Ielewe Chadema..,hii ndio tofauti yake na CCM...!

Rapkatuni

Member
Sep 27, 2011
29
5
Mwaka 2010-12 tulishuhudia matukio mengi yakijiri ndani ya taifa letu, ni matukio yaliyonasibishwa na siasa na kukua kwa demokrasia.,kulingana na muundo na mitindo ya utokeaji wake wengi tuliamini kuwa siasa katika Tanzania imepata muamko mpya na inashika hatamu katika kuleta mabadiliko ya kinchi katika Nyanja zote ambako siasa inagusa ama inahusika moja kwa moja, hapa nikijumuisha uchumi, tamaduni na jamii.

Katika matukio, lipo moja lilikuwa very significant and relative to what I am writing today.,nalo ni kukua na kutanuka kwa CDM mpaka kufikia kuwa chama kikubwa cha upinzani chenye mikiki na mabavu tele tena shupavu mbele ya CCM.,kushindwa na kufanikiwa kwake.

Kukua kwa chama hiki hakujatokea ghafla ama kwa bahati nasibu ni kwa kuwa kulikuwapo na mipango thabiti tena ya muda mrefu ya kuhakikisha chama hiki kinakua na kufikia malengo yake ya kuchukua nchi na kutawala dola. Kwa kuwa lengo langu si kuelezea historia ya kukua kwa CDM sitaingia ndani katika kulieleza hili.

Lengo kuu la waraka huu ni kueleza kupoteza kwangu matumaini na hamu ya kuwa shabiki wa siasa za Tanzania na imani yangu kuwa Siasa na wanasiasa wetu wanao uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya jamii ya watanzania ambao wapo katika dimbwi la umasikini na dhiki kuu. Nimepoteza imani kwao.

Kutokana na propaganda zilizopenyeshwa na kukubalika katika vichwa vya wengi ni kuwa hali ngumu ya maisha ya watanzania imeletwa na uongozi mbaya wa serikali ya CCM, ambayo wizi, ujambazi, uporaji, ufisadi, rushwa, elimu isiyo na tija(hafifu), uongozi wa kupeana (unprofessionalism) njaa,magonjwa,miundombinu hafifu,na mengineyo yameonekana kutawala. Kwa kiasi kikubwa kama si kwa asilimia zote nilikubaliana na hili, na nikawa attentive, makini na kujiaminisha kuwa hawa wanao address matatizo haya wanakuja na mbinu mbadala na mawazo tatuzi katika kushughulikia hali hii, na si mimi pekee bali watanzania walio wengi hasa wa mijini tuliamini hivyo.

Kushindwa kwa CDM;

Kulingana na yanayoendelea hivi sasa ndani ya CDM kikiwa kama chama kikubwa cha upinzani kunaonyesha dhairi kushindwa kwake katika kufikiri juu ya njia sahihi na mbinu piganizi katika kuyashughulikia matatizo yanayowakabili watanzania kiuchumi, kiutawala, pamoja na kijamii.
Na nitayazungumza machache na kwa mifano ili watu wapate kuelewa kiunaga ubaga.

1: Katika ufisadi,

CDM haijaonesha mipango thabiti juu ya kulishughulikia suala la ufisadi nchini zaidi ya kuitisha maandamano ya kupinga kulipwa mafisadi ambao wanabebwa na mahakama, hili linaonyesha ni kwa kiasi gani hakuna mipango thabiti,ya muda mrefu na endelevu juu ya kuzuia mianya ya rushwa, hali zinazopelekea rushwa na hata kutoa direction ya adhabu na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa mikakati hiyo ya kupambana na rushwa bali tumeona kuwa wapo viongozi katika CDM ambao wanapropagate ufisadi katika nafasi zao ndogo walizonazo hali inayotoa ishara ni kwa kiasi gani wanaweza kuwa pindi wakipata nafasi kubwa, kumbuka ya Mshahara wa Dk Slaa, kumbuka Magari ya Mbowe, kumbuka ukwepaji wa kodi wa chama, yale ya diwani kule Mara, n.k

2: Katika nchi ambayo demokrasia ni msingi na daraja la kuendea utawala wa sheria, wananchi (wapiga kura) lazima wawe na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi wanayotakiwa kuyachukua pindi wanapotumia fursa yao ya kupiga kura, Katika hili CDM wamekuwa mbele kulalamika na kupinga matokeo bila kufanya study yakinifu juu ya uhalisia wa wapiga kura Tanzania, wakiwa wanatumia sample space ambayo ni irrelevant kwa wakazi wa mijini na watumiaji wa mitandao katika kufanya tathmini zao za ushindi ama kushindwa., katika uchaguzi mkuu uliopita na zingine ndogondogo kama igunga, Mwanza na mara tathmini za kwenye mitandao zilionyesha kuwa CDM itashinda kwa kishindo na matokeo yamekuja tofauti mara zote katika chaguzi zote, na ni baada ya matokeo ndipo CDM hukakamaa na kunadi kuibiwa kura baada ya kutulia na kujifanyia tathmini yakinifu. UKWELI NI KUWA..,wapiga kura walio wengi ni watu wa vijijini ambao wengi katika wao ni masikini wa kutupwa , kulingana na ripoti ya benki ya dunia iliyotolewa October mwaka jana ni kuwa asilimia 83 ya masikini huishi vijijini,ambao katika hao milioni 6.4 wanaishi katika mstari wa umasikini wa kukosa chakula, milioni 10 wanakabiliwa na kukosa chakula kwa msimu-kwa maana wanakuwa nacho kipindi cha mavuno na kabla ya kipindi cha masika kinawaishia.,wengine milioni 12.7 hawapati mahitaji yao ya msingi, hii ikimaanisha kuwa zaidi ya watanzania milioni 30 wanaishi katika umasikini wa kutupwa idadi ambayo ni kubwa maradufu ukulinganisha na hapo nyuma na ni idadi inaonyesha kukua kwa umasikini na kufilisika kwa serikali inayotakiwa kuwahudumia watu hawa.
Katika hali kama hiyo watu hawa lazima watadanganyika kwa kupikiwa wali, kupewa t-shirt na kofia lakini pia watanunulika kwa bei rahisi sana, hali inayowawezesha viongozi wasio na nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo kujipenyeza kwa urahisi na kupata uongozi, wakati hali iko hivi huko vijijini CDM wao wako busy ARUSHA wakiandamana na kulala nje,wapo jamiiforums wakiipiga vijembe CCM, wakiunda blogs na kutengeneza website za kukusanya maoni ya watanzania kana kwamba watanzania wote wanatumia internet, wakati takwimu zinatuambia watanzania pungufu ya milioni mbili ambao wanatumia mtandao, mambo haya hayana mashiko wala msingi kiasi cha kupewa kipaumbele kiasi hiki. Lakini kuigawa siasa ya Tanzania kwa kigezo cha kanda na kuimarisha baadhi ya watu Fulani na kabila Fulani kwa kuwapa stahili kubwa katika chama, nafasi za uongozi hayana mvuto wala uhalisia wa siasa za Tanzania,CDM ipo Arusha kwa kila nguvu kana kwamba hakuna maeneo yenye kuhitaji usimamizi wa karibu wa kisiasa na kiuchumi bali ni Arusha pekee.

Lakini kama hayo hayatoshi, ni kuwa wakati serikali ikishindwa kusimamia fedha na miradi inayoelekezwa katika maeneo ya vijijini CDM inashindwa kuweka mkakati wa ufuatiliaji na taasisi ya kuhoji matumizi na utekelezaji ( hili linawezekana kisheria) ambapo kupitia taasisi hiyo usimamizi utaimarika lakini pia wapiga kura watapata mrejesho na kushuhudia nia ya kweli ya wanasiasa wao ya kuwaletea maendeleo.

3:Kulingana na mfumo wa sasa wa kiuchumi wa soko holela ambapo wenye nacho hupata fursa ya kujitajirisha zaidi kwa kupitia migongo ya walalahoi, CDM inayofursa ya kutoa muelekeo wa uchumi na mfumo unaojali na kugusa pande zote kwa kushauriana na wachumi walionao na kuandaa proposal ya sera zenye kulenga mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha,kodi, biashara, mishahara,na miamala mbalimbali katika sekta tofauti za kiuchumi hususani kilimo, ambapo watanzania walio wengi wamejiajiri huko. Na hili lazima lifanyike chini ya wataalamu wa uchumi na fedha lakini hili halijadhihiri hata kwenye bajeti yao mbadala.

4: katika mambo yanayopigiwa kelele katika uongozi chini ya serikali ya CCM ni undugunization katika ajira na mgawanyo wa vyeo na madaraka, katika hili CDM tuliamini watakuja na mbinu tofauti ya kuhakikisha kuwa vyeo na madaraja ya kazi yanagawanywa kulingana na uwezo, elimu na nafasi ya mtu,lakini tofauti na matarajio ya wengi bado ipo system ya kulimbikiziana vyeo ndani ya CDM, watu kama mnyika na wengineo wanavyo vyeo zaidi ya vitatu wakati mmoja kana kwamba hakuna vijana wengine katika CDM walio na uwezo na elimu ya kushika nafasi hizo. Lakini pia upo upendeleo wa dhahiri wa kupeana vyeo kwa nasabu na ukoo, ipo mifano katika hili, Tundu lissu na dada yake, Slaa na hawara yake,Ndesamburo na mwanae,mbowe na familia ya Mtei n.k

5: kupoteza umaarufu na kushindwa ushawishi kwa jamii.,hivi sasa kwa mtu aliye makini na siasa za ndani ya nchi, anaweza kugundua kwa urahisi kuwa CDM wamepoteza umaarufu na ushawishi kwa watanzania, umaarufu ambao ulipatikana kwa gharama kubwa na akili nyingi, hii inatokana na kupoteza uelekeo kwa media outlet zinazotumiwa na chadema, mfano wa magazeti kama mwanahalisi,mtanzania,Tanzania daima, majira, mwananchi na social medias kama jamii forums ama jambo forums,amua sasa blog n.k ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa na mvuto mkubwa kwa watanzania wapenda habari lakini kutokana na kuandika kwa mlengwa mmoja na kwa muda mrefu bila kubadilika zimepoteza ladha na thamani yake kwa watanzania na upendeleo, upotoshaji wa dhahiri pamoja na uchochezi vimechangia kuondoa hadhi na heshima ya vyombo hivi kwa watanzania wanahabari na wapenda habari.

6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wa kweli wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu., ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao na hasa vijana katika nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM. Kisa cha Zitto na Mbowe kipo dhahiri katika kutoa picha ya suala hili. Shibuda na “godfathers” ndani ya CDM.

Kwa kuhofia kuwachosha wasomaji, nitasitisha hapo na mengine naweza nikayazungumza kama sehemu ya comments, ila kwa kumaliza nitasema kuwa MTANZANIA TAMBUA WAZI KUWA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE NA NI JUKUMU LAKO WALA SI LA YULE.,ACHA KULALAMIKA, ACHA KUANDAMANA HOLELA, ACHA KUPIGA MAYOWE, CHUKUA HATUA ZA KWELI ZA KULETA MABADILIKO YA KWELI BILA KUFUNGWA KATIKA ITIKADI AMA IMANI.,BALI KWA MSUKUMO WA UTANZANIA WAKO NA UTAIFA WAKO.…!
 
6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wa kweli wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu., ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao na hasa vijana katika nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM. Kisa cha Zitto na Mbowe kipo dhahiri katika kutoa picha ya suala hili. Shibuda na "godfathers" ndani ya CDM.

Kwa kuhofia kuwachosha wasomaji, nitasitisha hapo na mengine naweza nikayazungumza kama sehemu ya comments, ila kwa kumaliza nitasema kuwa MTANZANIA TAMBUA WAZI KUWA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE NA NI JUKUMU LAKO WALA SI LA YULE.,ACHA KULALAMIKA, ACHA KUANDAMANA HOLELA, ACHA KUPIGA MAYOWE, CHUKUA HATUA ZA KWELI ZA KULETA MABADILIKO YA KWELI BILA KUFUNGWA KATIKA ITIKADI AMA IMANI.,BALI KWA MSUKUMO WA UTANZANIA WAKO NA UTAIFA WAKO.…!
Gamba ulijipanga ukajifungia na NEPI kuandaa huu upuuzi. Movement yoyote lazima iongozwe!! Umechemsha Gamba and for your info GAMBA maskini hujui We CDM have the CSO movement with us. Hang yourself!!!
 
Nimekuwa na shauku kusoma baada ya kuona lundo la maandishi kumbe utumbo wa juzi!.
Umechelewa kuuleta, labda ungekuwa na mvuto fulani kama ungeuleta miaka minne mitatu hivi iliyopita.
Kwasasa kuona mtu akiamini uliyoyaandika nitaamini kuwa yuko miaka minne nyuma.
Yaani anaishi 2009 ndani ya 2012 kama wewe!.
 
Mleta mada naomba nikusahihishe hapo unasome kuwa watu wanalalamika kudhusu 'undugunisation'. Sio sahihi.

Tatizo sio undugunisation bali vigezo. Watu wanastahili? Na chimbuko la hili ni utendaji mbovu wa baadhi ya wakubwa wa ccm lakini bado wapo kwenye nafasi zao. Katika hali hiyo sifa moja wanayobakia nayo ni 'undugu' na sio uwezo maana kama ni uwezo hawana. Nitakupa mfano; Ni kitu gani cha maana amefanya Hawa Ghasia? Au nini cha maana amefanya Prof Maghembe, angalia wizara zote alizoshika!

Hata kama watu wanatoka familia moja lakini kama wanafanya mambo yanaonekana sidhani kama watanzania wangelalamika. Lakini shida inakuja mtu anavurga kila wizara watu wanalalamika tena toka ndani ya chama lakini wanahamishiwa sehemu nyingine, ile iweje?

Mwisho, huwezi kuhalalisha utendaji mbaya wa ccm kwa kutumia chama kingine. Ni kupoteza muda.
 
TUNTEMEKE kashakuja na 'id' 19 tofauti. Ameanza toka jana kwnye thread ya Mbowe na shangingi la KUB. Bwana TUNTE kwasasa watz hawadanganywi na uvumi wwte. Watz wa leo sio wale walokuwa wakipiga makofi barabarani kumpokea mkuu wa wilaya, mkoa na viongozi wengine. Wewe kama ulinyimwa madarakahuko walokunyima walikuwa sahihi na waliona mbali. Hata uchufue vp CDM inazidi kusonga mbele na 2015 lazima ichkue Dola. Hatakama nao hawako smart ngoja 2waadabishe ccm kwanza ili wa2achie serikali.
 
Mabadiliko ya kweli yatakuja tu pale CCM itakapokuwa voted OUT. With CCM we are doomed
 
Hapa ndio utakijuwa kikwapa cha mgwanda kinavyotoa.

Hakuna ataekuja kujibu hoja, watakuja na matusi, huwa hawana hoja, tena wengi wa wanaojibu bila hoja humu ni haohao wabunge wa upinzani.
 
Hii thread yako inasanifu id yako, nashukuru kwa huu uzi wako kwa kuwa unakupa faraja wewe na magamba wenzako, lakini kwa wenye akili wanapima na kuchuja, kama unachuki binafsi na chadema kwa kipindi hiki utakufa kwa presha, ila siombei ufe ili chadema ikiwa inachanja mbuga wewe na magamba wenzako ambao hawaamini wawe mashuhuda
 
Umerukaruka weee na kutuchosha kusoma na kulaumu lakini mwisho wake umeshindwa kusema nini kifanyike au CDM wajirekebishe watu. Sana sana naona kama unashawishi tuendelee kuibeba ccm wakati inaumwa Nyambulila, ule ugonjwa wa kufa huku unajiona. Kwanza umeng'ang'ania Arusha wakati sisi huku Simiyu tuna wabunge wawili wa CDM na CCM nayo inao wawili kwa hiyo uArusha unaotaka kutushawishi ni unafiki.

Kazi ya kukamata rushwa na ufisadi sio ya CDM, wao wanatimiza wajibu wao kama whistle blowers lakini wakamataji ni takukuru ambao chama chenu cha magamba kimewakataza wasikamate.

Kifupi umepoteza muda wako bure kuandika rubbish na haujaeleza suluhisho la matatizo ya watanzania. Pia kama una muda soma alternative budget ya upinzani uone kama CDM hawana mawazo mbadala kama unavyotudanganya. Kwa kumalizia ni kwamba wewe mleta mada ni gamba

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nilitulia kidogo ili ni some, kila nilipokuwa naendelea kusoma niligundua vitu vingi.

.1:wewe ni mkereketwa wa nepi

2:kauli jk ni dhaifu ndio imekutuma kuandika haya.

3. Nimegundua kuwa hujui ata ulicho kiandika kwenye title ya thread

4. Nikagundua wewe ni mr zilipendwa maana unaongea mambo ya kizamani.

5 nikagundua unatatizo la amnesia

6.nikagundua wewe ni kada unayetumiwa na nepi kuweka booking ya wali maharage kwenye mikutano yenu.
 
Umerukaruka weee na kutuchosha kusoma na kulaumu lakini mwisho wake umeshindwa kusema nini kifanyike au CDM wajirekebishe watu. Sana sana naona kama unashawishi tuendelee kuibeba ccm wakati inaumwa Nyambulila, ule ugonjwa wa kufa huku unajiona. Kwanza umeng'ang'ania Arusha wakati sisi huku Simiyu tuna wabunge wawili wa CDM na CCM nayo inao wawili kwa hiyo uArusha unaotaka kutushawishi ni unafiki.

Kazi ya kukamata rushwa na ufisadi sio ya CDM, wao wanatimiza wajibu wao kama whistle blowers lakini wakamataji ni takukuru ambao chama chenu cha magamba kimewakataza wasikamate.

Kifupi umepoteza muda wako bure kuandika rubbish na haujaeleza suluhisho la matatizo ya watanzania. Pia kama una muda soma alternative budget ya upinzani uone kama CDM hawana mawazo mbadala kama unavyotudanganya. Kwa kumalizia ni kwamba wewe mleta mada ni gamba

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu huyu mleta Topic anauelewa kama wa Ngereja aliyekosa la kuchangia akaishia kuongelea mambo yaliyosababishwa na makosa ya uchapaji (typing error) kwenye maoni ya kambi ya upinzani kuhusu bajeti. Ameumbuliwa na Mh. Mdee akatulia sasa na huyu ulivyomuumbua atatulia tu.
 
ccm ina kazi kuwalipa wapuuzi wote kama nyinyi ni kupoteza muda wenu mmeshindwa kuwabadilisha mawazo manzese wakawatoza how about us mmeishiwa:dance:
 
Mwaka 2010-12 tulishuhudia matukio mengi yakijiri ndani ya taifa letu, ni matukio yaliyonasibishwa na siasa na kukua kwa demokrasia.,kulingana na muundo na mitindo ya utokeaji wake wengi tuliamini kuwa siasa katika Tanzania imepata muamko mpya na inashika hatamu katika kuleta mabadiliko ya kinchi katika Nyanja zote ambako siasa inagusa ama inahusika moja kwa moja, hapa nikijumuisha uchumi, tamaduni na jamii.

Katika matukio, lipo moja lilikuwa very significant and relative to what I am writing today.,nalo ni kukua na kutanuka kwa CDM mpaka kufikia kuwa chama kikubwa cha upinzani chenye mikiki na mabavu tele tena shupavu mbele ya CCM.,kushindwa na kufanikiwa kwake.

Kukua kwa chama hiki hakujatokea ghafla ama kwa bahati nasibu ni kwa kuwa kulikuwapo na mipango thabiti tena ya muda mrefu ya kuhakikisha chama hiki kinakua na kufikia malengo yake ya kuchukua nchi na kutawala dola. Kwa kuwa lengo langu si kuelezea historia ya kukua kwa CDM sitaingia ndani katika kulieleza hili.

Lengo kuu la waraka huu ni kueleza kupoteza kwangu matumaini na hamu ya kuwa shabiki wa siasa za Tanzania na imani yangu kuwa Siasa na wanasiasa wetu wanao uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya jamii ya watanzania ambao wapo katika dimbwi la umasikini na dhiki kuu. Nimepoteza imani kwao.

Kutokana na propaganda zilizopenyeshwa na kukubalika katika vichwa vya wengi ni kuwa hali ngumu ya maisha ya watanzania imeletwa na uongozi mbaya wa serikali ya CCM, ambayo wizi, ujambazi, uporaji, ufisadi, rushwa, elimu isiyo na tija(hafifu), uongozi wa kupeana (unprofessionalism) njaa,magonjwa,miundombinu hafifu,na mengineyo yameonekana kutawala. Kwa kiasi kikubwa kama si kwa asilimia zote nilikubaliana na hili, na nikawa attentive, makini na kujiaminisha kuwa hawa wanao address matatizo haya wanakuja na mbinu mbadala na mawazo tatuzi katika kushughulikia hali hii, na si mimi pekee bali watanzania walio wengi hasa wa mijini tuliamini hivyo.

Kushindwa kwa CDM;

Kulingana na yanayoendelea hivi sasa ndani ya CDM kikiwa kama chama kikubwa cha upinzani kunaonyesha dhairi kushindwa kwake katika kufikiri juu ya njia sahihi na mbinu piganizi katika kuyashughulikia matatizo yanayowakabili watanzania kiuchumi, kiutawala, pamoja na kijamii.
Na nitayazungumza machache na kwa mifano ili watu wapate kuelewa kiunaga ubaga.

1: Katika ufisadi,

CDM haijaonesha mipango thabiti juu ya kulishughulikia suala la ufisadi nchini zaidi ya kuitisha maandamano ya kupinga kulipwa mafisadi ambao wanabebwa na mahakama, hili linaonyesha ni kwa kiasi gani hakuna mipango thabiti,ya muda mrefu na endelevu juu ya kuzuia mianya ya rushwa, hali zinazopelekea rushwa na hata kutoa direction ya adhabu na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa mikakati hiyo ya kupambana na rushwa bali tumeona kuwa wapo viongozi katika CDM ambao wanapropagate ufisadi katika nafasi zao ndogo walizonazo hali inayotoa ishara ni kwa kiasi gani wanaweza kuwa pindi wakipata nafasi kubwa, kumbuka ya Mshahara wa Dk Slaa, kumbuka Magari ya Mbowe, kumbuka ukwepaji wa kodi wa chama, yale ya diwani kule Mara, n.k

2: Katika nchi ambayo demokrasia ni msingi na daraja la kuendea utawala wa sheria, wananchi (wapiga kura) lazima wawe na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi wanayotakiwa kuyachukua pindi wanapotumia fursa yao ya kupiga kura, Katika hili CDM wamekuwa mbele kulalamika na kupinga matokeo bila kufanya study yakinifu juu ya uhalisia wa wapiga kura Tanzania, wakiwa wanatumia sample space ambayo ni irrelevant kwa wakazi wa mijini na watumiaji wa mitandao katika kufanya tathmini zao za ushindi ama kushindwa., katika uchaguzi mkuu uliopita na zingine ndogondogo kama igunga, Mwanza na mara tathmini za kwenye mitandao zilionyesha kuwa CDM itashinda kwa kishindo na matokeo yamekuja tofauti mara zote katika chaguzi zote, na ni baada ya matokeo ndipo CDM hukakamaa na kunadi kuibiwa kura baada ya kutulia na kujifanyia tathmini yakinifu. UKWELI NI KUWA..,wapiga kura walio wengi ni watu wa vijijini ambao wengi katika wao ni masikini wa kutupwa , kulingana na ripoti ya benki ya dunia iliyotolewa October mwaka jana ni kuwa asilimia 83 ya masikini huishi vijijini,ambao katika hao milioni 6.4 wanaishi katika mstari wa umasikini wa kukosa chakula, milioni 10 wanakabiliwa na kukosa chakula kwa msimu-kwa maana wanakuwa nacho kipindi cha mavuno na kabla ya kipindi cha masika kinawaishia.,wengine milioni 12.7 hawapati mahitaji yao ya msingi, hii ikimaanisha kuwa zaidi ya watanzania milioni 30 wanaishi katika umasikini wa kutupwa idadi ambayo ni kubwa maradufu ukulinganisha na hapo nyuma na ni idadi inaonyesha kukua kwa umasikini na kufilisika kwa serikali inayotakiwa kuwahudumia watu hawa.
Katika hali kama hiyo watu hawa lazima watadanganyika kwa kupikiwa wali, kupewa t-shirt na kofia lakini pia watanunulika kwa bei rahisi sana, hali inayowawezesha viongozi wasio na nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo kujipenyeza kwa urahisi na kupata uongozi, wakati hali iko hivi huko vijijini CDM wao wako busy ARUSHA wakiandamana na kulala nje,wapo jamiiforums wakiipiga vijembe CCM, wakiunda blogs na kutengeneza website za kukusanya maoni ya watanzania kana kwamba watanzania wote wanatumia internet, wakati takwimu zinatuambia watanzania pungufu ya milioni mbili ambao wanatumia mtandao, mambo haya hayana mashiko wala msingi kiasi cha kupewa kipaumbele kiasi hiki. Lakini kuigawa siasa ya Tanzania kwa kigezo cha kanda na kuimarisha baadhi ya watu Fulani na kabila Fulani kwa kuwapa stahili kubwa katika chama, nafasi za uongozi hayana mvuto wala uhalisia wa siasa za Tanzania,CDM ipo Arusha kwa kila nguvu kana kwamba hakuna maeneo yenye kuhitaji usimamizi wa karibu wa kisiasa na kiuchumi bali ni Arusha pekee.

Lakini kama hayo hayatoshi, ni kuwa wakati serikali ikishindwa kusimamia fedha na miradi inayoelekezwa katika maeneo ya vijijini CDM inashindwa kuweka mkakati wa ufuatiliaji na taasisi ya kuhoji matumizi na utekelezaji ( hili linawezekana kisheria) ambapo kupitia taasisi hiyo usimamizi utaimarika lakini pia wapiga kura watapata mrejesho na kushuhudia nia ya kweli ya wanasiasa wao ya kuwaletea maendeleo.

3:Kulingana na mfumo wa sasa wa kiuchumi wa soko holela ambapo wenye nacho hupata fursa ya kujitajirisha zaidi kwa kupitia migongo ya walalahoi, CDM inayofursa ya kutoa muelekeo wa uchumi na mfumo unaojali na kugusa pande zote kwa kushauriana na wachumi walionao na kuandaa proposal ya sera zenye kulenga mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha,kodi, biashara, mishahara,na miamala mbalimbali katika sekta tofauti za kiuchumi hususani kilimo, ambapo watanzania walio wengi wamejiajiri huko. Na hili lazima lifanyike chini ya wataalamu wa uchumi na fedha lakini hili halijadhihiri hata kwenye bajeti yao mbadala.

4: katika mambo yanayopigiwa kelele katika uongozi chini ya serikali ya CCM ni undugunization katika ajira na mgawanyo wa vyeo na madaraka, katika hili CDM tuliamini watakuja na mbinu tofauti ya kuhakikisha kuwa vyeo na madaraja ya kazi yanagawanywa kulingana na uwezo, elimu na nafasi ya mtu,lakini tofauti na matarajio ya wengi bado ipo system ya kulimbikiziana vyeo ndani ya CDM, watu kama mnyika na wengineo wanavyo vyeo zaidi ya vitatu wakati mmoja kana kwamba hakuna vijana wengine katika CDM walio na uwezo na elimu ya kushika nafasi hizo. Lakini pia upo upendeleo wa dhahiri wa kupeana vyeo kwa nasabu na ukoo, ipo mifano katika hili, Tundu lissu na dada yake, Slaa na hawara yake,Ndesamburo na mwanae,mbowe na familia ya Mtei n.k

5: kupoteza umaarufu na kushindwa ushawishi kwa jamii.,hivi sasa kwa mtu aliye makini na siasa za ndani ya nchi, anaweza kugundua kwa urahisi kuwa CDM wamepoteza umaarufu na ushawishi kwa watanzania, umaarufu ambao ulipatikana kwa gharama kubwa na akili nyingi, hii inatokana na kupoteza uelekeo kwa media outlet zinazotumiwa na chadema, mfano wa magazeti kama mwanahalisi,mtanzania,Tanzania daima, majira, mwananchi na social medias kama jamii forums ama jambo forums,amua sasa blog n.k ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa na mvuto mkubwa kwa watanzania wapenda habari lakini kutokana na kuandika kwa mlengwa mmoja na kwa muda mrefu bila kubadilika zimepoteza ladha na thamani yake kwa watanzania na upendeleo, upotoshaji wa dhahiri pamoja na uchochezi vimechangia kuondoa hadhi na heshima ya vyombo hivi kwa watanzania wanahabari na wapenda habari.

6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wa kweli wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu., ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao na hasa vijana katika nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM. Kisa cha Zitto na Mbowe kipo dhahiri katika kutoa picha ya suala hili. Shibuda na “godfathers” ndani ya CDM.

Kwa kuhofia kuwachosha wasomaji, nitasitisha hapo na mengine naweza nikayazungumza kama sehemu ya comments, ila kwa kumaliza nitasema kuwa MTANZANIA TAMBUA WAZI KUWA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE NA NI JUKUMU LAKO WALA SI LA YULE.,ACHA KULALAMIKA, ACHA KUANDAMANA HOLELA, ACHA KUPIGA MAYOWE, CHUKUA HATUA ZA KWELI ZA KULETA MABADILIKO YA KWELI BILA KUFUNGWA KATIKA ITIKADI AMA IMANI.,BALI KWA MSUKUMO WA UTANZANIA WAKO NA UTAIFA WAKO.…!

Umejitahidi mkuu kuelezea jinsi nchi inavyoenda. Ila umeshindwa kutambua kwamba cdm si chama tawala na mamlaka yote ya nchi ikiwemo mahakama viko chini ya serikali chini ya ccm. Ungesema ccm kwa haya yote ningekuelewa kwa kiasi kikubwa kabisa mkuu. jipange sawa sawa kutushawishi sisi wadau.
 
:dance::playball: hukutakiwa kuandika notes, lakini sikulaumu ndio kawaida ya gamba
 
attachment.php
 
Back
Top Bottom