Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,720
1,639
Mnaemuita firauni ni babu yenu, wa asili! alikuwa ni Mweusi tii!! jina lake aliitwa Mkuu Ramesses wa II au Sese!

Nimekuwa nikiona habari kutoka kwa watu, kuwa mwili wa Ramesses ll huwa ukizikwa, unarudi juu kesho yake!!!

Hivi hili linawezekanaje!! tena watu wenye akili timamu kabisa wanaamini hili! wenye Degree na PHD!! Kwa kweli ni maajabu makubwa mno haya! hapa utaamini kuwa Binadamu ni dhaifu sana kwenye imani!, na ni rahisi sana kumteka mtu yoyote akili kwa kutumia kivuli cha Dini/Imani..

Leo hii kitabu chochote kitakatifu kingesema Kuiba si dhambi na mtu ili ufike mbinguni ni lazima uwe mwizi, basi tungeshuhudia watu wengi wasomi na wasio wasomi wakiwa ni wevi!! Yote ni kwa sababu binadamu wengi ni weak mno kwenye Imani!

Turudi kwenye maada.

Great ramesses ll alizikwaje?

Mwanzo alizikwa kwenye kaburi KV7 katika Bonde la Wafalme, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la malkia Inhapy.

Miaka mingi baadae waliuhamishia tena mwili kwenye kaburi la kuhani mkuu Pinudjem II. Yote hii ni sababu ya kumbukumbu katika hieroglyphics.

Kutokana na matetemeko yaliyoikumba Giza miaka kati ya miaka 1000 AD hadi 1500 AD vitu vingi vilipotea huku baadhi ya masanamu mengi yakiharibiwa vibaya na matetemeko hayo, na baadhi ya makaburi, majumba, na makumbusho mengine kupotea kabisa!
Huku mwili Wa Great Ramesses ll Nao ukipotea katika matetemeko hayo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Red sea.

Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida.

Pia si mwili wa ramesses ll tu uliopo kwenye makumbusho ya misri, ni miili mingi ya Mapharao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Egypt ya kale.

"Historia yake kwa Ufupi"

Ramesses II, au kwa jina jingine Sese alikuwa ni mfalme wa pili wa Uzao wa 19 wa familia ya kifalme. Na alikuja kuwa miongoni mwa Mapharao wenye nguvu kuwahi kuwepo Misri.

Ramesses II alipewa kiti cha Ufalme mapema kwenye umri wa miaka 20 na akaongoza (kati ya mwaka 1279 BC) hadi alipofariki miaka 67 baadae (1213 BC) kwa maradhi ya mishipa, na ini.
Aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa ni wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya mapharao.

Mbali na Vita Ramses II anakumbukwa mno katika juhudi za utunzaji wa Historia ya Misri katika mahekalu ya Ramesseum pamoja na Abu Simbel.
Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo katika mahekalu haya kwa sanamu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Ramsess kuwa mmoja wa mapharao muhimu wa misri ya kale.

Jeshi la Rammeses lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Meditrenian na Libya pia kutoka Hittites na Nubians.

Pia Alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusign mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga.

Katika historia Ramesses alishindwa vita moja tu! vita inayokumbukwa sana ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria ya leo) ambayo ilifanyika mwaka 1274 BC dhidi Wahiti. Ilikuwa ni vita kubwa iliyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita za kale. Rameses alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake kitu kilichofanya moja ya kikosi kufyekwa chote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Ramesses ikampasa arudi nyuma sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.

Dhana iliyozushwa Juu ya Kifo chake!

Vitabu kadhaa vya Dini kama vile Bible na Quran vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza!
Wao hudai kuwa Ramesses au Sese alifia kwenye maji wakati akiwafukuza waisrael!
Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi! ya kibinadamu!
Moja ya ushahidi ni wa Mwili/mummy wa Sese ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa!
Pia jambo jingine la kujiuliza ni kuwa Kina Musa wakati wakimkimbia Ramesses na kuwa wameshafanikiwa kuvuka bahari, huku nyuma waliwezaje kumuona Ramesses katikati ya kikosi cha askari wa misri akifa maji!? Hayo ni mambo yanayowatatiza wengi, huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa Ramesses mwili wake huwa hautaki kuzikwa!

Huyu Ndo Great Ramesses II au Sese mmoja wa Mapharao Muhimu zaidi Eghypt ya kale na leo katika historia,

Pharaoh.jpg

MWILI WA PHARAO RAMESSES ll / Firauni Uliopo kwenye maonyesho ya Ancient Egypt.
RamsesIIEgypt.jpg

SANAMU YA GREAT RAMESSES II ILIYOPO GIZA EGYPT

Nawasilisha
Secret Star
 
Hata Yesu Kristo mwana wa Yoseph alikuwa mweusi tii na nywere za kipilipili! Na ndio sababu utotoni alifichwa Misri kumkwepa Herode, kama angekuwa mzungu kama tunavyoonyeshwa kwenye sinema huko Misri wasingemficha...ila kwakuwa alikuwa mweusi basi alichangwanywa na weusi wenzanke.

Lugha ya mifano aliyokuwa akiitumia Yesu kwa mujibu wa biblia, asili take ni hapa usukumani...wazungu hawafundushi kupitia mifano ya "mpanzi na mbengu zilizoanguka kandokando ya njia..."
 
Wow asante kwa funzo.
 
kwa hiyo herode alikuwa Muzungu??? na alikuwa katika nchi ipi maana kuna siku nimesoma kuwa hiyo israel na misri walikuwa wanaishi watu weusi
 
Hata Yesu Kristo mwana wa Yoseph alikuwa mweusi tii na nywere za kipilipili! Na ndio sababu utotoni alifichwa Misri kumkwepa Herode, kama angekuwa mzungu kama tunavyoonyeshwa kwenye sinema huko Misri wasingemficha...ila kwakuwa alikuwa mweusi basi alichangwanywa na weusi wenzanke.
Lugha ya mifano aliyokuwa akiitumia Yesu kwa mujibu wa biblia, asili take ni hapa usukumani...wazungu hawafundushi kupitia mifano ya "mpanzi na mbengu zilizoanguka kandokando ya njia..."
kuna mantiki hapa maana kama angekuwa mweupe si rahisi kwenda misri kwa weusi na kama angekuwa mweusi si rahisi kwenda misri yenye weupe
 
hutyo herode si alikuwa mfalme wa Israel Mkuu-na kama ndivyo basi ni dhahiri alikuwa akiongoza weupe wenzake kwa maana hiyo waisrael ni weupe.sasa dhana na ya kuwa waisrael halisi walikuwa weusi inatoka wapi??
Yah ni kweli aisee
 
Mkuu sasa hawa waharabu wamisir walitokea wapi?? na waliwezaje kufanikisha kuwafukuza wenyeji wa hapo hao weusi maana kwa kipindi hicho hao mapharao walikuwa na nguvu sana,so waarabu walifanikiwa vipi kuingia hiyo nchi??:?
Kwani RED INDIANS WA NORTH AMERICA WAKO WAPI? na AUSTRALIA wale watu wa asili wako wapi? MZUNGU NENDA NAE KWA HEKIMA NA BUSARA PAMOJA NA UFAHAMU WA HALI YA JUU. ..
 
Nimekuwa nikiona habari kutoka kwa watu, kuwa mwili wa Ramesses ll huwa ukizikwa, unarudi juu kesho yake!!!

Great ramesses ll alizikwaje?

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Red sea.

Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida.

Secret Star

Ndo umemaliza?

"Ijue Historia ya Firauni na Uongo Aliozushiwa"

Je unaona ulichoandika kinaendana na heading?

Thread kama Bongo Movie.
 
Mkuu sasa hawa waharabu wamisir walitokea wapi?? na waliwezaje kufanikisha kuwafukuza wenyeji wa hapo hao weusi maana kwa kipindi hicho hao mapharao walikuwa na nguvu sana,so waarabu walifanikiwa vipi kuingia hiyo nchi??:?

Kumbuka Waarabu sio wa kwanza kuingia hapo, na Wamisri hao wa kale walikuwa na vituo vya elimu hasa eneo la Alexadria ambalo watu wa mataifa mbalimbali walikuwa wanakuja kusoma hapo, hivyo Waarabu ni race ya mwisho kuingia hapo Misri baada ya Wayunani-Greeks na kisha Warumi chini ya Alexander the great

Hiyo picha hapo chini inaonyesha watu wa race mbili tofauti, hao wanaotahiri ni watu Weusi ambao ndio wenye huo ujuzi na utamaduni, wakiwapa tohara hao wageni watu weupe? Wagiriki, Warumi, Waarabu?

image.jpg
 
Ndo umemaliza?

"Ijue Historia ya Firauni na Uongo Aliozushiwa"

Je unaona ulichoandika kinaendana na heading?

Thread kama Bongo Movie.
Kama uko sawa unaweza kutambua vyema kabisa kuwa nilikuwa namaanisha Uongo aliozushiwa juu ya kifo chake, kama una shida kidogo za kiimani huwezi kuelewa, utaona nimeandika Bongo Movies au Futuhi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom