itel Mobile ni kampuni ya masuala ya teknolojia na uvumbuzi ambayo imejikita hasa kwenye masuala ya utengenezaji wa simu tangu ianzishwe mwa 2007.
Kutoka mwaka 2007 mpaka sasa ni miaka 10, kampuni hii ilianza na simu za batani na kufikia miaka ya 2010 ilianza kutengeneza smartphone, ambapo mpaka hivi sasa kuna simu aina nyingi za smartphone. Ambapo ziko simu kwaajili ya picha nzuri yaani kamera mfano itel S11, itel S31 pia zinazotunza chaji zaidi ya siku tatu huku ukiitumia kadri uwezavyo na uwezo wa kuchaji simu nyingine kupitia OTG function mfano itel P51 na Itel 1556
itel S11 itel S31 itel P51
Kitu cha pekee kabisa kampuni hii imekuwa ikijali wateja na kutoa huduma kwa watu wa viwango vyote vya kiuchumi au kipato kuanzia kipato cha juu mpaka cha chini. Bidhaa za itel mtu yeyote anaweza kukidhi gharama zake tofauti na makampuni mengine.
Lakini pia kupitia idara ya uhusiano, itel mobile kwa Tanzania imekuwa msaada mkubwa kwa makundi mbalimbali katika kujitolea misaada mbalimbali, shuleni, kwenye vituo vya watoto yatima na watu wenye mahitaji maalum.
Kila unaponunua simu ya itel unapata warantii mwaka mzima na hapa simu yako ikileta hitilafu unaweza kupeleka kwenye vituo vya matengenezo CarlCare Service Centers ambavyo viko mikoa ifuatayo:
1. Dar es Salaam kituo kipo Posta mtaa wa Samora jengo la NHC ghorofa M na Kariakoo mtaa wa Msimbazi jengo limeandikwa CarlCare karibu na kituo cha Polisi Msimbazi
2. Arusha kituo kipo mtaa wa Zaramo mkabala na stendi ya mabasi ya mkoa ni ghorofa ya 3.
3. Mwanza kituo kipo Mtaa wa Rwagasore Jengo liko ploti namba 93 Ghorofa ya pili.
4. Dodoma kituo kipo Mtaa wa Uhuru jengo namba 8, ploti namba 27 ghorofa ya kwanza.
5. Mbeya kituo chetu kipo Mwanjelwa jengo la Kabwe ghorofa ya kwanza.
2007-2017 itel 10 Years Cheers!