IGP Sirro ipo siku utayajutia maneno haya. Wa kufa ni nani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
IGP inaonekana yupo biased na Upinzani wa nchi yetu. Inaonekana ni kama naye ameshakua Mwanasiasa hasa toka chama tawala. Atambue kuwa utulivu hauletwi kwa vitisho.

Anaposema kuna mtu anataka kufa, unamaanisha nini na atauawa na nani? Mzee wangu IGP angalia maneno ya kuongea achanana na chuki za wazi wazi. Siku yakitokea ya kutokea hizi kauli zako ni reference na bahati nzuri wewe ni mwanasheria unajua nini unafanya.

Unashindwa kuiga mfano wa aliyekua IGP na kachero mbobevu Said Mwema ambaye alijikita kulea zaidi pande zote zinazosigana kama watoto wake. IGP umesoma management kwa ajili ya kuongoza na kusuluhisha na siyo kutisha. Tumia muda wako mwingi kutoa usia na ushauri na siyo vitisho. Saidia watu kufahamu kutii sheria.

Hivi kweli ndugu yetu hujui madhara ya kauli zako?
 
Ushauri mzuri kiongozi wa kitaifa nimuhimu kutunza kauli zake, hata hivyo tumejifunza mengi kutokana na kauli zake. Tungo tata huzaa mawazo fikirishi ambayo hukuza uelewa mpana 'public figures have to keep their words'
 
Siro siyo mwanasheria. Ulisomea biashara pale UD. Na A level alisoma EGM

Nampa tahadhari kanda Siro kuchukua tahadhari katika kila tendo na kauli ili asimalize vibaya. Huu ivhaguzi siyo sawa na mwingine wowote uliowahi kufanyika. Ataelewa baadaye.
 
Yule kamanda Sirro aliyekua RPC Mwanza Enzi za JK na huyu Sirro IGP naona kama nawaona watu 2 tofauti kabisa; wanafanana sana sura na sauti, tabia ni 2 tofauti, sijui kilitokea nini kwa kweli.
 
Back
Top Bottom