Dseni
Member
- Aug 13, 2012
- 36
- 42
IGUNGA: HII NDIYO MBINU MPYA YA KUTUIBIA WALIPA KODI WA ARDHI?
Nasikitika kuwaambia kuwa kuna mbinu mpya ambayo mimi naona kama imebuniwa kwa ajili ya kuwaibia wananchI-Wazalendo wa wilaya ya Igunga kuhusu malipo ya kodi ya ardhi.
Ninacho kiwanja kimoja pale Igunga.
Leo tarehe 21.02.2020 nilienda kwa ajili ya kulipia kodi ya ardhi baada ya kusafiri kwa muda mrefu na kushindwa kulipia kodi ya ardhi hiyo tangu 2018 hadi 2020. Nilipoenda niliwaambia nataka kulipia; na nikaambiwa NIPELEKE RISISTI ZOTE NILIZOWAHI KULIPIA TANGU NINUNUE KIWANJA HICHO.
Nikawaambia kwamba mimi sikumbuki niliweka wapi risiti ya malipo hayo, lakini ninayo risti ya mwisho kulipia ambayo ni mwaka 2017. Lakini afsa alikataa kwamba yeye hawezi kurekebisha deni hilo mpaka risiti zote zipatikane na zitumwe ofisi ya Mkoa kwa ajili ya kuthibitisha. Mimi nilipata mshtuko baada ya kusikia hivyo! Ni kwa mara ya kwanza naambiwa nipeleke risiti zote! Baada ya kuona hivyo nikawa nimeingiwa na maswali kwamba;-
a) Je ni halali kwa halimashauri kuniomba risti zote za malipo ya zamani ilihali hata wao wanazo nakala? kwa nini wasiangalie kwenye nakala zao za awali-ndiyo maana nasema ni mbinu mpya ya kutuibia.
b) Pesa tunayolipa kwa kawaida tunaenda kulipia bank (NMB)- Sasa kwa nini wasiende NMB wakusanye bank statement na wachambue ni nani kalipa au la? Mazingira ya kuomba risiti zote ni kutuibia.
c) Je kwenye risti zao hakuna sehemu wamesema “tunza risiti.” Sasa kama hakuna tahadhari ya kutunza risiti, au wanataka kutumia mwanya huu kutuibia tu?
Baada ya muda siyo mrefu afsa mmoja aliyesaini kwa jina la MUSA YOSIA NKINDWA aliniletea “assessement” ambayo inaonesha kwamba sijawahi kulipia ardhi hiyo tangu mwaka 2008 mpaka leo, na kwamba ninadaiwa Tsh 730,000/=
Kinachonishangaza ni kwamba mimi nimekuwa nikilipia tangu nilipokinunua kiwanja hiki tatizo ni kwamba sina risti zote-sasa huyu ndugu eti amekataa hata mwaka niliolipia kwamba eti yeye hana mashine ya kurekebisha deni. Eti as long as ninadaiwa-basi nahitaji kulipa tu hakuna namna. Yaani anaongea bila hata kupepesa macho. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba ninayo risti ya mwaka 2017. Nilimwambia kwamba yeye haoni kwamba mimi nimeshalipia huko nyuma kote? Je NIMEWEZAJE KUPATA RISTI YA MWAKA 2017 kutoka ardhi Igunga-Ikiwa SIKULIPA KULE NYUMA? Haingii kwenye akili hata kidogo.
Baadaye niligundua kitu kimoja:-
a) Inaonekana kwamba hapo zamani pengine walikuwa wanatupiga tu pesa na wala ilikuwa haiingizwi popote pale.
b) Kwa sasa wanataka kufidia madeni yao kwa kutukandamiza sisi kwa kisingizio cha mfumo mpya wa malipo.
c) Wanatumia mgongo wa raisi wetu kwamba hapa kazi tu kwa ajili ya kudhulumu wananchi wa kawaida.
Mimi naona watendaji wa namna hii:-
a) wanakatisha tamaa walipa kodi-mtu anaamua kuacha kulipa kodi kwa sababu ya uonevu
b) bado wana elementi za kupokea rushwa-kwa sababu huwezi kunilazimisha mimi pesa ambayo tayari nilishalipa-eti nilipe tena. hiyo kitu haiwezekani.
NAOMBA KUJUA KAMA HICHI KILICHOTENDWA NI HAKI AU SI HAKI. NA JE NAWEZA KUFANYAJE ILI KUTATUA SHIDA HII?
WATU TUNAYO NIA YA KULIPA KODI-LAKINI WAKUSANYAJI WA KODI HAWATUPI USHIRIKIANO.
NAHITAJI MSAADA TAFADHALI
Mimi mwananchi.
0769080629
Risiti ya malipo
Sent using Jamii Forums mobile app