kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
Leo kuna upigaji kura ya maoni ya kuteua atakaye peperusha Bendera ya CHADEMA kwa nafasi ya Ubunge jimbo la Igunga, ninapenda kuchukua nafasi hii kuelezea hali halisi na kinachotaka kufanyika hapa Igunga.
Kuna njama za makusudi zimepangwa na kuratibiwa na baadhi ya viongozi ili kuhakikisha Mwl.Kashindye apati nafasi ya kugombea Ubunge kwa awamu hii akiwemo na kiongozi mkubwa aliyejitanabaisha kuwa ana mapenzi na CHADEMA Igunga .
Ikumbukwe Mwl. Kashindye alijiondoa kwenye utumishi wa Umma kama Mkaguzi wa Elimu Wilaya na kuingia kwenye Siasa huku akipoteza rasilimali zake, muda wake na kujiweka kwenye hatari kwani CCM hawakuwa tayari kumuona yupo kwa jinsi alivyoichachafya wakati wa uchaguzi mdogo.
Kinachosikitisha na kuhudhunisha ni baadhi ya viongozi wanadiliki kuweka wazi na kusema Mwl.kashindye kwa sasa hana fedha hivyo hata wakimpitisha hataweza kushinda huku watu hao hao wakiwa hawana kumbukumbu kuwa waliweza kushinda nafasi walizopo sasa bila wao kutumia fedha isipokuwa ni wanachama na wananchi walio na mapenzi mema na CHADEMA ndio walijitolea mali zao kukichangia chama hadi kufanikisha kushinda nafasi hizo.
Napenda kutoa angalizo kwa uongozi makao makuu wawe makini sana na suala hili hapa Igunga kwani kukua kwa kasi kwa CHADEMA Igunga hasa wakati wa uchaguzi Mdogo wa Marudio haikuwa kwa sababu eti CHADEMA kilipendwa au kinapendwa sana, sababu kuu ya yote hayo ilitokana na ujio wa Mwl.kashindye kwa kujitoa kwenye utumishi wa umma na kuamua kugombea Ubunge kwa lengo la kuwakomboa wana Igunga kwani alipata support kubwa sana kutoka kwa watumishi wa Umma na hasa walimu kwani hawakuwa tayari kumuangusha Mwalimu mwenzao na pia ni huyu huyu kashindye aliyefanya kazi ya Ziada kama mwenyekiti wa CDM Wilaya kuweza kufanya kampeni zilizozaa matunda ya Igunga kupata viti vingi vya wenyeviti wa Vitongoji na vijiji katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ni vema ikaeleweka wazi hawa vijana waliokuja kugombea sasa wote sio wenyeji wa Igunga na hawaishi Igunga, mmoja anakaa Kahama na mwingine anaishi Dar es salaam na wananchi wa Igunga kwa sasa wameweka wazi hawako tayari kumchagua mtu anayetoka mbali na kuja kupitia Ubunge na kutokomea zake pasipo kuwa pamoja na wananchi kwenye shida na raha.
Kwa Igunga napenda kuweka wazi kama jina la Mwl.Kashindye alitapitishwa ni vema Uongozi makao makuu ukafanya mapinduzi ili kurejesha jina lake kwani pasipo kufanya hivyo CHADEMA itakuwa imejiondoa rasmi kwenye ushindani na itapoteza nafasi za huo Ubunge na hata udiwani kwani wananchi hawatakuwa na imani tena kwa chama kwani itakuwa imeonyesha kutothamini mchango pale mtu anapojitoa kwa moyo wake wote kwenye chama.
Nawasilisha!!