If you have a weak heart dont Open! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

If you have a weak heart dont Open!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlachake, Nov 2, 2011.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  [​IMG]mwili wa marehemu mzee Laurance Nkwera
  [​IMG]Umati wa Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakiwa wamemshikilia dada wa marehemu aliyekuwa akilia huku akimlaumu marehemu kaka yake kwa kujihisisha na uchawi na kukataa ushauri wake.

  MTU MMOJA aitwaye Laurance Nkwera 60 mkazi wa Kijiji cha Ibani Ludewa katika Mkoa mpya wa Njombe amekufa kwa kuchomwa moto na kuungua vibaya kwa imani za kishirikina, huku nyumba yake ikiteketea, na familia yake kunusulika kifo kwa kutoboa nyumba.

  Mwandishi wa mtandao huu kutoka Ludewa Basil Makungu anaripoti kuwa tukio hilo limetokea usiku wa octoba 01 mwaka huu majira ya saa nane alfajili baada ya mlango wa Nyumba yake kufungwa nje na watu wasiojulika kutokana na mvutano uliotokea kati yake na wauaji kabla ya wauaji hao kumzidi nguvu na hatimaye kuchoma nyumba yake.

  Akizungumza katika eneo la tukio Cesilia Haule ambaye ni mke wa marehemu Laurance alisema kuwa yeye na mumewe walikuwa wamelala chumbani na watoto wao wawili wakiwa wamelala sebuleni na kwamba ilipofika saa nane za usiku watu wasiojulikana waligonga mlango na kutoa masharti ya kutokutoka nje.

  Ester Nkwera ni mtoto wa marehemu na Mwanafunzi wa darasa la nne
  katika shule ya msingi Kimbila anasema yeye alikuwemo ndani wakati Nyumba ikiunguzwa moto na kwamba yeye na mama yake walifanikiwa kujiokoa kwa kutoboa nyumba yao ya miti lakini Baba yake alibaki pamoja na mdogo wake Laurance.

  Laurance ni mtoto wa marehemu mwenye miaka mitano tu, yeye alinusurika kifo kwa kupita katika mikono ya wauaji ambao walikuwa wamezingira nyumba hiyo ya miti huku wakiwa wamesimama pembeni kuhakikisha Nyumba na vyote vilivyomo vinateketea.

  Mwenyekiti wa kitongoji cha Ibani Philipo Haule, Afisa Mtendaji Kata Onesmo Haule wamesema kuwa marehemu pamoja na watu wengine wanne ni muda mrefu walikuwa wakituhumiwa kujihusisha na kuwatesa watu kwa uchawi ikiwemo kubaka wake za watu kiuchawi, kuua watu na kuwafanyisha kazi usiku kwa uchawi.

  Wakizungumza kwa masharti ya kutoandika majina kwa kuhofia usalama wao wakazi wa kitongoji cha Ibani Ludewa walisema wamechoshwa na udhalilishwaji unaofanywa na wachawi ikiwemo kuwabaka wake zao kiuchawi,kuwauwa na kuwatumikisha kazi usiku na kwamba watahakikisha wanaikomesha tabia hiyo kwa kila anayehusika kwa kuwa wananfahamika.

  Aidha Monica Mchiro Diwani wa Kata ya Ludewa alikiri kufanyika kwa
  mkutano wa hadhara octoba 11 mwaka huu unaowahusu watu watano wanaotuhumiwa na Wananchi kuwatesa kwa nguvu za uchawi hata hivyo watuhumiwa akiwemo marehemu walikana kuhusika na matukio hayo.

  Bi
  Monica aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa polisi na ofisi za vijiji na Kata kuhusu uhalifu wowote uanotokea katika maeneo yao.

  Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundala amemwagiza mkuu wa polisi wilaya kuhakikisha wale wote waliohusika na ukatili huo wanakamatwa haraka na kupelekwa mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

  Aidha Bundala amekemea vikali tabia hiyo na kusema kuwa kwa jamii iliyoelimika haiwezi kufanya mambo kama hayo, na kuongeza kuwa kuna haja ya kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa namna ya kukabiliana na matukio kama hayo kwa kufuata sheria.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa
  Iringa Kamishna Msaidizi wa polisi Evarist Mangala alikiri kutokea kwa mauaji hayo na kwamba taarifa kamili atatoa baada ya kupata taarifa kamili ingawa alikiri kuwa chanzo cha

  mauaji ni imani za kishirikina.

  Source:
  Francis Godwin. Blogspot.com
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha mno.
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mmmmmmmmmmmmh,inatisha kwa kweli
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Maskini watoto bado wadogo wanaona baba yao anavyokufa kinyama..nawaonea huruma sana..
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,136
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  Watu wa vijijini wanamatatizo kweli, kisa cha kumchoma mwenzao kama hivyo ndo nini?
   
 6. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inabidi serikali iangalie upya swala la Kujichukulia Sheria mkononi.
   
 7. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Matatizo ya kujichukulia sheria mikononi ni mbaya sana kwa kweli
   
 8. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah maskini....tena amewiva haswa
   
 9. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nililisema hili kwenye post yangu ya ludewa mkanizodoa haya ona sasa bado watuhumiwa tisa wa kuchomwa. Mambo ya lifua hayo. Ukitaka picha za mikutano ya awali ninazo. Tulimshauri polisi wakata hakuelewa ona sasa tumepoteza mwananch na mali.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,171
  Trophy Points: 280
  kweli wachawi hawafi kirahisi, naona mzee unachangia thread ambayo wewe ni steringi
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaah!! Bujibuji bwana, watu wako kwenye majonzi nawe unaleta utani..
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ludewa ni Wilaya yenye "matatizo maalum" katika nyanda za juu kusini - na Mbozi pia!
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mbozi ni noma asee!!
   
 14. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  buji buji yaani nimeamini kila ufanyalo Linaendana na avatar yako. Mzee mzima NKEM (Long John) yaani nimejikuta nacheka msibani.
   
 15. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  sheria mkononi si sawa hata kama alikuwa mchawi.
   
 16. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  kama alishauriwa na yeye hakusikia ulitakawafanyeje////???
   
 17. L

  Leliro Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtindo huu, kijijini si mahala pa kuishi!
   
 18. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hawa watoto watakuja kerivenji
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Jamani acheni uchawi!
   
 20. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Tumrudie Mungu jamani. Dhambi sana.
   
Loading...