IGP Sirro: Polisi haitumikii siasa

IGP Sirro: Polisi haitumikii siasa

Huyu mzee hajielewi huyu..hata jukumu lake la ulinzi wa raia halijui..anasema yeye ataangalia usalama wa nchi..ukisema usalama wa nchi ni pamoja na mpaka mipaka yake na kulinda adui asiingie nchini akatushambulia akatuteka....
Hiyo sio kazi yake..hii ni hatari kama kiongoz mkubwa kma sirro kutokujua majukumu yake na mipaka yake ya kazi..ndomaana anashindwa kuongea akiwa na ujasiri kwasababu ni liongo..
Vyeo vya kupewa huwa vinashida sana..ameonyesha ukilazaa.a wake na hii inaonyesha ni namna gani wanatumiwa kisiasa na kulishushia heshima kundi letu la polisi(sio jeshi la polisi hawana hadhi)..
Ni ngumu sana kujitenga na ukweli ambao Upo real..shame on U Saimon padre
 
Hivi polisi wa Tz wanapata faida gani kwa kuukandamiza upinzani? Wanai support CCM kwa sababu maisha yao ni mazuri na hawahitaji mabadiliko au ni nini? Kwa nn wasitende haki tu? Imagine unaua raia mwenzio afu unarudi nyumbani na amani kisa CCM, kweli?
 
Mzee wangu IGP Sirro, nawe ni binadamu kama wengine!
 
Siro ajitathimini.
Mfano, kama jeshi la polisi halitumiki na wanasiasa uchwara mbuzi wa CCM ni kwa nini Bashe hajakamatwa kama wabunge na wana CDM wanavyoteswa huko jela kila kukicha!?

Mfano, juzi BASHE ametuhumu TISS na akasema wananchi wake wakichoka watachukua hatua.

Mbona polisi hawajamhoji kuwa hicho kikundi chake kitakacho choka kipo wapi!?
Kitachukua hatua IPI!?
Wapo wa ngapi!?

Maswali ni.mengi sana ukitathimini ubaguzi unaofanywa na viongozi wengi wa serikali dhidi ya upinzani na wananchi wa kawaida.

Tufikie hatua tuwe wawazi , wa kweli na watendaji haki kwa kutii taratibu za nchi.

Siro,. kumbuka Mzee Kova alikuwa nafasi hizo ila juzi alikuwa analialia kuwa sasa hivi hata hakumbukwi, wala simu akipigia watu hawapokei.

Jitafakari baada ya ofisi unaishi na watu huko mtaani ambao ndiyo msaada wako wa kwanza.

Ila kumbuka tu kuwa ,management ya NEC na DED wa kinondoni muda siyo mrefu watagonga hodi pale The Hague, ICC kwa kusababisha kifo cha Binti AAB hapo Jana.
 
Siro sikushangai kwa unafiki huu na huenda una kadi ya ccm mfukoni na unaandaa mazingira ya kupewa cheo cha kisiasa kama Zelote ukistaafu! Usikwepe kusema ukweli juu ya wewe na kikosi chako kukengeuka kutoka kuwa jeshi na kuwa wafuasi na walinzi binafsi wa ccm! Ona Mungu anavyokuchora, polisi wako kaua tena asiye na hatia akiwa ndani ya basi! Hujasema lolote! Iokoe polisi kutoka mateka wa ccm!
 
tutii sheria ndio salama yetu.

Kamwe huto salimika endapo utajaribu kuvunja sheria na amani ya nchi yetu,lazima ushughulikiwe kikamilifu. sote ni watanzania tunahitaji amani na usalama sio fujo.
 
Hahaha hii ingepelekwa jukwaa la Chit Chat au lile la burudani
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Siro, amejibu tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa na kuwaonea viongozi wa vyama vya upinzani, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu juu ya hilo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, IGP Sirro amesema jeshi la polisi halimkamati mtu kwa sababu ni kiongozi wa chama cha siasa au ni kiongozi wa dini, bali humkamata mtu iwapo kuna taarifa za uhalifu zilizowafikia kwani halifuati siasa., hivyo jukumu lao ni kuhakikisha usalama wa nchi.

“Polisi hakamati viongozi wa siasa, polisi hakamati viongozi wa dini, polisi anakamata mhalifu, na mhalifu anapomkamata anamhoji kama kuna ushahidi anampeleka mahakamani, kama hakuna ushahidi anamuachia”, alisema IGP Sirro.

IGP Sirro aliendelea kwa kuwataka wananchi wamuache afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayewajibika na kusimamia amani, na kusema endapo utakamatwa na kukutwa hauna hatia, hawatasita kukuchia huru.

Chanzo: Muungwana
Wewe uliyeleta uzi huu hata kama una elimu ya ngumbalo unaamini yaliyosemwa na IGP ?
 
Mpaka Yesu arudi hii nchi ishalaaniwa baada ya awamu ya nne
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Siro, amejibu tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa na kuwaonea viongozi wa vyama vya upinzani, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu juu ya hilo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, IGP Sirro amesema jeshi la polisi halimkamati mtu kwa sababu ni kiongozi wa chama cha siasa au ni kiongozi wa dini, bali humkamata mtu iwapo kuna taarifa za uhalifu zilizowafikia kwani halifuati siasa., hivyo jukumu lao ni kuhakikisha usalama wa nchi.

“Polisi hakamati viongozi wa siasa, polisi hakamati viongozi wa dini, polisi anakamata mhalifu, na mhalifu anapomkamata anamhoji kama kuna ushahidi anampeleka mahakamani, kama hakuna ushahidi anamuachia”, alisema IGP Sirro.

IGP Sirro aliendelea kwa kuwataka wananchi wamuache afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayewajibika na kusimamia amani, na kusema endapo utakamatwa na kukutwa hauna hatia, hawatasita kukuchia huru.

Chanzo: Muungwana
Nyie endeleeni kujaza wanchi chuki na ujasiri, siku mkigeukwa utaomba po
 
Back
Top Bottom