Ijue Haki Ya Kumiliki Mali

DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
337
Katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sehemu ya Tatu kifungu cha 24 (i) na (ii), katiba inaelezea haki ya kumiliki mali na pia haki ya kulindwa kwa mali.
kinasomeka hivi :-

“ 24.(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu
anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.”

“ 24 (2) Bila ya kuathiri
masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang'anywa
mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha
au madhumuni mengineyo bila ya idhini
ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili".

Hivyo ndugu wanajf Mali zetu zinalindwa kikatiba lakini Tusisahau kuwa na Vielelezo vya umiliki wa hizo mali .

Swali Chokozi ....
Je walioficha sukari wana haki ya kufanya hivyo ? .
 
Back
Top Bottom