The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Kwa kiasi kikubwa sasa biashara (Industry) mbalimbali zinakutana na mabadiliko mengi na yasiyotarajika na kutabirika (environmental uncertainty).
Ushindani katika biashara umekuwa mkubwa, makampuni makubwa (giant players) yanaingia kwa kasi na kwa nguvu kubwa (aggresively) katika masoko mapya na kuangamiza wenyeji (established companies) katika soko na industry kwa ujumla.
Mifumo ya usambazaji (distribution channels) hutofautiana nchi na nchi na kila kukicha hubadilika kutokana na ukuaji wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Pia imekuwa ni kawaida kwa kampuni moja kujifunza na kuiga MKAKATI wa kampuni nyingine (market leader) katika soko, tena kitendo hichi sasa hufanyika very rapidly. Hivyo imekuwa ni suala gumu kwa kampuni kuwa na faida ya kiushindani (Competitive Advantage) kwa muda mrefu.
Hali hii hujulikana kama HYPERCOMPETITION, na huweza kuhimilika kwa kutumia mbinu mbalimbali za kimkakati (STRATEGIES). Miongoni mwa mbinu zitumikazo katika mazingira haya ni ile ijulikanayo kama CANNIBALIZATION; hichi ni kitendo cha kampuni kubadilisha bidhaa yake ambayo bado inafanya vizuri sokoni na kuleta bidhaa nyingine kwa lengo la kumuwahi mshindani wake kabla hajafanya kitendo hicho, hapa lengo ni kumfadhaisha na kumpoteza kimkakati mshindani husika, maamuzi ya kutumia mkakati huu mara nyingi hufanyika katika ngazi ya "corporate" na "business" katika kampuni.
Kipindi cha nyuma mbinu hii ilipata upinzani mkubwa ila kwa sasa makampuni mengi huitumia kutokana na hali ya kutotabirika katika soko, na ndipo kipindi kimoja Bill Gates, CEO wa Microsoft alipata kunena " ..............Cleverness is the position in this business"
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
(House Of Strategy)
Karibu kwa huduma za uandishi wa michanganuo ya miradi na mipango mkakati, pia kwa ushauri na semina katika maeneo ya USIMAMIZI WA MIRADI na MIPANGO MKAKATI.