Idara ya Uhamiaji iache kutumika kisiasa kwenye suala la Manji

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,536
John Msumule, Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar amesema kuwa lazima Mfanyabiashara Yusuf Manji afikishwe mahakamani na kushtakiwa kwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kuishi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Msumule amenukuliwa akisema "Hawa tutuwashtaki, ila hatutawashtaki pekee yao tutamuunganisha na Yusufu Manji ambaye ndio ameajiri watu hawa. Tulitaka kumkamata ilitumuunganishe lakini tumepata taarifa kuwa yuko hospitali amelazwa. Akitoka lazima aje hapa ili nayeye tumshtaki, hatutajali fedha wala cheo"

Lakini swali la msingi Manji anashtakiwa kama nani? Msumule amesema kuwa atashtakiwa kama muajiri. Je Manji ndiye afisa muajiri/rasilimali watu (HR) wa Quality Group? Jibu ni HAPANA. Manji si Afisa muajiri na hajawahi kuwa Afisa muajiri wa Quality Group.

Tangazo la tar.12 mwezi April mwaka 2016 lililochapwa na gazeti la "The Citizen" lilimnukuu Manji akitangaza kung'atuka nafasi zote za utendaji ndani ya Quality Group. Hivyo kwa sasa Manji si Muajiri, si Meneja, si Mkurugenzi, si mwenyekiti wa Bodi. Kwa kifupi alijitoa katika nafasi zote za kiutendaji na kubaki kuwa mshauri tu na mmoja wa wamiliki wa Quality Group ambayo ni kampuni ya familia.

Sasa unamshtaki vipi mtu wa namna hii unawaacha watendaji ambao wao ndio wanahusika moja kwa moja katika kuajiri? Hii inadhihirisha kuwa uamuzi huu wa Idara ya Uhamiaji wa kulazimisha kumshtaki Manji una nia ovu na umelenga kumkomoa.

Mwanasheria Belinda Chepchumba anasema "Manji ni shareholder tuu kumanisha hawezi kuwajibishwa kwa makosa ya waajiriwa wake (criminally liable for acts of employees). Kuna kitu kisheria kinaitwa lifting veil of incorporation na huwa inafanywa na mahakama tu na sio polisi wala idara ya uhamiaji. Na hiyo lifting of veil inawagusa wakurugenzi (Directors) na sio wahisani (shareholders). Hii ina maanisha kuwa Manji hawezi kuhusishwa (kwa vyovyote vile katika kesi hii) kwa sababu yeye ni shareholder tu. Idara ya Uhamiaji iwashtaki wakurugenzi, maafisa waajiri au watendaji wengine wa Quality Grpup na sio Manji ambaye ni shareholder tu. Warejee companies Act of Tanzania (ya mwaka 2002)."

Hata hivyo moja kati ya makampuni yaliyokutwa na wafanyakazi wasio na vibali ni kampuni ya saruji ya Dangote iliyopo mkoani Mtwara. Lakini mmiliki wa kampuni hiyo Ndg.Aliko Dangote hajatishiwa kukamatwa kama alivyotishiwa Manji. Badala yake upande wa Dangote Idara ya Uhamiaji imesema itamkamata Afisa Uajiri wa kampuni hiyo (Human Resource Officer).

Sasa kwanini kwa Dangote wamshtaki Afisa Uajiri lakini kwa Manji wamshtaki mmiliki? Hii ni double standard ya kijinga kabisa. Au kwa sababu Manji ni mwekezaji mzawa na Dangote ni mwekezaji mgeni? Kwahiyo katika nchi hii mgeni anathaminiwa kulko mzawa or? Idara ya Uhamiaji iache kutumika kisiasa.!
 
Walimwita kwa kosa la madawa ya kulevya, sasa wamekosa ushahidi wanamtwika kesi mpya kabisa wakati yeye alijiuzuru uongozi wa kampuni toka April mwaka jana, ndiyo maana wananchi huwa wana lalamka kuwa polisi wana tabia ya kubambikia watu kesi
 
Manji alijiuzulu April 2016 inawezekana hao wageni wasio na hati za ukaazi walianza kufanya kazi kwenye makampuni ya Manji wakati Manji bado yupo kwenye nafasi ya utendaji.
Uhamiaji wanaweza kuwa wamekosea kwa sababu kwanini hawakukagua hizo kampuni za Manji kipindi cha nyuma.
Manji naye amekosea kuajiri wageni ambao hawana hati za ukaazi ,kwa vyovyote vile Manji anafahamu kuwa kuna wafanyakazi wageni wanaofanya kazi bila vibali na kipindi cha nyuma hakukuwa na mtu mwenyewe ubavu wa kukagua makampuni yake.
Manji atashinda hii kesi lakini yeye binafsi na wafanyakazi wake wanatakiwa wafuate sheria za nchi utawala umebadirika na kila zama na kitabu chake.
 
Kila nikikumbuka yule mzee wa uhamiaji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nakasirika sana.

Na kwanini baada ya kutuhumiwa kwa madawa ya kulevya ndio umekuja mlolongo wa tuhuma?
Hili hawakulijua hapo kabla?

Au baada ya kuona kwenye madawa ya kulevya hana hatia ndio wanamtafutia namna ya kumkomoa?
Tunaojua yote haya ni rasharasha tu...mvua yenyewe ni kunduchi na ndio wanatafuta namna ya kuifikia.

Huu ni uonevu!
 
Kuna uovu mwingi unatuhumiwa kufanywa na wanaoitwa wafanyabiashara maarufu kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa waandamizi ..Yawezekana taifa likayumba ikiwa makaburi yatafukunyuriwa kama ipasavyo ili kubaini vinasaba vya wahusika katika ujangiri wa maendeleo yetu kwa miongo kadhaa..

Maridhiano ya kitaifa yawezekana yakawa suruhisho mahususi kwa mustakabari wa kuijenga nchi yetu.Pamoja na maridhiano,Tukae chini na kutafakari athari za maamuzi yetu,mikakati yetu,Mipango yetu,Mbinu zetu kisiasa,kiuongozi,kimaendeleo...

Tanzania ni nchi yetu,Maslahi ya nchi yapaswa kuwekwa mbele kabisa kuliko maslahi yetu binafsi
 
Tusitetee tu kwa sababu ya kutetea. Kwanza tujiulize kwa nini Manji ALIJIUZULU?
Tukijua hilo tutakuwa tumefunguka macho.

Kile Manji alichofanya ni TECHNICAL RESIGNATION/Kujiuzuli kwa kitekinikali ili kama AKISHITAKIWA kesi ISIGUSE kampuni yake. Hilo si siasa bali ni ujanja wake kujaribu kukwepa sheria.

Hata wale wafanyakazi wa kigeni waliobaki. WACHUNGUZWE ili kudhibitisha zile kazi wanazozifanywa HAZIWEIZI kufanywa na Watanzania. Vinginevyo wacheni sheria ifanye kazi.
 
Mimi toka kwenye ishu ya madawa ya kulevya makonda aliposema tumefanya uchunguzi miaka kumi kwa hiyo tukikuiita hatukuonei lakini wamemuita gwajima lakini wameshindwa kupata ushahidi wowote, sasa unajiuliza huo upelelezi wa miaka 10 umeshindwa vipi kugundua gwajima hana hatia?, halafu makonda kwenye hotuba yake juzi alisema "wananiita bwana mdogo lakini nataka nione nani ataingia shimoni" hii kauli alimlenga manji na kwa kweli kwa yanayotokea ni ushahidi tosha
 
Sasa kwanini kwa Dangote wamshtaki Afisa Uajiri lakini kwa Manji wamshtaki mmiliki? Hii ni double standard ya kijinga kabisa. Au kwa sababu Manji ni mwekezaji mzawa na Dangote ni mwekezaji mgeni? Kwahiyo katika nchi hii mgeni anathaminiwa kulko mzawa or? Idara ya Uhamiaji iache kutumika kisiasa.![/QUOTE]
Haya ni maagizo. Over
 
Back
Top Bottom