Wana JF ktk magazeti ya leo nimesikia kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema anategemea kupokea TUZO inayohusu AMANI hapa Tanzania,
Swali langu hapo ni kwamba ni lipi haswa alilofanya mkuu huyo mpaka apewe TUZO hiyo? ama anapewa hiyo Tuzo kwa kuwa Polisi wake wamekuwa wakishiliki ktk mauwaji ya watu wasio na hatia?
Kwani Sio siri kwamba Jeshi la Polisi Tanzania lina sifa chafu na yayumkinika kuamini kuwa ni taasisi inayochukiwa sana na walalahoi.Sifa kuu mbili za jeshi hili linaloongozwa na IGP Saidi Mwema ni :-
1) RUSHWA ILIYOKUBUHU na
2) UBABE WA KUPINDUKIA.
na hata ukisoma mhalili wa gazeti la( 01/06/2011) Tanzania daima lina sema POLISI WATASABABISHA VITA
Sasa inakuwaje tena IGP Mwema apewe Tuzo ya amani kama bado kuna kasoro nyingi zinazojitokeza ktk chombo anachokiongoza?
Kutakuwa na vigezo wanavyompima navyo mtu!
Utaweza kukuta maana ya AMANI kipolisi huenda ni kuwa rais hajapata kashkash za raia za kumkosesha usingizi!
Kutakuwa na vigezo wanavyompima navyo mtu!
Utaweza kukuta maana ya AMANI kipolisi huenda ni kuwa rais hajapata kashkash za raia za kumkosesha usingizi!
hehehehe
yaani unamaanisha matatizo yote tuliyonayo bado Raisi wetu anapata usingizi? hata vifo vya vijana arusha,mara hata PALE Polisi walipo pambana na raia Dar bado raisi aliendelea kupata usingizi?
Hata madikteta huwa na nishani nyingi nyingi tu.Kinachofanyika siyo kitu kipya ila kipya kitatokea siku za mbele Watanzania watakapopata uongozi tofauti unaojali maslahi ya taifa na si ya vikundi maslahi, tuzo hizi zitageuka kuwa vyeti vya aibu na laana
Ipi hiyo amani? Yan kila siku askari wanaua raia af wanasema kuna amani? Huku tunapoelekea inawezekana kila mtu akawa na bunduki yake iwe km huko drc hakuna amani ubabe ndo upo saaana!!!!
Hiyo tuzo inatolewa na nani, nadhani kutoka hapo tukiwa na info kamili inaweza kuwa na maana katika kuchangia. Kiujumla tuzo ya amani kwa IGP ni kama tusi kubwa ikipokewa kwani ni polisi wenyewe wanaochafua amani kwa kupokea rushwa, kubambika kesi, na kupenda kubonyeza triga hata pale 'mtuhumiwa' anapokuwa amenyoosha kitambaa cheupe
Nadhani anatunukiwa tuzo ya kuwahakikishia Mafisadi amani kwa kutumia nguvu za askari wake. Ni tuzo ya kumpongeza kwa kutekeleza matakwa ya mafisadi pasipo kujali maslahi ya walio wengi.