Idadi ya wapiga kura za urais na ubunge Segerea inatatanisha

Hapa Jaji Damian Lubuva yeye analetewa taarifa tu za upigaji kura hivyo jukumu letu wapiga kura/wadau kuhoji inakuwaje kura halali za Ubunge zilizopigwa zikawa na tofauti kubwa na kura ''halali za Urais'' kuanzia ktk ngazi ya kituo, jimbo mpaka Taifa NEC.

Nina hakika kama Jaji Lubuva + NEC akibanwa kuhusu matokeo hayo kwa evidence basi lawama zitawaendea aliopiga bao la mkono na yeye Jaji Lubuva anaweza kuchukua maamuzi mazito kama Mh. Jecha wa ZEC.

Lakini ikiwa wadau hatuji na evidence yeye Jaji Lubuva atandelea kusoma matokeo 'rasmi'' , maana tumeona jinsi Maalim Seif alivyokuja na evidence za takwimu mpaka Mwenyekiti wa ZEC akabwaga manyanga na mbeleko ya kukibeba chama tawala.
 
Kuna jambo baya sana linajongea tz.mungu tusaidie.hivi hata jaji haoni aibu kusoma matokeo mabovu kwa uma,ujue kuna mguu wa kuku kisogoni mwake,hana la kufanya ni kuokoa maisha yake tu.
 
Lazima tukubali kuwa bado watanzania bado wanahitaji elimu ya kutosha ya uraia, watu wengi sana hawajapiga kura na kura zilizoharibika ni nyingi mno. Kibaya zaidi hata hapa mjini nako ni mbaya sana waliopiga kura jimbo la Ilala ni wachache mno

kwa hali inayoendelea kushawishika kupiga kura mwaka 2020 hapana
 

Lubuva yupo sawa.inawezekana hizo kura 50,000 ziliharibika watu mliamka na usongo wengine eti mlipanga kujitia hasira kumbe mnaenda kuharibu kura
 
Imawezekana watu wakaamua kupigia ubunge na kutokupigia raisi AU

Kupigia raisi na kutopigia ubunge.

Hapo ni sawa tu ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…