IGP Sirro, nakutaarifu Dar na Arusha si salama kwa safari za usiku

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,159
9,241
Naomba waraka huu umfikie rafiki yangu ambaye sasa tangu amepanda cheo amekuwa adimu sana,nakumbuka mara ya mwisho tulikutana wiki moja kabla ya kupandishwa cheo na kuwa IGP tukapiga story mbili tatu kisha ukamtania dada niliyekuwa nae...... eenh ushakumbuka. sasa turudi kwenye hoja ya msingi

Mimi nikiwa mmoja wa watu wanaoendesha gari ndogo usiku pia nikiwa mmoja wa watu wenye conection nyingi za wasafiri usiku napenda nikupe ripoti iliclassfied baada ya kuitunza kwa muda mrefu lakin kwa hili la jana hapana ngoja nisifanye siri.

Utekajinyara katika barabara ya dar hadi arusha umerudi upya tena huenda kwa kasi zaid.ikumbukwe sijawahi kuandika taarifa ya uongo au isiyo na uhakika kuhusu barabarani hivyo naomba wahusika walifanyie kazi

utekaji nyara kwa sasa unaanzia msoga pale anapokaa mzee kikwete tena watekaji wa hapa wala hawateki usiku mkubwa wenyewe ni kuanzia saa tano usiku tu hawa huwa wanasilaha za jadi hawana silaha za moto

Wami nalo ni eneo baya kwa sasa kwani usithubutu kabisa pikipiki zikufuate nyuma au ukaona pikipiki moja imekupita kwa kasi maeneo haya tafadhali tafadhali chukua tahadhali, hawa wanapikipiki nne, wanazifichaga pale ambapo askari wako mchana wanajificha kwa kupiga tochi maana askari wako sasa wametengeneza vihandaki flani ili waweze kupiga tochi bila kuonekana

Mkata kabuku hili ni eneo baya kwa kwani hata ukisimama kwa dharula lazima utaona watu wanakujia na mapanga, wanatabia ya kukupiga mapanga na kukuua endapo utasimama kipande chenye giza, ila cha kushangaza beria utaiacha mbwewe na askari wako wote wamejazana pamoja hapa kwenye beria, (kwa kurahisisha hutapishana na gari yoyote ya patrol eneo hili bali utazikuta zimepaki kwenye beria)

Mombo hadi mwanga hapa sasa ndio kiumeni ukipita maeneo haya saa saba saa nane saa tisa au saa kumi usiku kuwa makini sana maana jana tu wenzangu wametekwa pale mkumbara alteza cresta na bmw na spacio zilitekwa baada ya kukuta mawe makubwa kabla ya kufika saweni kwa rasta muuza mirungi (jembe langu) gari hazikuvunjwa sana ila jamaa zangu wamejeruhiwa licha ya gari moja ilikuwa na silaha ya kujihami lakini haikusaidia, hiki kipande unaweza kuendesha gari dakika 30 usipishane na gari wala mbwa. yaani pamenyooka haswa. hivyo kwa usiku kutekwa ni rahis sana na kam ulikuwa hujui watekaji hawakai sehem isiyo na network.

Njoro same hadi mwanga hapa ndio kipande kigumu zaidi kwani miundo mbinu ya barabara sio rafiki mimi binafsi yalikuta hapo njoro na watekaji wa hapa wanasilaha za moto na askari wanaokaa kweye beria ya same ni kama hawako serious yaani gari wanakuwa nayo lakini ukirudi kuwafuata uwaambie twendeni kuna majambazi wameteka magari walinambia subiria pakuche lakini cha kushangaza watekaji au wanaofanya maeneo haya wanajulikana kama kuna mmoja pale njoro ka.........

Igp nimejaribu kuandika kwa ufupi bila kuboa sana ila kusafiri kwangu kote usiku mimi nalitupia lawama jeshi lako la polis haliko serious na patrol, yaani polis utawakuta sehem zenye miji wamepaki eti wako doria wakati ukitoka kilomita mbili nje ya mji unakuta watu wanachezea mashoka. sijui tatizo magari machache au tatizo mafuta au tatizo madereva sijui ila muhimu polis tanzania ikaiga toka kenya maana mabus yanatembea usiku bila kutekwa ila kwa tz suluhisho likaja ni kuzuia mabus kutembea usiku. hapa utasemaje watanzania wako huru kwenye nchi yao.

kuna eneo hili la manyoni hadi tinde nipe muda nikamilishe uchunguzi maana sometime unatamani hata kuwataja kwa majina lakin unashindwa kwa kuhofia kufichuliwa.

la mwisho kwa wale wanaosafiri jion toka arusha na moshi kuelekea dar nyie nawapa pole sana maana mko kwenye hatari kubwa sana ya kushambuliwa nyinyi na magari yenu,.
 
Sijui tunakoelekea hakika kwa hilo jibu la askari, eti subiri kuche/asubuhi"

Mimi nikiwa dodoma kituo kikuu nikiwapa taarifa za kupotelewa na mtoto walinipa jibu ambalo nilikasirika na nilitamani NIMTUKANE huyo afande.

>>Otheryz hapa kwetu bongo naona kama bado tunafuga uzembe, mfano bus kuzuiwa chalinze lisiende Dar kisa zaidi ya saa 23:00 marufuku..!! SIJUI.
 
Sijui tunakoelekea hakika kwa hilo jibu la askari, eti subiri kuche/asubuhi"

Mimi nikiwa dodoma kituo kikuu nikiwapa taarifa za kupotelewa na mtoto walinipa jibu ambalo nilikasirika na nilitamani NIMTUKANE huyo afande.

>>Otheryz hapa kwetu bongo naona kama bado tunafuga uzembe, mfano bus kuzuiwa chalinze lisiende Dar kisa zaidi ya saa 23:00 marufuku..!! SIJUI.
kipimo tosha cha jeshi letu kuwa dhaifu ni pamoja na kuzuia mabus kusafiri usiku
 
Back
Top Bottom