Ifanye pesa isiwe ya msimu, buni vyanzo vingine vya mapato

Lamomy

JF-Expert Member
Sep 4, 2023
15,517
37,909
Kilimo kina msimu, hilo tunalielewa, msimu wa masika, vuli, kipupwe na hata kiangazi. Pesa hazina msimu. Ukifanya kazi kwa bidii na ukizitafuta, mwaka mzima unaweza ukawa kwenye masika ya hela wakati wengine wakiugulia kwa kusema hali ngumu wewe utakuwa huelewi wanaongea kichina au kimakonde.

Huwezi kubadili majira ya mwaka kwenye kalenda, lakini unaweza kubadili majira ya pesa kwenye akaunti zako za benki.

Wengi tunaridhika na utajiri wa tarehe 30. Kila mtu anakuwa mbabe ikifika mwisho wa mwezi. Kila mtu anajiona milionea lakini zikifika tarehe kama hizi, tarehe 15-23 ya kila mwezi, yule milionea aliyekuwa ana mbwembwe sana wiki 2 tu zilizopita, hana kitu.

Na kila mwezi majira yake ni hayahaya, maji kupwa maji kujaa lakini hashtuki... Anaona ni sawa tu kuwa na hela tarehe 30 lakini apeche alolo wiki 2 baadae akihaha kukopa ili afike tarehe nyingine ya mshahara.

Je, wewe ni mmoja wao? Tajiri wa msimu ni wewe?

Tarehe 30 HR anakupa kiburi, wiki 2 baadaye unapaki gari haina wese unaanza kuomba lifti kwa co-workers wanaokaa karibu na wewe Kimara wakupitie. Je, ni wewe?

Tajiri wa mshahara, ukiona tangazo la punguzo la wafanyakazi unasikia nnya inagonga pichuchu, huna Plan B, na huna hata miaka 30 lakini akili yako imezeeka, unajiita bosslady kwa mshahara wa kila tarehe 30?

Babako aliishi kwa mshahara, akastaafu, na sasa anaishi kwa pensheni, hatumlaumu. Kipindi alichoishi hali haikuruhusu, eti na wewe, unataka uishi kama baba'ko, ili na wewe uje ustaafu uishi kwa pensheni?

Babako ameishi kwenye ujima, wewe una kila sababu ya kutoishi kama yeye kwa sababu una kila kitu ambacho yeye hakuwa nacho. The tools, the technology, the information, the education. Ukipata matokeo sawa na babako aliyeishi karne ya 20 umefeli.

Mshahara hautakupa utajiri, mshahara unapaswa ulipie luku. Bili za maji, housegirl, wese la gari na bata.

Maendeleo yako mengine yanahitaji other revenue streams ambazo huna na huonyeshi dalili za kuzitafuta. Utakufa maskini hakika au utaishi kwa pensheni ya 60,000 kwa mwezi kama mamako mstaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wake up now month end millionaire! You're alive so that u can challenge the status quo na sio kuishi-ishi tu kama bolizozo.

 
Umeongea vyema kwa sehemu yako, ila maisha yako tofauti sana na maneno/nadharia tunazoambiwa na kusikia.

Hakuna asiependa kuwa tajiri, au uchumi wake uwe bora, changamoto ni namna ya kuendelea mchakato wa kukua kiuchumi. Elimu yetu imewafanya wasomi wengi wawe waoga kuanzisha miradi ya maendeleo mapema. Nadhani hili somo linawafaa sana watoto ambayo hawajayaanza maisha ya mapambano, waonyeshe nini wafanye, wafanye Kwa namna gani na wakifeli wapi warekebishe mapema..

Juzi nimepokea simu ya jamaa amefilisika baada ya kujikusanya na kuanzisha biashara ambayo alipata washauri na akawaamini, akaacha kazi kaingia mzigoni kwenye biashara, leo anajutia maamuzi ya kuacha kazi. Kiufupi wote hatuwezi kuwa matajiri na ili uwe tajiri lazima kuna maisha uyaache/kuyasahau kwa muda pia ni muhimu kujiamini wewe mwenyewe, waswahili wanasema "akili ya kuambiwa changanya na wa kwako".

Tuendelee kujifunza chief.
 
Mkuu nilijua unatoa solution kumbe na ww unatulalamikia
MBONA jamaa katoa ushauri mzuri tuu, mnamzodoa kwa sababu Gani? Ila kama Mimi nimemuelewa vizuri TU, yupo sahihi, solution ufungue kichwa chako uone fursa ingine badala ya hiyo uliyokuwa nayo kwa sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom