Ijue historia fupi ya chakula aina ya Bacon

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,663
215,530
1572510549999.jpeg

Bacon ni nyama iliyowekwa chumvi, mara nyingi nyama hii hutoka tumboni au mgongoni mwa nguruwe. Huliwa kama chakula cha nyongeza hasa katika kifungua kinywa

Utaratibu wa kuhufadhi nyama hasa ya tumboni kwa nguruwe ilianza miaka 1,500 iliyopita na waanzilishi walikuwa Wachina.

Wakati huo ufugajivwa nguruwe haukuwa kawaida. Ufugajivwa nguruwe duniani ulianza miaka 500 iliyopita.

Wachina waligundua njia hii ili kuweza kuhifadhi nyama baada ya mawindo mazuri ya nguruwe mwitu.

Sikuhizi utamaduni wa kula bacon kama sehumu ya kifungua kinywa umeenea sana hasa Ulaya Magharibi.

Jina bacon lilianzia Ujerumani na Ufaransa likimaanisha 'backside at buttock of a pork'
 
Asante kwa kuleta mada ila tu historia yako si sahihi. Heri kutaja vyanzo unapochukua elimu yako.
Naangalia hapa wikipedia ya Kiingereza (kwa sababu wanataja vyanzo vya kitaalamu katika makala), soma Domestic pig - Wikipedia.
Utaona kuna usahhidi nguruwe walifugwa tangu angalau miaka 10,000.

Kwa watu wanaojua Biblia itoshe kukumbuka Luka 8, 32-34 tunapoona nguruwe walifugwa katika makundi makubwa. ("34 Watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe waliona yaliyotokea, wakakimbia wakaeneza habari ")
Vile vile Luka 15 ,15 , mfano wa mwana mpotevu aliyepaswa kuomba kazi ya kulisha nguruwe.

Kumbe hii dunia miaka 2000 iliopita, ufugaji wa nguruwe ulikuwa kawaida kabisa katika mashariki ya kati (mazingira ya Palestina), hata kama sheria za Wayahudi zilikataza ulaji wa nyama hii.

Msingi wa bacon ni mbinu wa kuhifadhi nyama (yoyote, pia samaki) katika chumvi inayoua bakteria na kuzuia kuoza. Pamoja na kutia chumvi kuna pia desturi ya kuweka nyama (baada ya kutia chumvi) kwenye moshi ya moto inayoimarisha kinga cha wadudu ambako inapokea ladha fulani inayopendwa na watu wengi.

Mbinu hizi zinatumiwa pia kwa nyama ya kila aina (pamoja na ng'ombe, kondoo, nyamapori) na samaki, hata kwa jibini.
 
Ufugaji wa Nguruwe Umeanza miaka 500 iliyopita? Labda Tanzania. Wenzetu wameanza kufuga nguruwe toka miaka zaidi ya 2000 iliyopita. We unasema 500? Uliza vizuri aliyekusimulia.

View attachment 1249733

Bacon ni nyama iliyowekwa chumvi, mara nyingi nyama hii hutoka tumboni au mgongoni mwa nguruwe. Huliwa kama chakula cha nyongeza hasa katika kifungua kinywa

Utaratibu wa kuhufadhi nyama hasa ya tumboni kwa nguruwe ilianza miaka 1,500 iliyopita na waanzilishi walikuwa Wachina.

Wakati huo ufugajivwa nguruwe haukuwa kawaida. Ufugajivwa nguruwe duniani ulianza miaka 500 iliyopita.

Wachina waligundua njia hii ili kuweza kuhifadhi nyama baada ya mawindo mazuri ya nguruwe mwitu.

Sikuhizi utamaduni wa kula bacon kama sehumu ya kifungua kinywa umeenea sana hasa Ulaya Magharibi.

Jina bacon lilianzia Ujerumani na Ufaransa likimaanisha 'backside at buttock of a pork'
 
Baba Koni kawaje chakula......kweli baba Koni kaharibika hivi ....hakuaga hivyo huko nyuma
 
Wakati huo ufugajivwa nguruwe haukuwa kawaida. Ufugajivwa nguruwe duniani ulianza miaka 500 iliyopita.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom