IGP Sirro itupie jicho ofisi ya RPC Kilimanjaro

Mangi Mkubwa

Senior Member
Jan 3, 2014
107
29
Mkoa wa Kilimanjaro kwa sasa unasimamiwa na Simon Maigwa akiwa ndo Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa na tabia kwa baadhi ya Wafanyabiashara na watu maarufu pindi anapoingia RPC mpya kufika ofisini kwake na kuanza kutengeneza mazingira ya mahusiano naye kwa kutoa rushwa ili kuficha maovu yao.

Leo sitakwenda huko zaidi nitajikita kwenye sakata la Mfanyabiashara Izack Ngowi kujeruhi kwa risasi. Izack alishambulia moja ya kijana ambaye ni mfanyabiashara Mjini Moshi, kwa risasi December 31 mwaka jana (2021), na kumjeruhi eneo la bega.

Tukio hili limeibua sintofahamu nyingi kwa kuonesha kuwepo kwa uonevu unaofanywa na Jeshi la Polisi, kwa vijana waliokuwepo siku ya tukio na kupinga kitendo hicho kukamatwa na kuswekwa ndani na kupewa kesi mbalimbali huku wengine wakitisiwa kupewa kesi za armed robbering.

Kabla ya tukio la December 31, la kushambulia na kujeruhi IZACK NGOWI alikuwa na matukio kadhaa ya kutishia na matumizi mabaya ya Silaha lakini hakuna sehemu yoyote yaliripotiwa wala kufikishwa mahakamani.

Nakumbuka November 27 saa kumi usiku IZACK alifyetua risasi kadhaa hewani katika eneo la Redstone Mjini Moshi ukiwa ni ugomvi wa kugombania mwanawake, na tukio hili wapo waliofika kuripoti kituo cha Polisi Moshi,Je Izack alipandishwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Silaha ?na kama hakufikishwa ni nini kilizuia kufikishwa mahakamani na ilikuwaje akarejeshewa silaha yake?ni maswali ambayo yanaendelea kuleta wasiwasi na ofisi ya RPC Maigwa ambayo tunaomba IGP aimulike kwa ukaribu.

Tukio la kushambulia na kujeruhi lilitokea mwezi December mwishoni tunaweza kusema lilitokana na uzembe wa Jeshi la Polisi ikiwemo ofisi ya RPC, kwani IZACK angekuwa hajarejeshewa silaha ambayo alishaonesha kuitumia vibaya angetumia nini kujerushi December 31?na kama angekua ameua jeshi la polisi lingeeleza nini uma?

Kwa sasa IZACK amekwishapandishwa mahakamani, na yupo nje kwa Dhamana, lakini kinachoendelea ni ukamataji wa ovyo na wa maelekezo unaofanywa na Jeshi la Polisi pamoja na kuzuia dhamana ambayo ni haki kwa raia, huku taarifa zilizopo ikiwa ni maelekezo kwa vijana wote ambao walikuwepo siku alipofanya shambulizi na kuonesha kutokuwa upande wake.

Yapo matukio mengi ambayo yanaendelea katika Ofisi ya RPC ambayo tutaendelea kuyaanika hapa ikiwemo baadhi ya vigogo wa jeshi hilo ambao wana ukaribu zaidi na mfanyabiashara IZACK ambao wanaendelea kupaka matope jeshi la polisi.
 
Kwa sasa wamesamkamata na kumhoji kijana aitwaye Ibra Ismail anayefanya kazi kwenye duka la Tumaini Shirima hapo stendi kuu ya mabasii,RPC anasema kijana yule alikii kufyatua risasi na kuhaibu gari la Izack,huu ni mpango maalumu wa kudhoofishas kesi ya msingi anayokabiliwa nayo IZACK.
 
Back
Top Bottom