Ifahamu Kampuni ya Simu za Mkononi ya 'itel Mobile'

Mar 5, 2020
18
28
itel Mobile ilianzishwa mwaka 2007 jijini Hong Kong nchini China kwa kutambua kiu ya wateja ya kuunganishwa kimawasiliano Duniani. Kwa kutumia Falsafa yetu ya "Join · Enjoy", tunafurahi kumpa hamasa na nafasi sawa kila mtu kwa kutoa bidhaa bora kabisa na zinazokidhi haja ya mawasiliano duniani kote.

Kutoka mwaka 2007 mpaka 2019, wateja wetu wamekuwa wakiongezeka kwa kasi ulimwenguni kote kwa mauzo na ongezeko la ofisi katika nchi mbalimbali duniania kote huku tukiwa kwenye zaidi ya nchi 50 ikiwemo Tanzania. Wateja zaidi na zaidi wanaendelea kutufahamu, kuunganishwa kimawasiliano kwa bidhaa zetu za simu na kuunga mkono kampuni yetu katika kuleta teknolojia zaidi.

Kwa ushirikiano na upendo wa wateja wetu, itel Mobile ilifikia kiwango cha juu cha mauzo ya simu milioni 80 mwaka 2007 na kushika nafasi ya 16 ya Kampuni zinazopendwa zaidi Barani Afrika katika mwaka huo, hii ni kulingana na taarifa za Jarida mashuhuri la “African Business”.

Unataka kufahamu zaidi kuhusu itel Mobile? Endelea kuwa nasi hapa Jamii Forums, pia ungana nasi katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram, Twitter na LinkedIn, tafuta tu 'itel Mobile Tanzania. Asante!
 
To be honest itel ndo simu mbovu kuwahi kutokea katika huu mgongo wa ardhi hususani matoleo ya smartphones

Kwanza kioo kinataka msuli kuminya halafu hakina sensor iliyo stable. Unakusudia kuminya 2 yenyewe inaminya 4

Kwenye hivi viswaswadu atleast mmeteka soko lakini kwenye smart mmebugi mazee

It's Scars
 
Scars,
Ila nahisi ulitumia matoleo yao yale ya mwanzoni kabisa ya TACHI sio SMARTPHONE zenye android. Yale kweli yalikuwaga yanasumbua sana. Ila sasahivi kiukweli simu zao hazisumbui udhaifu wao ni storage wameishia kwenye GB32 NA RAM2 na zingine zilizo nyingi ni GB16 kwa RAM1.
 
Ila nahisi ulitumia matoleo yao yale ya mwanzoni kabisa ya TACHI sio SMARTPHONE zenye android. Yale kweli yalikuwaga yanasumbua sana. Ila sasahivi kiukweli simu zao hazisumbui udhaifu wao ni storage wameishia kwenye GB32 NA RAM2 na zingine zilizo nyingi ni GB16 kwa RAM1.

Hapana mzee nalijua hilo ndo maana nimetumia neno smartphones. Hizo touch sio kusudio langu na hazina hadhi ya kuitwa smartphones wala touch screen kwasababu hata touch yake inazidi kufifia kadri siku unavyozidi kuitumia. Itafika siku hiyo touch bila kijiti au kimbao huwezi kupokea simu (sasa mimi sizungumzii hizi).

Nazungumzia hizi smartphones tena hapa nimeilenga itel A series

Kama hii simu imetengenezwa china basi eidha watoto wakichina katika kuchezea chezea vifaa vya baba zao wakajikuta wametengeneza itel.



It's Scars
 
honestly hii ni kampuni mbovu kuliko zote nilizowahi kutumia hapa tz.... ITEL haikuwa hata na hadhi ya kutengeneza simu za batani nyinyi mlifaa muwe mnatengeneza midoli ya watoto.
Hamna kampuni hapo hili ni chaka la wahuni

si umeona jamaa mwenyewe kasusia uzi wake

It's Scars
 
Mimi ni muuzaji Smartphones itel mnazingua....ila
2160
2180
5081
5625
2150
2190
2090
2060
na viswaswadu vyote mmejitahidi....

Nawezaje kuwa sales guy wenu maana huyu dogo mlompa dhamana huku anazingua
 
simu nzuri ila shida moja. Mi natumia itel kitochi inasumbua ukishaongea na simu kwenye kukata hadi nibonyeze mara mbili au tatu bila hivyo simu inaendelea kuwa hewani na hiki kitochi ni cha pili cha kwanza kilikuwa hivo hivo
 
Huyu ndugu wa Itel atakuwa anasoma hizi comments halafu anabadili kwenda kichina kisha anawatumia wachina halafu wanamfuta kazi.

Ila huu ndio uzuri wa social media,Niliwahi mshauri mtu kabla hujaenda sokoni hakikisha ndani kuko sawa.Hizi feeback ni nzuri sana ila walitakiwa wawe wameshazipata na wawe na majibu.na hapo ndio msingi wa kuwa na SOCIAL MEDIA STRATEGY unakuja kwani unapokuwa na strategy ina maana tayari unakuwa na mpango wa kudeal na negative feedback.

Binafsi natumia ITEL kama simu yangu pekee,ni ya batani ya line 3 na huu ni mwaka wa tatu na imeonesha uvumilivu wa hali ya juu yaani VALUE FOR MONEY binafsi situmii smartphone-I cannot afford it.

Huyu bwana wa ITEL nimualike kibiashara zaidi aje PM tuongee zaidi namna bora ya kusimamia hii show ya JF.Hii haifanani na FB wala huko kwingine hapa unapata real feedback na ukitaka ushauri wa solution pia wanakupa.

Karibuni Jamii Forum.Nawakaribisha sana kwa niaba ya Wana JF wote wenye mapenzi mema
 
Back
Top Bottom