Ifahamu taasisi ya ‘Jicho la Tanzania’

Ifahamu taasisi ya ‘Jicho la Tanzania’

Joined
Apr 10, 2023
Posts
11
Reaction score
15
20230414_170301_0000.jpg
 
Faida zake ni zipi?
Chama kinajihusisha na nini
SEHEMU YA III: UANACHAMA NA AINA ZA WANACHAMA
IBARA 10: Uanachama
Shirika lipo wazi kwa mtu yoyote ikiwa-
Ni Mtanzania;
Ana umri wa miaka 18 au zaidi;
Ana akili timamu;
Atakubaliana na malengo ya Shirika.
IBARA 11: Aina za Wanachama
Kutakuwa na aina tatu za wanachama katika Shirika ambazo ni-
Wanachama Waanzilishi: Ni wale ambao walishiriki katika kuanzisha Shirika;
Wanachama wa Kawaida: Ni wale watakaojiunga baada ya kusajiliwa Shirika;
Wanachama wa Heshima: Ni wanachama wa Shirika ambao watapewa uanachama kutokana na nafasi yao katika jamii na mchango wao katika Shirika.
IBARA 12: Haki na Wajibu wa Mwanachama
Kuchagua au kuchaguliwa isipokuwa mwanachama wa heshima;
Kushiriki vikao na kupata taarifa za maamuzi ya Shirika;
Kupata taarifa za maendeleo ya Shirika;
Kuhudhuria mikutano na vikao vinavyomruhusu.
Kulinda, kutunza na kuheshimu katiba ya Shirika pamoja na Sheria za nchi;
Kushiriki shughuli zote rasmi za Shirika zitakazo amriwa na uongozi wa Shirika;
Kulipa Ada ya kwa mwezi;
Kuhudhuria Mkutano.
IBARA 13: Kukoma kwa Uanachama
Kifo;
Amekiuka katiba ya Shirika;
Kuugua ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari;
Kushindwa kuhudhuria Mkutano Mkuu kwa kipindi cha tatu mfululizo;
Kushindwa kulipa ada kwa kipindi cha pili mfululizo;
Mwanachama kujiondoa mwenyewe kwa ridhaa yake.
 
We PRO kujielezea umeshindwa man.

Ungeanza hivi..

Jicho Tanzania ni Taasisi ya Serikali inayoshughulika na...

Hapo tupe history, mission na vision, mnatoa huduma gani, kwa watu gani, kama kuna gharama au mnalipa watu.. ofisi wap.. etc
 
We PRO kujielezea umeshindwa man.

Ungeanza hivi..

Jicho Tanzania ni Taasisi ya Serikali inayoshughulika na...

Hapo tupe history, mission na vision, mnatoa huduma gani, kwa watu gani, kama kuna gharama au mnalipa watu.. ofisi wap.. etc
SEHEMU YA II: DIRA, DHAMIRA NA MADHUMUNI.
IBARA 7: Kauli Dira
Kuwaunganisha vijana, wanawake, wanaume na makundi yote ya kijamiiili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake, kwa kushiriki moja kwa moja katika miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Jamhuri ya Muungano waTanzania.
IBARA 8: Kauli ya Dhamira
Kutoa elimu kwa jamii kwa ujumla ili itambue wajibu wa kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kizalendo ili kujiletea maendeleo ya taifa kwa ujumla.
IBARA 9: Madhumuni
Kuhamasisha wanawake,vijana na makundi yote ya kijamii kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira kama kichocheo cha ujasiriamali.
Kuwaunganisha vijana kote nchini, kuunga mkono juhudi za serikali kupinga ukatili, unyanyasaji, ubaguzi, mila na dini potofu, ubadhilifuwa wa mali za umma, uhujumu uchumi na matumizi ya dawa za kulevya.
Kuwafikia jamii zilizoachwa nyuma kimaendeleo ikiwa ni pamoja na jamii zinazo hamahama za wafugaji,waokota matunda pori wala mizizi na wavuvi kuwapatia elimu ili kuleta maendeleo endelevu.
kuchochea uwajibikaji na roho ya kizalendo kwa jamii.
Kuuelimisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kushiriki katika miradi inayo tekelezwa ndani ya taifa letu na namna ya kutunza miundo mbinu hiyo kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Kutoa elimu ya Uraia,Utawala bora, maadili na uzalendo kwa jamii na kuenzi nafasi na mchango wa kila mmoja katika kujiletea maendeleo.
Kukuza uelewa juu ya namna ya kutumia fursa za kimazingira kujiletea kipato kwa kutumia fursa zinazopatikana ndani ya maeneo yao, kuanzia Mtaa hadi taifa.
Kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa yatima, wajane, wazee na waathirika wa madawa ya kulevya katika upatikanaji wa huduma muhimu za kibinadamu kama elimu, afya na malazi.
Kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Tehama na kutumia Tehama kujiingizia kipato kwani hii ni njia inayo weza kuwasaidia watanzania wengi kujiajiri.
 
Back
Top Bottom