Ifahamu sayari ya Saturn kiundani zaidi

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,962
Naamini mko poa.

Leo hebu tuendelee kuzifahamu sayari zilizoko kwenye mfumo wa jua letu, na tutaiangalia kiundani zaidi sayari ya Saturn hebu tuanze.

1. Ni sayari ya 6 kutoka umbali wa jua letu.
340px-Planets2013.svg.png

2.Ni sayari ya pili kwa ukubwa baada ya Jupiter.
3. Ni sayari unayoweza kuiona kwa macho.
4.Ni sayari yenye mfumo wa pete (rings) imara.
Saturnoppositions-animated.gif

5.Ni sayari yenye miezi (moons) 62,na mwezi wake mkubwa unaitwa (Titan moon) na ni wa pili kwa ukubwa ktk mfumo wa jua letu baada ya mwezi wa Jupiter unaoitwa Ganymede.
220px-Titan%27s_orbit.svg.png

6.Titan moon kumeonekana kuwa na mazingira yanayofanana na Dunia yetu.
7.Ni sayari ya gesi ya hydrogen na helium( si udongo kama duniani)
600px-Saturn_diagram.svg.png

8.Saturn ulizunguuka jua kwa wastani wa umbali wa 1.4 bilion km, na ikizunguuka kwa spidi ya 9.69 km/s ikitumia siku 10,759 sawa na miaka 29.5.
9. Rings (pete) za sayari ya Saturn zinakadiriwa kuwa urefu wa umbali 6,630 km hadi 120,700 km na zikiwa na unene wa mita 20 na zimeundwa na maji yaliyoganda (barafu) 93%.
10. Hili hapa ni jedwali la kuangalia mambo ya Mass,weight, density na n.k.
Planetary Fact Sheet

Haya wakuu, mimi ni binadamu kama kuna mahali nimekosea rekebisha,ongezea au chochote kinachofaa kifanye.
 
Saturn inaonekana kwa macho bila telescope kwa mwezi huu wa July, maeneo ya Afrika mashariki linakuwa utosini kuanzia saa 3 unusu usiku hadi saa 4 unusu usiku ( 2130hrs-2230hrs ) ...sayari huwa hazimeremetimeremeti zinawaka moja kwa moja.
 
Fafanua ??
 
Kuona itategemea anga limekaaje kwa sehemu ulipo ... Mara nyingi nyota huwa zinametameta yaani mwanga huwa ni wa kufifia, sayari mwanga wake haufifii... Wakati wa usiku angalia upande wa kusini mashariki, juu ya kichwa(utosini)... Kuanzia saa mbili au saa tatu... Kuna nyota moja angavu sana.. Ina mwanga mwekundu (ni sayari ya Mars) kwa chini yake kuna nyota inayong'aa sana (Antares) upande wa kushoto wa nyota hio ndio kuna sayari ya saturn (mwanga wake hafifu kidogo)
NB somo hili linahitaji kufunzwa kwa vitendo kuliko nadharia lakini kuna apps zinaweza kukusaidia... Kwa play store download app hii Star walk, Sky View au star chart... App store Star Walk
 
Saturn inaonekana kwa macho bila telescope kwa mwezi huu wa July, maeneo ya Afrika mashariki linakuwa utosini kuanzia saa 3 unusu usiku hadi saa 4 unusu usiku ( 2130hrs-2230hrs ) ...sayari huwa hazimeremetimeremeti zinawaka moja kwa moja.
Unaotofautishaje na nyota?
 
Asante kwa shule, kwa kuongezea tu:-
  1. Density ya saturn ni ndogo kuliko maji (0.687g/cm3), hii ni kwa sababu saturn ni gas giant planet (haina solid surface).
  2. Wakati Galileo anaigundua mwaka 1610 hakuweza kutoa maelezo sahihi kuhusu rings, sababu kubwa ni kwamba telescope yake haikuwa na nguvu ya kuona rings vizuri, yeye alihisi labda ni moons. Hadi mwaka 1655 Christian Huygens alipotumia telescope nzuri aliweza kugundua rings za Saturn
  3. Saturn imetembelewa na vifaa 4 kutoka duniani (spacecraft), Cassini ndio space craft iliyoenda karibu zaidi na hii sayari (mwaka 2004) na kuleta picha nzuri na za karibu za Saturn na moons zake
  4. Saturn inakisiwa kuwa na miezi (moons) zaidi ya 150, iliyopewa majina mpaka sasa ni 62, hii ilitoka na cassini kupiga picha miezi mingi mingine...
  5. Siku moja ya Saturn ni sawa na masaa 10 na dakika 32 za duniani (shorter day)
  6. Saturn inaweza onekana kwa macho (ila hutaweza ona rings), ni sayari tano tu kwenye mfumo wetu wa jua zinaweza onekana kwa macho (bila telescope)
  7. Inasadikiwa kuwa baadhi ya moon za saturn zinaweza kuwa na micro-life, hii ni baada ya kugundulika liquid water south of big moons za Saturn. Haijajulikana hadi sasa kwa nini south ya hizo moon ni warm kiasi cha kuwa na liquid water.
Hiyo ni nyongeza tu
 
1. Hiyo no1 ni sawa na kusema huwezi kukanyaga si ndio ???
 
Asanteni Njaa jaiy4 Bravo Mike Haya tuendelee kuelimishana na vitu vingine kuhusu hii sayari.

Mwezi huu wa July , sayari zionekanazo kwa macho makavu ni Venus, Mars, Jupiter, Saturn na kwa taaabu ni Uranus zikiwa zimejipanga kwenye mstari mmoja kila moja ikizama magharibi kwa wakati wake, Venus @ 1900hrs +-, Mars @ 0300hrs +-, Jupiter @ 2250hrs +-, Saturn @ 0415 hrs +-, Uranus @ 1300 hrs +-.
 
1. Hiyo no1 ni sawa na kusema huwezi kukanyaga si ndio ???

Yes, haina solid surface, labda ndani sana....inasemekana ina solid core. Kwa sababu ni ball of gas, then density yake ni ndogo
 
Back
Top Bottom