Natumai siku inaenda vizuri kwa kila mmoja wetu!
Nilikua napitia video moja ya huyu kaka anaita Nick Vujicic (Ningependa kila mmoja amtafute google au youtube). Yaani nikifika kwenye point ya kukata tama, maisha ya huyu kaka yananiinua moyo saana. Amezaliwa bila mikono wala miguu lakini kajikubali na hajaruhusu hali yake imrudishe nyuma... Anafanya vitu ambavyo ata wengi wetu wenye viungo vyote vya mwili tunashindwa fanya.
Ata siku moja tusiruhusu madhaifu yetu yaturudishe nyuma kwenye mahusiano, familia, taaluma ata kwenye elimu na kwenye jamii. Mungu hakukosea kutuumba hivi na kamwe tusijitafutie kasoro. Badilisha unavyojiona mwenyewe na utafanikiwa sana, siri ni kujiamini, kua jasiri na usikate tamaa.!
View attachment 481536View attachment 481537View attachment 481539View attachment 481540View attachment 481541View attachment 481542View attachment 481543View attachment 481544View attachment 481545