Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,548
Mkuu wa jeshi la polisi, IGP Said Mwema amesisitiza kuwa jeshi la polisi halitaendelea kuwafumbia macho watu wanaovuruga amani ikiwa ni pamoja na kuchoma nyumba za kuabudia na kuuana kwa kisingizio cha kidini
Wana JF naomba kufahamishwa kitu hapa, hivi kuna Protocol Approach katika kutoa matamko kuhusu hali ya amani hapa nchini hususani masuala haya ya kidini? Nauliza hivi kwa sababu vurugu hizi zimekuwepo kwa kipindi na kama kawaida geared by "Mihadhara ya Kidini" ambayo bado ipo na tena kwa kiburi. Hivi karibuni kutaibuka Mhadhara wa Dini ya Kislamu pale Mbagala Zakhem, baada ya ule uwanja kufungwa kufuatia vurugu za "Mkojo" sasa inavyoonekana Serikali kwa kuwa "Inajua inachokifanya" Imeruhusu Mihadhara kuendelea pale Zakhem. Tusubiri nini kimedhamiriwa na Seriakali yetu. Kwa kuwa IGP anasema kuwa Serikali haitavumilia viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani, kama hajui viashiria hivyo ni MIHADHARA YA WAISLAMU KUWATUSI WAKRISTO NA DINI YAO. Tunaweza kusema kuwa Serikali iwe staright forward katika suala la kulinda AMANI wala lisiwe ni la kupendezesha jamii fulani hapa. Kumbuka Mh. IGP Dhamana ya AMANI ipo juu yako hadi IGP mwingine atakapokuja Chukua Hatua SASA.