LENGISHO
Senior Member
- Sep 15, 2017
- 169
- 265
MISINGI NA HAKI ZA BINADAMU
Haki ni ustahili wa kupata kitu, hivyo mtu ana haki kama mtu hyo anastahili kutenda katika uelekeo Fulani au anastahili kutendewa na watu wengine. Mfano unaposema una haki ya kwenda nyumbani unastahili kwenda nyumbani na mtu mwingne hawezi kukukataza au kukuzuia kwenda nyumbani.
Haki inaweza kuwa ni ya mtu mmoja au makundi, Mfano mfanyabiashara Vs wafanyakazi katika chama cha wafanyakazi , wana haki ya kuwa huru bila kuachishwa kazi kwa nguvu au ghafla na hii inatambulika kisheria , vivyo hivyo jamii ina haki za jumla kama vile haki ya Kumiliki Ardhi, Haki ya kupata elimu n.k
ZIFUATAZO NI MISINGI YA HAKI HAKI ZA BINADAMU
1. Hazihamishwi wala kutenganishwa (Universality and inalienability): Watu wote kila , Haki hizi haziwezi kunyang’anyika. Hawezi kumnyang’anywa haki yako. Haki hii imefafanuliwa na kuonyeshwa katika kifungu cha 1 katika tamko la haki za binadamu “All human being are born free and equal in dignity and right”.
2. Hakuna kubwa wala ndogo ( Indivisibility): Yaweza kuwa inahusiana na siasa, uchumi, utamaduni au kijamii , Haki za binadamuu zinarithishwa kwa kila utu wa mwanadamu ( Hakuna haki kubwa wala yenye umuhimu zaidi ya nyingine).
3. Usawa na Hazibagui ( Equality and Non- discriminatory): Binadamu wote ni sawa na Mtu yeyote hawezi kubaguliwa au kumbagua mtu kutokana na jinsia, rangi ,kabila, taifa, umri , dini, ulemavu, n.k kama ilivyoainishwa katika tamko la haki za binadamu
4. Uwajibikaji na Utawala wa Kisheria ( Accountability and Rule of Law): Nchi na Viongozi wengine wanawajibika kuangalia kila binadamu anatendewa haki . wanapaswa kufuata sheria na misingi ya haki mbalimbali za kimataifa na kitaifa. Raia/ mwananchi, vyombo vya habazi Asasi Zisizo za Kiserikali ( AZISE) na mashirika ya kimataifa wanawajibu na nafasi kubwa ya kuziwajibisha serikali katika kuhaikisha kuwa haki hizi zinatimizwa.
5. Haki zinaingiliana na Kutegemeana ( Interdependence and interrelatedness ): Kila haki inachangia katika kutimiza utu wa binadamu kupitia kuridhika kimaendeleo, Kisaikolojia, Kiuchumi, mahitaji ya kiroho n.k Utekelezaji wa haki moja unategemea sana njia moja au nyingine ya utekelezaji wa haki nyingne. Kwa mfano, utimizaji wa haki ya Afya unategemea utimizwaji wa haki ua kuendelea, kupata elimu , kupata taarifa na kadhalika.
6. Kushiriki na kujumuika ( Participation and Inclusion) Watu wote wanahaki ya kushiriki na kupata taarifa kuhusiana na maamuzi na masuala yanayohusu ustawi wa maisha yao ya sasa na ya baadae.
Vile vile tamko la haki za Binadamu linampa haki raia na kuamuru uwajibikaji toka kwa nchi na serikali zake kutimiza wajibu wake. Tamko pia limehakikishwa na linalindwa na sheria za kimataifa
HAKI NA SHERIA ZA RAIA KAMA ZILIVYOAINISHWA
1 Haki inapatikana ndani ya sera za serikali, sera ya elimu na Mafunzi ya mwaka 1995inasema “ Serikali itahakikisha kupatikana kwa elimu ya awali, elimu ya msingi na elimu ya watu wazima kwa wananchi wote kama haki ya msingi ( Kifungu cha 3.2.1 Ukurasa wa 18 )”
2. MKUKUTA ilikuwa iinahamasisa ahadi ya sera katika malengo kama “Ugawaji sawa wa rasilimali za umma na kushughulikia tatizo la rushwa ipasavyo” Nguzo 3> lengo2).
3. Haki inasimama katika sheria inaitwa haki ya sheria , hizi ni haki zinazotokan na sheria ambazo huruhusu kumpa uwezo mtu kutenda kwa mwelekeo Fulani au kuhitaji kutendewa na wengine
4. Haki za kisheria ni haki zilizotokana na sheria mama za nchi ( Katiba). Katiba ya nchi ni msingi wa sheria za nchi . Mfano wa sheria zinayohusu haki za mwanadamu/raia wa Tanzania ni katika katiba ya Tanzania sehemu ya tatu ‘ Haki wajibu Muhimu IBARA ya 12,13,14,15,18,17,18,19,20,21,22, mpaka ibara ya 30 inaelezea haki za mwanadamu/raia