Ielewe Chadema..,hii ndio tofauti yake na CCM...!

attachment.php
[/QUOT

the truth is still the truth.."
 
Mwaka 2010-12 tulishuhudia matukio mengi yakijiri ndani ya taifa letu, ni matukio yaliyonasibishwa na siasa na kukua kwa demokrasia.,kulingana na muundo na mitindo ya utokeaji wake wengi tuliamini kuwa siasa katika Tanzania imepata muamko mpya na inashika hatamu katika kuleta mabadiliko ya kinchi katika Nyanja zote ambako siasa inagusa ama inahusika moja kwa moja, hapa nikijumuisha uchumi, tamaduni na jamii.

Katika matukio, lipo moja lilikuwa very significant and relative to what I am writing today.,nalo ni kukua na kutanuka kwa CDM mpaka kufikia kuwa chama kikubwa cha upinzani chenye mikiki na mabavu tele tena shupavu mbele ya CCM.,kushindwa na kufanikiwa kwake.

Kukua kwa chama hiki hakujatokea ghafla ama kwa bahati nasibu ni kwa kuwa kulikuwapo na mipango thabiti tena ya muda mrefu ya kuhakikisha chama hiki kinakua na kufikia malengo yake ya kuchukua nchi na kutawala dola. Kwa kuwa lengo langu si kuelezea historia ya kukua kwa CDM sitaingia ndani katika kulieleza hili.

Lengo kuu la waraka huu ni kueleza kupoteza kwangu matumaini na hamu ya kuwa shabiki wa siasa za Tanzania na imani yangu kuwa Siasa na wanasiasa wetu wanao uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya jamii ya watanzania ambao wapo katika dimbwi la umasikini na dhiki kuu. Nimepoteza imani kwao.



Kutokana na propaganda zilizopenyeshwa na kukubalika katika vichwa vya wengi ni kuwa hali ngumu ya maisha ya watanzania imeletwa na uongozi mbaya wa serikali ya CCM, ambayo wizi, ujambazi, uporaji, ufisadi, rushwa, elimu isiyo na tija(hafifu), uongozi wa kupeana (unprofessionalism) njaa,magonjwa,miundombinu hafifu,na mengineyo yameonekana kutawala. Kwa kiasi kikubwa kama si kwa asilimia zote nilikubaliana na hili, na nikawa attentive, makini na kujiaminisha kuwa hawa wanao address matatizo haya wanakuja na mbinu mbadala na mawazo tatuzi katika kushughulikia hali hii, na si mimi pekee bali watanzania walio wengi hasa wa mijini tuliamini hivyo.

Kushindwa kwa CDM;

Kulingana na yanayoendelea hivi sasa ndani ya CDM kikiwa kama chama kikubwa cha upinzani kunaonyesha dhairi kushindwa kwake katika kufikiri juu ya njia sahihi na mbinu piganizi katika kuyashughulikia matatizo yanayowakabili watanzania kiuchumi, kiutawala, pamoja na kijamii.
Na nitayazungumza machache na kwa mifano ili watu wapate kuelewa kiunaga ubaga.

1: Katika ufisadi,

CDM haijaonesha mipango thabiti juu ya kulishughulikia suala la ufisadi nchini zaidi ya kuitisha maandamano ya kupinga kulipwa mafisadi ambao wanabebwa na mahakama, hili linaonyesha ni kwa kiasi gani hakuna mipango thabiti,ya muda mrefu na endelevu juu ya kuzuia mianya ya rushwa, hali zinazopelekea rushwa na hata kutoa direction ya adhabu na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa mikakati hiyo ya kupambana na rushwa bali tumeona kuwa wapo viongozi katika CDM ambao wanapropagate ufisadi katika nafasi zao ndogo walizonazo hali inayotoa ishara ni kwa kiasi gani wanaweza kuwa pindi wakipata nafasi kubwa, kumbuka ya Mshahara wa Dk Slaa, kumbuka Magari ya Mbowe, kumbuka ukwepaji wa kodi wa chama, yale ya diwani kule Mara, n.k

2: Katika nchi ambayo demokrasia ni msingi na daraja la kuendea utawala wa sheria, wananchi (wapiga kura) lazima wawe na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi wanayotakiwa kuyachukua pindi wanapotumia fursa yao ya kupiga kura, Katika hili CDM wamekuwa mbele kulalamika na kupinga matokeo bila kufanya study yakinifu juu ya uhalisia wa wapiga kura Tanzania, wakiwa wanatumia sample space ambayo ni irrelevant kwa wakazi wa mijini na watumiaji wa mitandao katika kufanya tathmini zao za ushindi ama kushindwa., katika uchaguzi mkuu uliopita na zingine ndogondogo kama igunga, Mwanza na mara tathmini za kwenye mitandao zilionyesha kuwa CDM itashinda kwa kishindo na matokeo yamekuja tofauti mara zote katika chaguzi zote, na ni baada ya matokeo ndipo CDM hukakamaa na kunadi kuibiwa kura baada ya kutulia na kujifanyia tathmini yakinifu. UKWELI NI KUWA..,wapiga kura walio wengi ni watu wa vijijini ambao wengi katika wao ni masikini wa kutupwa , kulingana na ripoti ya benki ya dunia iliyotolewa October mwaka jana ni kuwa asilimia 83 ya masikini huishi vijijini,ambao katika hao milioni 6.4 wanaishi katika mstari wa umasikini wa kukosa chakula, milioni 10 wanakabiliwa na kukosa chakula kwa msimu-kwa maana wanakuwa nacho kipindi cha mavuno na kabla ya kipindi cha masika kinawaishia.,wengine milioni 12.7 hawapati mahitaji yao ya msingi, hii ikimaanisha kuwa zaidi ya watanzania milioni 30 wanaishi katika umasikini wa kutupwa idadi ambayo ni kubwa maradufu ukulinganisha na hapo nyuma na ni idadi inaonyesha kukua kwa umasikini na kufilisika kwa serikali inayotakiwa kuwahudumia watu hawa.
Katika hali kama hiyo watu hawa lazima watadanganyika kwa kupikiwa wali, kupewa t-shirt na kofia lakini pia watanunulika kwa bei rahisi sana, hali inayowawezesha viongozi wasio na nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo kujipenyeza kwa urahisi na kupata uongozi, wakati hali iko hivi huko vijijini CDM wao wako busy ARUSHA wakiandamana na kulala nje,wapo jamiiforums wakiipiga vijembe CCM, wakiunda blogs na kutengeneza website za kukusanya maoni ya watanzania kana kwamba watanzania wote wanatumia internet, wakati takwimu zinatuambia watanzania pungufu ya milioni mbili ambao wanatumia mtandao, mambo haya hayana mashiko wala msingi kiasi cha kupewa kipaumbele kiasi hiki. Lakini kuigawa siasa ya Tanzania kwa kigezo cha kanda na kuimarisha baadhi ya watu Fulani na kabila Fulani kwa kuwapa stahili kubwa katika chama, nafasi za uongozi hayana mvuto wala uhalisia wa siasa za Tanzania,CDM ipo Arusha kwa kila nguvu kana kwamba hakuna maeneo yenye kuhitaji usimamizi wa karibu wa kisiasa na kiuchumi bali ni Arusha pekee.

Lakini kama hayo hayatoshi, ni kuwa wakati serikali ikishindwa kusimamia fedha na miradi inayoelekezwa katika maeneo ya vijijini CDM inashindwa kuweka mkakati wa ufuatiliaji na taasisi ya kuhoji matumizi na utekelezaji ( hili linawezekana kisheria) ambapo kupitia taasisi hiyo usimamizi utaimarika lakini pia wapiga kura watapata mrejesho na kushuhudia nia ya kweli ya wanasiasa wao ya kuwaletea maendeleo.

3:Kulingana na mfumo wa sasa wa kiuchumi wa soko holela ambapo wenye nacho hupata fursa ya kujitajirisha zaidi kwa kupitia migongo ya walalahoi, CDM inayofursa ya kutoa muelekeo wa uchumi na mfumo unaojali na kugusa pande zote kwa kushauriana na wachumi walionao na kuandaa proposal ya sera zenye kulenga mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha,kodi, biashara, mishahara,na miamala mbalimbali katika sekta tofauti za kiuchumi hususani kilimo, ambapo watanzania walio wengi wamejiajiri huko. Na hili lazima lifanyike chini ya wataalamu wa uchumi na fedha lakini hili halijadhihiri hata kwenye bajeti yao mbadala.

4: katika mambo yanayopigiwa kelele katika uongozi chini ya serikali ya CCM ni undugunization katika ajira na mgawanyo wa vyeo na madaraka, katika hili CDM tuliamini watakuja na mbinu tofauti ya kuhakikisha kuwa vyeo na madaraja ya kazi yanagawanywa kulingana na uwezo, elimu na nafasi ya mtu,lakini tofauti na matarajio ya wengi bado ipo system ya kulimbikiziana vyeo ndani ya CDM, watu kama mnyika na wengineo wanavyo vyeo zaidi ya vitatu wakati mmoja kana kwamba hakuna vijana wengine katika CDM walio na uwezo na elimu ya kushika nafasi hizo. Lakini pia upo upendeleo wa dhahiri wa kupeana vyeo kwa nasabu na ukoo, ipo mifano katika hili, Tundu lissu na dada yake, Slaa na hawara yake,Ndesamburo na mwanae,mbowe na familia ya Mtei n.k

5: kupoteza umaarufu na kushindwa ushawishi kwa jamii.,hivi sasa kwa mtu aliye makini na siasa za ndani ya nchi, anaweza kugundua kwa urahisi kuwa CDM wamepoteza umaarufu na ushawishi kwa watanzania, umaarufu ambao ulipatikana kwa gharama kubwa na akili nyingi, hii inatokana na kupoteza uelekeo kwa media outlet zinazotumiwa na chadema, mfano wa magazeti kama mwanahalisi,mtanzania,Tanzania daima, majira, mwananchi na social medias kama jamii forums ama jambo forums,amua sasa blog n.k ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa na mvuto mkubwa kwa watanzania wapenda habari lakini kutokana na kuandika kwa mlengwa mmoja na kwa muda mrefu bila kubadilika zimepoteza ladha na thamani yake kwa watanzania na upendeleo, upotoshaji wa dhahiri pamoja na uchochezi vimechangia kuondoa hadhi na heshima ya vyombo hivi kwa watanzania wanahabari na wapenda habari.

6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wa kweli wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu., ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao na hasa vijana katika nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM. Kisa cha Zitto na Mbowe kipo dhahiri katika kutoa picha ya suala hili. Shibuda na “godfathers” ndani ya CDM.

Kwa kuhofia kuwachosha wasomaji, nitasitisha hapo na mengine naweza nikayazungumza kama sehemu ya comments, ila kwa kumaliza nitasema kuwa MTANZANIA TAMBUA WAZI KUWA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE NA NI JUKUMU LAKO WALA SI LA YULE.,ACHA KULALAMIKA, ACHA KUANDAMANA HOLELA, ACHA KUPIGA MAYOWE, CHUKUA HATUA ZA KWELI ZA KULETA MABADILIKO YA KWELI BILA KUFUNGWA KATIKA ITIKADI AMA IMANI.,BALI KWA MSUKUMO WA UTANaZANIA WAKO NA UTAIFA WAKO.…!

Nyinyiemu wote ndembe@dhaifu
 
hivi ni lini watu wa ccm mkakubali udhaifu wenu kama chama chenu kingekuwa kinafanya yale wanayotaka Watanzania leo hii Chadema kisingekuwa na umaarufu wowote.
Mmejisahau mnafanya ufisadi,mnashindwa kusimamia rasilimali za nchi na kuachwa kuchukuliwa lirahisi na mataifa ya nje kwanini hamjifunzi kutoka kwa chama cha kikomunisti cha China ambacho kimeendelea kubadilika kutokana na wakati na wakati huo huo kukataa kufunga ndoa na mafisadi kuwepo kwa chama cha upinzani kama Chadema kuna manufaa makubwa kwenu kwani kunawapa fursa ya kujitathimini kama maamuzi mnayofanya ni kweli yanakidhi matakwa ya watanzania
mliliondoa Azimio la Arusha lakini leo hii kwenye kila mjadala watu bado wanalilia
Mlisimamia muungano lakini mlikaa kimya pale katiba ya muungano ilipovunjwa na Wazanzibar leo hii chokochoko zote za muungano zimechangiwa na uongozi wenu dhaifu
Mwisho nakushauri badala ya kuwalaumu Chadema angalieni wapi mmejikwaa na kuchukua hatua kujaribu kurejesha imani ya wananchi waliyokuwa nayo kwenu
 
hivi ni lini watu wa ccm mkakubali udhaifu wenu kama chama chenu kingekuwa kinafanya yale wanayotaka Watanzania leo hii Chadema kisingekuwa na umaarufu wowote.
Mmejisahau mnafanya ufisadi,mnashindwa kusimamia rasilimali za nchi na kuachwa kuchukuliwa lirahisi na mataifa ya nje kwanini hamjifunzi kutoka kwa chama cha kikomunisti cha China ambacho kimeendelea kubadilika kutokana na wakati na wakati huo huo kukataa kufunga ndoa na mafisadi kuwepo kwa chama cha upinzani kama Chadema kuna manufaa makubwa kwenu kwani kunawapa fursa ya kujitathimini kama maamuzi mnayofanya ni kweli yanakidhi matakwa ya watanzania
mliliondoa Azimio la Arusha lakini leo hii kwenye kila mjadala watu bado wanalilia
Mlisimamia muungano lakini mlikaa kimya pale katiba ya muungano ilipovunjwa na Wazanzibar leo hii chokochoko zote za muungano zimechangiwa na uongozi wenu dhaifu
Mwisho nakushauri badala ya kuwalaumu Chadema angalieni wapi mmejikwaa na kuchukua hatua kujaribu kurejesha imani ya wananchi waliyokuwa nayo kwenu


If you cheat me once, shame on you! if you cheat me TWICE SHAME ON ME!!

WATANZANIA NINADHANI WAMESHAGUNDUA MUONGO NI NANI! cha ajabu watu wanatusikitisha humu kwa KUJA NA KUJIFANYA WANAIPENDASAAAAAAAAAANA CCM ETI INAONEWA, KUMBE WAO NDIO WANAIDIMIZA SAAAAAAAANA CCM! YAANI SIJUI WAMELIPWA NINI KUJA KUIANGAMIZA CCM NAMNA HII WALE WENYE AKILI KUBWA WALIOKO CCM WAMEOGOPA NA KUKAA KIMYA NA KUWAACHA WENYE AKILI NDOGO KAMA HUYU KUTAMBA NA KUSEMA WANAONEWA AU ! KUTOKUBALI MAKOSA!! KUNA MSEMO .......ACCEPT MISTAKES A FOOL WILL NEVER ACCEPT HIS OR HER MISTAKES!! TENA WENGINE NI POSHO HIZO ZA MAFISADI ZINAWASUMBUA TU!! MTU ANAKUJA ANAANDIKA MENGI ILI JIONI AKASAINI POSHO YA MUDA MFUPI HADI AKAUZA UTU NA AKILI ZAKE PUMBA TU!!
 
Back
Top Bottom