EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema
"Salam, ….. naomba tafakari mob justice (kujichukulia sheria mikononi) ni adui wa human rights rule of law, (sheria za haki za binadamu). Good governance (Utawala bora) iwe kwa raia au askari aliyeuawa … ambaye niko njiani kwenda … kumzika. Na iwe sababu yoyote, hata Mungu hampendi anayetoa kikatili roho ya mtu mwingine…..Where are the good people? (Wako wapi watu wema?). Lets join hands and have ant mob justice campaign in this country for common good (Tushikamane kupinga wanaojichukulia sheria mikononi katika nchi kwa ajili ya ustawi)."
Huo ulikuwa ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu (SMS) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema, uliokuwa ukilalamikia kitendo cha baadhi ya wanakijiji wa Mwakashahala kata ya Puge, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora, kumuua polisi Joseph Milinga, Aprili 20, 2011 baada ya kuwakamata wakiwa na bangi.
Mwaka jana aliuawa polisi wa cheo cha chini. Mwaka huu ameuawa RPC. Mwaka kesho sujui atauawa polisi wa cheo gani. Kama RPC anauawa kilaini hivi ndani ya ardhi ya Tanzania basi hata usalama wa IGP Mwema ni wa mashaka sana maana "mob justice" is still at work.
UPDATE
Habari za kuaminika nilizopata hivi punde ni kwamba RPC Wa mkoa Wa mwanza KAMANDA BALO amekufa kwa kupigwa risasi. Habari zaidi zitaendelea!!
UPDATE
Askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia cha FFU ameuawa kwa kupigwa mapanga na kukatwa kichwa kufuatia vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar jana mchana na kuendelea hadi leo. Mob justice still at work? (updated 18th October 2012)
UPDATE
VITENDO vya wananchi kujichukulia sheria mikononi vinaendelea kushika kasi ambapo askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wanadaiwa kuuwa na wananchi wenye hasira kali jana. Taarifa ambazo zililifikia Tanzania Daima Jumapili wakati tukielekea mitamboni jioni, zilisema kuwa mauaji hayo yalifanyika baada ya wananchi hao kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi cha Mugoma wilayani humo baada ya askari hao kudaiwa kumpiga risasi fundi wa pikipiki.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea mchana wakati askari kadhaa wa kitengo cha usalama barabarani walipofika kwa fundi pikipiki huyo na kutaka kuichukua pikipiki aliyokuwa akiitengeneza kwa madai kuwa ilikuwa na makosa. Kwamba fundi huyo aligoma na kueleza kuwa asubiriwe mwenye pikipiki ili kuepuka kudaiwa chombo hicho cha usafiri.
Mmoja wa mashuhuda hao, aliyatambulika kwa jina moja la Libela, alidai kuwa baada ya mvutano wa muda mfupi, askari hao walifyatua risasi na kumpiga fundi huyo mguuni na kifuani, hivyo kusababisha kifo chake. Aliongeza kuwa, tukio hilo liliwapandisha hasira wananchi na kuwafukuza askari hao waliokimbilia katika kituo hicho cha polisi.
Lebela alifafanua kuwa, wananchi hao waliamua kukichoma moto kituo hicho hatua iliyosababisha askari waliokuwemo kutoka na kukimbia kila mmoja na muelekeo wake. Alisema kuwa askari aliyetajwa kwa jina la Koplo Paschal alianguka wakati akijinusuru, hivyo kuvamiwa na wananchi waliokuwa na zana mbalimbali za jadi ambazo walitumia kumshambulia na kumuua papo hapo.
Wananchi hao pia wanadaiwa kumfuata askari mwingine anayetajwa kwa jina la Pc Alex aliyekuwa amekimbilia kwenye nyumba ya mwananchi mmoja na kumtoa kwa nguvu na kisha kuanza kumshambulia hadi kumuua.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku ya soko katika eneo hilo la Mugoma linalopakana na nchi jirani ya Burundi ambapo raia wa Tanzania na Burundi hukutana na kufanya biashara jirani na kituo hicho cha polisi.
Kutokana na kuchomwa moto kwa kituo hicho, nyaraka mbalimbali zinadaiwa kuteketea, huku pikipiki na baiskeli kadhaa zilizokuwa kituoni hapo nazo zikiteketea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi, hakuweza kupatikana kuthibitisha tukio hilo kutokana na simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.(updated 17th December 2012)
UPDATE
Wananchi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamemuua askari polisi mmoja na kumjeruhi mwingine kwa kutumia silaha za jadi, baada ya askari hao waliokuwa doria kumuua kwa kumpiga risasi mwendesha pikipiki kwa kuvunja sheria za barabarani.
Source: RADIO ONE BREAKING NEWS
..polisi mmoja wa wa pikipiki na dereva wa bodaboda wauawa katika kijiji cha litola wilayani namtumbo.sababu ya mauaji inasemekana kuwa kulikuwa na polisi wawili wakiwa kwenye pikipiki wakawa wanamfukuza dereva wa bodaboda ambaye alikaidi kusimama,baada ya polisi kuona wameshindwa kumkamata dereva wa bodaboda wakaamua kumtandika risasi na kupelekea kifo cha dereva wa bodaboda.
wananchi kuona hivyo wakaungana kuwafukuza polisi.kuona hali nh tete polisi wa nyuma ambaye alikuwa amekamata bunduki akawa ameruka na bunduki akawa ameidondosha,raia mmoja akaioata akamtandika yule polisi aliyekuwa anaendesha pikipiki nae akauawa hapohapo na yule aliyeruka kwenye pikipiki ameumia vibaya sana na ametoweka inasadikiwa amejificha.mpaka sasa inasemekana bunduki haijulikani iliko gari mbili za polisi zimeelekea kwenye tukio moja likiwa limejaa polisi waliojikamilisha kwa mapambano na nyingine iko tupuinasemekana ni kwa ajili ya kubebea maiti.
wananchi wa namtumbo wanalalamikia sana utendaji kazi wa polisi,umekuwa ukiwanyanyasa sana madereva wa bodaboda,vijana wa kitanzania wanaojitafutia riziki zao.lawama zaidi ni kwa hawa polisi kuendekeza rushwa na kuwabambikia makosa ya uwongo na wananchi wamechoka.