We Know Next
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 815
- 382
Mheshimiwa Kamanda Mwema - IGP,
Nadhani utakuwa na taarifa na kama huna taarifa basi tunaomba uanze kuifanyia kazi taarifa hii:
Kuna Genge moja la Kitapeli ambalo limezuka hapa jijini na kufanya utapeli wa kuvamia viwanja vya watu na kujifanya ni vya kwao. Genge hili linafanya kazi zake zaidi maeneo ya Kawe, Mbezi Beach, Tegeta, Boko mpaka Bunju. Genge hili la matapeli wanatembea na Magari yameandikwa Free Mansos, na wanatembea na silaha ( Bastola) vibindoni mwao na inasemekana wanapesa nyingi sana, ambazo ni pesa chafu. Wamekuwa wakifanya utapeli na usumbufu huo kwa baadhi ya watu wenye viwanja vyao ktk maeneo husika.
Kwa nini basi ni mtandao hatari?
Genge hili limejiimarisha sehemu zote muhimu ambazo linaweza kufanikisha kufanya mambo yao kwa urahisi, maeneo hayo ni katika Jeshi lako la Polisi, ofisi za manispaa, mahakama za ardhi, Wizara ya Ardhi na Makapuni binafsi ya ulinzi.
1. Jeshi la Polisi - Kuna baadhi ya polisi wanashirikiana na genge hili katika kuwadhurumu watu haki zao za msingi, tena kuna wengine ni maafisa wa juu kabisa ktk jeshi hili la Polisi. Maafisa hao wamekuwa wakikataa kutoa msaada kwa waathirika kwa misingi kuwa, migogoro ya ardhi Polisi haihusiki, ni wizara ya ardhi pekee. Hata mtu akienda kuripoti kuwa kuna wavamizi, wamevamia kiwanja, wamevunja nyumba, na wamekuja na silaha, bado polisi hao wanakataa kutoa msaada kwa walalamikaji. Badala yake, Polisi hao hao, wanakushauri kuwa la kufanya na wewe anza kubomoa kila anachokifanya huyo mvamizi. Kamanda, Tanzania tumefika hapo kweli? Yaani kimbilio la walalahoi limekuwashubiri? Unataka watu wachukue sheria mikononi? Maafisa hao wachache wasiokuwa na utu wala kufahamu kazi yao, wananunuliwa na pesa za hongo kutoka ktk genge hilo na kuwafanya kuwa nao ni wanamtandao, yaani polisi wanamsaidia mharifu? Je ni maadili ya kazi hakuna? Au ni sababu ya mishahara midogo? Kitakachokuja tokea Kamanda, watu wanaanza kukosa imani na Jeshi lako, na hata kuanza kujenga uadui na polisi, sababu tu, ya hao maafisa wachache wa polisi. Itafika kimbindi watatengwa kutokana na mambo haya. Genge hilo, limejijenga ndani ya polisi kwa ajili ya kupata usalama wao, kwani wanajua kabisa, wakifanya uvamizi huo, watu watakimbilia polisi kutoa taarifa, kwahiyo polisi hawata respond kwa haraka kama inavyotakiwa.
Maswali yangu ni haya kamanda,
i. Wananchi waende wapi ikiwa kama kimbilio lao, yaani polisi wakati wa matatizo ya uhalifu na ya jinai kuna kuwa hakuna msaada?
ii. Ikiwa kama maafisa hawa wataendelea kununuliwa na kuwa wanamtandao wa kiuhalifu, je unajenga jeshi la namna gani?
iii. Hivi wananchi wakipoteza imani na polisi tutakuwa salama kweli?
iv. Ni Kwanini maafisa wachache wa polisi waharibu sifa ya jeshi lako lote?
v. Nilisema mwanzo kuwa, unaweza kuwa umelisikia kundi hili au hapana, lakini je jibu lake au suluhisho lake ni nini kwa lolote kati ya uelewa au kutoelewa kuwepo kwa Genge hilo?
Nafahamu, kunaweza kuwa na wanajamvi wengine ambao wamesha lisikia au kukutana na mambo ya Genge hili, labda wanaweza kuongezea kwa hapa nilipoishia....! Kamanda, Mtandao huu ni hatari, chukua hatua.. PART II itaendela na maeneo mengine..