Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

hutyo herode si alikuwa mfalme wa Israel Mkuu-na kama ndivyo basi ni dhahiri alikuwa akiongoza weupe wenzake kwa maana hiyo waisrael ni weupe.sasa dhana na ya kuwa waisrael halisi walikuwa weusi inatoka wapi??
Mkuu usiwe zumbukuku unaniangusha.Hayo unayoyauliza yalishajibiwa kwenye thread kadhaa kule jamii intelligence.
 
Ww dini gani? Unataka nikuorodheshee dini ili uchague moja au?
Nitafurahi sana ukifanya hivyo, ila kukupunguzia kazi, Nitajie Dini tatu za kale zaidi katika Historia, Nani nitakutajia moja niliyomo ndani yake
 
Hakuna chochote cha maana ulichoandika ,umeandika kishabiki shabiki kama stori za kijiweni.
 
huyo firauni alifia kwenye bahari pamoja na majeshi yake..biblia ilificha mwisho wake lakini katika uislam kaelezewa vizuri tu.sa kama wewe mtoa mada utawaskiza hawa wanahistoria wa leo au utafuata maelezo ya dini..
suala la mwili kuwa kama sanamu baada ya kufa ni kwamba yeye ndiye mtu wa kwanza kufa na kufanyiwa vile na MUNGU..alifanywa sanamu ili awe fundisho kwa vizazi vyote vijavyo had mwisho wa dunia.hapo ndipo wahuni walipojifunza kukausha marehemu baada ya kufa ili wamhifadhi bila kuoza..
soma deep zaid mkuu
 
postmortem aliyofanyiwa firauni huyo hapo pichani,inaonekana alikufa kwa mibamizo ya maji

uchunguzi wake ulifanyikia ufaransa kama sikosei ni miaka 70 na dr bucaille
 
NIMEITOA FB HII SASA NAIKUBALII AMEENDA KWENYE KEYPOINT.
UKWELI USIOZINGATIWA

Assalaam alaikum warahmatullah wabarakaatuh

Sifa zote njema zinamstahiki Allah tabaaraka wataala,na rehma na amani zimuendee kipenzi chetu na kiigizo chetu chema mtume Muhammad swallallahu alayhi wasallam na maswahaba wake na wote wenye kuwafuata mpk siku ya kiama.

Ndugu zangu leo tuusome ukweli huu kuhusu mal uuni fiaraun ambao wengi hatuujal wala hatuna mazingatio nao.

Firaun alikuwa mfalme aliyetawala taifa la misri.mfalme huyu aliyekuwa anamuabudia shetan alifika hatua ya kujiita mola wa waisrael. Aliwatesa sana huku akiwaua watoto wa kiume kwa hofu ya kupinduliwa utawala wake. Wakat mwingine Allah hufanya jambo lake kupitia adui yake. Baada ya nabii Mussa alayhi salaam kuzaliwa alilelewa na firaun.

Baadae Allah akampa unabii na kumtuma mjumbe wake huyo kwa firaun ili kuwaokoa wana was Israel. Wakat wakiyakimbia majeshi ya firaun Musa na waisrael walifika pwani ya bahar ya red sea alielekezwa na Allah apige fimbo yake bahar na baada ya kufanya jivyo bahar ikajitenga wakapita. Allah anasema

فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانْفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ

Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.

Baada ya kuvuka upande wa pili majeshi ya firaun nayo yakawa yameshaingia na kufik katikat ya bahar. Nabii Musa akawa hajui afanyeje kwa kuwa firaun hakuwa mbali nao. Allah akamwambia akamwambia Mussa alayhi salaam

وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُنْدٌ مُغْرَقُونَ

Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.

Allah akayaangamiza majeshi ya firaun naye pia akaangamia. Baada ya tukio hill ndio ukawa mwisho wa mal uuni huyu yy na jeshi lake.

Mwaka 1898 kwa mara ya kwaza baada ya miaka mingi sana kupita mwili wa firaun ukaonekana kando ya bahar ya red sea nchini misri. Mwili huo ulikutwa haujaoza ,ulikuw kama umeopolewa siku chache. Ikaaminiwa na wamisri kwanba huo sio mwili wa yeyote yule said ya firaun, baadaye ukahamishiwa katika jumba la makumbusho mpk leo .

Mwaka 1981 rais wa ufaransa ,Fransisco mata aliutaka mwili wa firaun kutoka serekal ya misri ili waufanyie uchunguz na wabaini huo mwili ni wa nan na kwann hauozi.

Akaagiza jopo la wanasayans likiongozwa na dokta wa upasuaji( surgeon) bingwa duniani wa wakat huo aliyeitwa professor Maurice bucaille kuufanyia uchunguzi mwili huo. Wanasayans hawa hawakuon dawa wala kemikal yeyote ktk mwili huo inayosababisha mwili huo kutooza kama binadam wengine. Baada ya uchunguzi wao waligundua mwili huo ulikuwa umejaa chumvi nyingi inayothibitisha kuwa uliopolewa baharin. Baada ya njia za kisayansi kufel kupata ukweli kuhusu mwili huo ni wa nani na kwann hauozi ikabid wawahoji viongoz wa dini.

Wakatazama katika biblia na kukuta kuwa ndani ya biblia hakuna mahala popote penye maelezo kuhusu mwili huo. Biblia inasema:
KUTOKA 14 : 27-28

Mussa akaunyoosha mkono wake juu ya bahari na kulipopambazuka ikarudi kwa nguvu zake, wamisri wakakimbilia mbele yake na BWANA akawakukutia mbali hao wamisri kati ya bahar. Yale maji yakarud yakafunikiza magar na wapanda farasi hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahar nyuma yao hakusalia hata mtu mmoja.

Hapo biblia inabainisha kwamba firaun na jeshi lake lote waliangamizwa na hakuna aliesalia.

Swali likazid kuwa gumu na kukosa jibu kwa wanasayansi hao kuwa mwili huo ni wa nan na kwann hauozi????

Ndipo wakashauriwa kuiuliza qur an ( kitabu chetu waislam) ambapo baada ya kuiuliza qur an walijibiwa na kufahamishwa kila walichokuwa wakihitaj. Qur an ikawaambia kwamba huo mwili ni wa firaun na Allah aliamua kuuihifadhi ili uwe Ishara kwa watu watakaoishi duniani zama za mwisho. Allah anasema

فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ
Basi leo tutauokoa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.

Mabwana hawa wakawa wamepata kilichowasunbua kwa muda mrefu lakini kubwa ni kwamba:

Hapa kuna mambo mengi tunajifunza sisi tunaoishi duniani hivi sasa kwa kuwa huyu mtu Allah alimuhifadhi ili awe ishara kwamba yeyote atakaewakadhibisha wajumbe wa Allah mwisho wake ni kuangamizwa( kama ambavyo leo waislam tunavyompinga mtume Muhammad swallallahu alayhi wasallam. Mfano hai:

Mtume swallallahu alayhi wasallam alisema tukiona Majumba yanaenda juu yaani maghorofa tujue ni dalili ya kiama. Leo waislam magorofa tumeyaona lakini tunasema MAENDELEO.

hivi kati ya mtume swallallahu alayhi wasallam na sisi anayeyajua maendeleo nan???

Kwa kauli yake kuwa ghorofa ni dalili ya kiama sie kusema ni maendeleo na baadhi ya misikiti yetu mpk majumba yetu ni ghorofa hapa hatujampinga????

Lengo la kutuambia ghorofa ni dalili ya kiama ni ili na sie tujenge????

Inna lillaah wainnaa ilayh raajiuun

Mtume swallallahu alayhi wasallam tunampenda mdomoni tu lakin mioyoni mwetu hayupo.

Allah anasema tena kuhusu firaaun Laanatullaah alayhi

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِلْآخِرِينَ

Kisha tukawafanya( firauni na waliomtwii) kuwa watangulizi na mfano kwa vizazi vitakavyokuja baadaye( ambao ndio Sisi tuliokuja baada ya firauni Laanatullaah alayhi)

Firauni alikataa ujumbe wa Allah tabaaraka wataala alioletewa na Mussa alayhi salaam. Akawambia watu wake

أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِنْ هَٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ

Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?

Katika tafsir ya ibn kathiir asema Ibnu jariir ( radhi za Allah zimuendee) asema firauni alimaanisha musa alayh salaam hakuwa na jeshi, mamlaka ya utawala na hakuwa na mali sasa vp wafuate ilhal musa alayh salaam hana kitu( choka mbaya)

Watu wakamsikiza na kumkubal wakauacha ujumbe wa Allah mwisho wake wakaangamizwa wote.

Na hata ss wajumbe wa Allah haya ndio yanayowakuta kwa kuwa hawana mali, jeshi wala mamlaka hivyo watu wwanawadharau na kuwachukulia kama waomba misaada. Mfano wetu ni firauni Laanatullaah alayhi.

Allah atunusuru

Inasemekana professor MAURICE BUCAILLE alisilimu akaamua kujifunza na kiarabu na baadae aliandika kitabu kinachoitwa THE QUR AN, THE BIBLE AND SCIENCE akifafanua ukweli na usahihi wa qur an tukufu.

Tukio hili pia ni la ajabu na mazingatio kwa wenye kutafuta haki, mwili wa mtu kutooza mpk leo Kw zaid ya miaka 3000 kupita na mpaka NYWELE zake pia hazijanyonyoka.

Makosa aliyoyafanya mtu huyu ya kujiita na kujinadi kuwa yeye ni Mungu ni makosa makubwa yaliyosababisha Allah akaamua kumuweka ili kila atakaezaliwa hapa duniani amshuhudie mpk dunia itakapomalizika kabisa.

Makosa aliyoyafanya firaaun Laanatullaah alayhi ndio yanayofanywa na viongozi wetu wa sasa. Na wenye jukumu la kukemea ni sisi waislam ( Mashekh, maulamaa kwa kuwa wao ndio warithi wa mitume)

Msiba mkubwa ni kwamba mashekh na maulamaa( WAISLAM) tunayakubal haya ndio maana tu kimyaaaaaa. Na hii ndio moja ya sababu za waislam kupigwa na kudhalilishwa duniani, na mpaka jina zuri wakatuchagulia,saivi wanatuita GAIDI/ MAGAIDI

Ipo siku tutakutana na aliyetupa jukumu la kukemea haya yanayofanyika sijui tutamjibu nn.

Kwa elimu zaid ingia you tube andika zama za mwisho 1

Imeandaliwa na elber mmbaga

0675648283

na

hassan mrisho

0678932949

Niwie radhi kama nitakuwa nimekukwaza ila lengo langu ni kuelimika zaidi. Vitabu vya dini maarufu (Biblia na Quran) kwa nyakati tofauti vinamtaja Farao kwamba aliadhibiwa na MUNGU/ALLAH kwa kukufuru na kujiita mungu, mkuu adhabu aliyopewa ni kuololewa mwili wake kutoka baharini alipozama na majeshi yake na kuufanya mwili wake kutooza ili vizazi vya baadae (tukiwemo sisi) tujifunze.

Kwa akili yangu ndogo nafahamu kuwa Faraoh ni cheo (Mfano Rais, Mfalme, Sultani n.k) na siyo jina kama wengi wanavyofikiri. Mafarao walikuwa wengi maana walikuwa mmoja akifa mwingine anarithi. Swali la kwanza ni Faraoh yupi kati ya mafarao waliotawala Misri alimkufuru MUNGU? (naomba atajwe kwa cheo na jina). Swali la Pili ni kwa nini MU
 
Uwe Muelewa, Hakuna haja ya yrye kuzikwa sasa ili hali watu wanatafuta miili mingine ya Wamisri hao wa kale kwa ajili ya Utalii! Hivyo sababu kubwa ya yeye kutokuzikwa sasa ni utalii..
2. Miili ya Wafalme wa kale wa Misri iliwekwa dawa maalumu iliyowezesha miili yao kukaa miaka mingi bila kuharibika, na yeye Aliwekewa Dawa hiyo, Isitoshe Mwili si wake peke yake uliopo kwenye makumbusho ya misri ya kale! miili ni mingi sana, ya mapharao mbalimbali na mamalkia na yote ipo kama ya huyohuyo Pharao sababu ya dawa zilizotumika katika kuhifadhi maiti..
Mnasema huyu ni pharao wa ||, je,mwili wa pharao wa | hupo?.
 
Uwe Muelewa, Hakuna haja ya yrye kuzikwa sasa ili hali watu wanatafuta miili mingine ya Wamisri hao wa kale kwa ajili ya Utalii! Hivyo sababu kubwa ya yeye kutokuzikwa sasa ni utalii..
2. Miili ya Wafalme wa kale wa Misri iliwekwa dawa maalumu iliyowezesha miili yao kukaa miaka mingi bila kuharibika, na yeye Aliwekewa Dawa hiyo, Isitoshe Mwili si wake peke yake uliopo kwenye makumbusho ya misri ya kale! miili ni mingi sana, ya mapharao mbalimbali na mamalkia na yote ipo kama ya huyohuyo Pharao sababu ya dawa zilizotumika katika kuhifadhi maiti..
Umeeleza vizuri mkuu

Ni ajabu jinsi watu wanavyofungwa macho na imani zao kiasi cha kushindwa kusoma historia
 
Waarabu ni race ya mwisho kuingia hapo Misri baada ya Wayunani-Greeks na kisha Warumi chini ya Alexander the great
Waarabu Race ya mwisho kukaa Misri walitokea wapi hapa Duniani?????

tunajua Wayunani walitoka kwao U-Greek ya leo, Warumi Walitoka- Roma ya leo! na hao waarabu hawakuwa na asili ya kwao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom