Ifahamu Pearl au kwa kiswahili "lulu" kama ilivyozoeleka kwa watu wengi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,705
Watu wengi wamezoea kutamka neno “LULU” wakiimaanisha nikitu chenye thamani kubwa ila naamini wengi wao hawajui hizo lulu ni kitugani, zipoje, zinapatikana wapi na matumizi yake ni yapi na kulitambua hilo hapa chini ni maelezo mafupi ya “LULU” OR PEARL

LULU nikama goroli flani hivi yaani spherical balls zenye rangi nyeupe ya kung’aa/white or bluish-grey, goroli hizi au lulu zina thamani kubwa kiasi kwamba zinafananishwa thamani yake na madini mengine ya vito kama ruby, sapphire, tanzanite, diamond na tanzanite kwa maana hiyo ukizipata hizi lulu pia ni utajiri kama utaziuza.
“LULU” hupatikana chini kabisa ya kina cha bahari, lulu hizi hutolewa na samaki mmoja anayeitwa OYSTER, samaki huyu anamagamba yaani shells na ndani ya haya magamba goroli lulu hizi ndio hupatikana na samaki mmoja anaweza kuwa na lulu nyingi tu zakutosha kukufanya wewe uondokane na umaskini. Baada ya samaki hawa kufa na kuoza kule chini ya bahari lulu hizi hubakia chini ya kina cha bahari kwani huwa zenyewe haziozi na hivyo watu huenda huko kuziokota au pia huwakamata samaki hawa na kuwapasua na kuchukua hizi lulu
LULU nikama madini mengine ya vito huwa zina matumizi mengi, lulu maranyingi hutumika kama urembo kwa wanawake kwa kuzivaa shingoni au mkononi pale zinapotungwa na kuwa kama cheni au bangiri

Hapa chini ni picha ya hizo lulu zenyewe hebu zitazame zilivyo na picha moja inaonyesha lulu hizo zilivyojipanga ndani ya huyu samani na hapo zinaonekana baada ya kumpasua huyo samaki anayeitwa OYSTER. Lulu zipo NATURAL yaani lulu zinazotoka kabisa kwenye kiumbe hai yaani samaki (ndio hizi hapa chini kwenye picha na ndizo naziongelea hapa) pia lulu zipo ARTIFICIAL yaani lulu feki za kutengeneza viwandani ila zote hutumika kwa mapambo hasa kwa wanawake, lulu za kwenye samaki ndio zenye thamani kubwa na sio hizi za kutengeneza kiwandani feki, hizi feki zinatengenezwa ili watu wa kipato cha chini nao wasioweza kununua mkufu uliotengenezwa kwa original lulu waweze kununua mikufu hii bei ndogo
HII NDIO LULU/PEARL

FB_IMG_1632511955693.jpg
 
Aliyeona lulu kwenye hiyo picha anioyeshe tafadhali, au ndio hivyo vidoti
 
Maelezo ni mazuri mtoa mada, lakini hili la jamii ya kono kono kuita "samaki" ni kukanganya ufahamu wa wasomaji hasa waswahili.
 
Back
Top Bottom