Ifahamu Michoro ya mwamba (Igeleke), kivutio kikubwa cha utalii Iringa

roservelt

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,418
1,510
Habarini wadau?

Kama mgeni katika mkoa wa Iringa nimejaribu kutembelea vivutio vya utalii ndani ya mkoa huu.

Ndani ya mkoa huu kuna vivutio vingi vya utalii kama makumbusho ya chief Mkwawa, mabaki ya zama za mawe za kale (Ismila) jiwe lililokuwa linazungumza kipindi cha utawala wa Mkwawa (Gangilonga), michoro ya mwamba (Igeleke) na vivutio vingine vingi. Kwa leo nitazungumzia kuhusu michoro ya mwamba iliyoko Igeleke.

Igeleke ni neno la kihehe linalomaanisha mawe yaliyobebana, eneo hili linapatikana ndani ya manispaa ya Iringa karibu na barabara kuu ya Iringa-Dodoma.

Ndani ya hifadhi (IGELEKE) ndiko iliko michoro ya mwamba pamoja na vivutio vingine vingi. Ilielezwa kuwa hapo zamani, kinga za mwamba huu zilikuwa zinaheshimiwa sana na jamii ambayo ilikuwa ikizitumia kwa matambiko.

Mabaki ya Akiolojia kutoka ardhini yanaonesha kuwepo kwa shughuli za kibinadamu kwa miaka mingi kuanzia mwishoni mwa zama za mawe, miaka 40,000 iliyopita mpaka zama za chuma na mpaka mbali katika kipindi kinachojulikana kama cha kihistoria.

Michoro ya mwamba huu ni ya mtindo wa hunter- forager ambayo inatokana na aina ya madini ya Ukaria. Kuna zaidi ya maumbo 30 ya kibinadamu na wanyama ikiwa ni pamoja na twiga, tembo, pofu, na nyumbu na vilevile miti yenye umbo la kinara cha mshumaa inayojulikana kama candelabra. Inasemekana kwamba michoro hiyo ilichorwa na watu wa kale wa eneo hilo.

Ukiachana na michoro ya mwamba , ndani ya hifadhi (IGELEKE) kuna vivutio
kama , aina kumi na saba 17 ya miti ya matunda, jiwe kubwa lenye mipasuko ndani yake, pamoja na pango lililoundwa kwa mawe.

JIWE KUBWA LENYE MIPASUKO NDANI YAKE. Inasemekana jiwe hili lilitumika zaidi na watu wakale kipindi cha vita ya chief Mkwawa (WAHEHE) dhidi ya wanajeshi wa kijerumani. Ndani ya mipasuko ya jiwe hilo wahehe walijificha kama njia ya kujilinda dhidi ya wanajeshi wa kijerumani.

PANGO LILILOUNDWA KWA MAWE. Ndani ya hifadhi (IGELEKE) kuna pango lililoundwa kwa mawe. Inasemekana pango hili lilitumiwa na watu wa kale wa eneo hili, kupumzika, kujilinda dhidi ya jua na mvua pamoja na kuendesha shughuli zao mbalimbali za kila siku.
vingine.

1476357464566.jpg
1476357530397.jpg
1476357557076.jpg
1476357591419.jpg
1476357646668.jpg
1476357676574.jpg
1476357715995.jpg
1476357755382.jpg
1476357773612.jpg
1476357804457.jpg
1476357841233.jpg
 
Back
Top Bottom