT 125.

Crankshaft huwa inapozunguka kama baiskeli ukikanyaga pedal lakini kwenye injini ya pikipiki pembeni ya crankshaft Kuna kifaa kinaitwa flywheel hiki kina umbo la duara husaidia kutunza nishati na kumaintain ule mzunguko uwe vile vile wakati piston ikiwa kazini.
Kama isingekuwapo flywheel ingekuwa pikipiki inaenda kwa kusua sua( Nimekosa maneno sahihi ya kiswahili kuelezea Uzuri tusameheane mkuu).
Kumbe jina lake ni Flywheel. Mafundi wangu waliita Furawili/Frawili.

Asante nimeongeza msamiati
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom