Town Hustler
JF-Expert Member
- Oct 25, 2016
- 277
- 367
Hapa Tanzania kuna sehemu ukienda na ukapewa historia zake unaweza kubaki mdomo wazi, kwa kuwa ukiangalia mji huo kama hauendani na hiyo historia. Lakini kimsingi kuna miji hapa Tanzania kwa kweli imebarikiwa kuwa na historia ya kusisimua. Moja ya mji huo ni Tukuyu.
Tukuyu ni moja ya mji unaopatikana wilayani Rungwe, takribani kuna umbali wa kilomita 68 kutoka Mbeya Mjini, kilomit 67 kutoka wilaya ya Kyela, kilomita 632 kutoka makao makuu ya nchi yaani Dodoma, kilomita 468 kutoka Songea na kuna umbali wa kilomita 858kutoka mji mkuu wa kibaishara Dar es Salaam.
Ukiwa hapo Tukuyu unaweza kufika maeneo kama Bagamoyo na Tukuyu Stendi. Hali ya hewa katika eneo hili ni baridi sana ukizingatia Tukuyu ni moja ya sehemu inayopatoka nyanda za juu kusini. Kwa wakati wote mji wa Tukuyu unakuwa wa kijani na hii ni kutokana na uwepo wa mvua kwa mwaka mzima.
Wakazi asilia wa mji huu wa Tukuyu ni Wanyakyusa waliopata kufika hapo miaka mingi sana hata kabla ya 1800 wakitokea huko Malawi. Ambapo huko Malawi wanafahamika kwa jina la Wakhonde kutoka mkoa wa kaskazini mwa nchi ya Malawi. Japo kumekuwa na masimulizi mengi sana juu ya kabila la Wanyakyusa. Lakini kuanzia miaka ya 1900 hapo Tukuyu kulikuwa na ujio wa makabila mengine yaliopata kutokea sehemu mbalimbali. Ikiwa na maana kwamba sasa mji wa Tukuyu unapata kukaliwa na watu kutoka makabila mengine yanayopatikana hapa Tanzania.
Na inapata kusimuliwa kuwa, watu wengi walikuja kwa sababu za kisiasa hasa uwepo wa wakoloni wa kijerumani tangu 1885 na hawa walitoka huko Pwani, yaani Bagamoyo, Pangani na Tanga, na pia uwepo wa biashara, hapa tunawazungumzia wakazi kutoka Makete, yaani Wakinga.
Ukifika hapa Tukuyu utapata kuona makazi ya watu yakiwa juu ya milima ambayo mengi yao yamejengwa kwa matofari ya kuchoma.
Ukiachilia mbali habari hizo, ukifika hapa Tukuyu utapata kuona wakulima wa Chai inayolimwa kwenye milima na utapenda kuona namna inavypovunwa. Lakini pia kilimo cha ndizi utaweza kukiona hapo, na ukifika tu hapo stendi utawakuta wakina mama na wakina baba wamejipanga wakiuza nafaka na matunda mbalimbali yakiwemo maparachichi na ndizi. Hakika mji wa tukuyu ni moja ya mji ambao unavutia sana.
Ukija upande wa utalii kuna mambo kibao ya kuvutia. Kwanza ukiwa unaingia Tukuyu mjini hapo mwanzoni utakutana na mtaa au eneo linaitwa Bagamoyo, hapo utapata kujua historia adimu sana ya wakazi wa mtaa huo.
Lakini pia kuna milima ambayo inapatikana Kaskazini-mashariki na kusini Mashariki mwa mji wa Tuyuku, hasa ule mlima Rungwe ambao ni moja ya mlima wa Volkano iliokufa. Ukienda mbele maeneo ya Masoko unaweza kuona ziwa Kisibha au Kisiba ambalo lipo kwenye mlima na lina maajabu kibao ukipata kufika hapo.
Lakini pia hapo Tukuyu kuna shule ya pili kupata kujengwa na serikali ya mkoloni yaani mwaka 1919. Ifahamike kuwa shule ya kwanza ilijengwa huko Tanga na hivyo shule ya pili ilijengwa hapa Tukuyu. Na sababu ya kujengwa shule hiyo ni kutokana na Wanyakyusa kuonekna kupenda Elimu na kuukubari Ukristo kwa haraka sana.
Hiyo shule inaitwa shule ya msingi Tukuyu na ipo karibu sana na stendi ya mabasi hapo Tukuyu umbali wa mita 10 kutoka hapo Kituo,ukiwa kama unaenda Kyela au mlango wa kuingilia stendi. Ukiachilia mbali shule hiyo, hapoTukuyu kuna Boma ambalo kwa sasa linatumika na serikali,boma hilo ni la Wajerumani, ambalo lilijengwa baada ya kuzama kwa boma la kwanza kwenye ziwa Nyasa boma hilo ambalo lilijengwa miaka ya 1900 lilitumiwa na wajerumani mpaka walipoondoka miaka ya 1919.
Ukiwa hapo Tukuyu boma hilo lipo karibu na Benki ya NMB umbali wa mita kama 40. Kwa ujumla ukiwa hapoTukuyu utafurahia mengi sana hasa wale wapenda nyama choma na ndizi za kukaanga hapa ndio penyewe.
Asili ya jina Tukuyu ni historia ndefu sana, lakini nitakusimulia kwa ufupi sana. Inasimuliwa kuwa mji wa Tukuyu ulipata kuwepo hata kabla ya miaka ya 1800. kwani hata hiko kipindi ambacho Wajerumani wanafika miaka ya 1885, waliwakuta wakazi wa hapo ambao ni Wanyakyusa. Lakini kwa kuwa eneo hili lilikuwa na muonekano mzuri, iliwafanya Wajerumani kuweka makazi yao hapo na kuamua kujenga boma lao hapo.
Na hivyo idadi ya watu kuongezeka siku baada ya siku kutokanana uwepo wa Wajerumani hao ambao nao waliwaleta watu wengi kwa shughuri za kisiasa na kiuchumi. Na inasimuliwa kuwa, hapo zamani kabisa mji wa Tukuyu ulianzia na kukua kwenye eneo ambalo sasa hivi panaitwa mtaa wa Bagamoyo.
Na sababu ya mtaa huo kuitwa bagamoyo ni kwamba, Wajerumani waliwaleta watu wengi kutoka huko pwani ya Bagamoyo. Na ndipo hapo watu hao walipoanzisha makazi yao na mtaa wao au eneo lao likaitwa Bagamoyo. Lakini ikukumbwe kuwa, kabla ya hapo kulishakuwa na makazi ya Wanyakyusa ambao kisingi hata neno Tukuyu linaanzia huko.
Kulingana na masimulizi ya Wenyeji na baadhi ya Wanahistoria wanasimulia kuwa, kuwa neno hili Tukuyu lilitokana na aina ya miti ilioitwa Mikuyu.
Na kutokana na maandiko ya wapelelezi wa mwanzo na mchanganyiko wa watu mbalimbali ndipo kukatokea neno Tukuyu na hata kwenye maandiko ya awali palifahamika kama Tukuyu. Na mpaka leo panaitwa Tukuyu.