Ifahamu Saikolojia ya Hasira

Bess

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
542
649
Hasira ni nguvu hasi inayomjaa mtu na kama sifa ya nguvu/nishati nyingine lazima itafute kitu cha kupokea;

Mtu akiwa nayo automatically inahamia kwenye maeneo fulani fulani ya mwili:

• Mwingine huenda mikononi anapiga kila kilicho mbele yake hasa cha thamani, hapa akiwepo aliyemkasirisha karibu analiwa kofi ama ngumi

• Mwingine hasira huenda miguuni na kupiga teke kilicho mbele yake

• Mwingine huenda mdomoni, maneno anayotoa makali anapata ahueni anatuliza hasira yake.

• Mwingine huenda tumboni, anatafuta chakula anachopenda anakipiga hasa, akishiba anasahau; japo hapa ni hatar sababu atapata obesity na madaktar watamshauri punguza misosi

• Mwingine huenda masikioni, akisikiliza nyimbo, counselling ama aki'share kwa mwenzake hasira inaisha

• Mwingine huwa na uwezo wa kui'ahirisha ndiyo maana biblia inamsifu sana mtu anaeweza ku control hasira yake; anaitwa ni mfano wa mtu autekaye mji
Mithali:16.32
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji

Hasira isipopata pa kuhamia ama kuahirishwa huzalisha kitu inaitwa uchungu, huu ni mlango mkubwa sana wa adui kuingia na kufanya makazi Ndiyo maana mda maalum wa kukaa na hasira kibiblia ni siku moja tu

Jua lisizame....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom