Mimi ni moja ya wananchi tunaomiliki viwanja eneo la Mwabepande kitalu P. Tuligharimia upimaji na baadaye baadhi yetu kupatiwa hati katika eneo ambalo manispaa wanampango wa kujenga kiwanda cha kusindika takataka. Mwezi wa tisa mwaka jana tuliitwa na watumishi wa Ardhi Kinondoni kuelekezwa mpango huo wa Serikali. Kwa kuwa ni jambo la maendeleo hatukuona shida kuachia eneo hilo baada ya watumishi hao kutuahidi kutupatia viwanja mbadala eneo la Bunju ndani ya miezi isiyozidi mitatu.
Hawa watu wamezuia maendelezo yoyote na wengine waliokuwa kwenye hatua mbalimbali ya kupata hati, hatua hizo zimeshitishwa. Kinachosikitisha ni kuwa watumishi hao hawajatupa mrejesho wowote tangia kikao hicho. Tumewahi kuandika barua mwezi Januari kutaka kujua kinachoendelea, watu hao wamekataa kujibu hata barua yetu.
Inashangaza wananchi tuliokubaliwa kutii maombi ya Manispaa bila shurti pamoja na kwamba tuna hati zetu walizotoa wao, leo wanatuona hatuna maana tena maana hata barua yetu hawataki kujibu. Mh. Mayor wa Kinondoni tulikupa nakala ya barua hiyo, kama haukuiona tunaweza kuleta nakala nyingine. Tafadhali tusaidie maana hawa jamaa ni zaidi ya jipu sasa.