I Think I love my wife

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... na nadhani nampenda mke wangu.
 
Huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... na nadhani nampenda mke wangu.

Kwenye RED! Kwa hiyo huna uhakika?
 
I think uko sahihi kabisa, ni swali ambalo wengi wetu (married couples) inatupasa kujiuliza na we have to be true to ourselves though it might be difficult to change things but still there is a need of doing it.
 
For me, you better not THINK but rather BE SURE....

Mpaka umeamua kumuoa tena kwa mimbwembwe yote ile (kama nilikuwepo) najua ni kwa sababu ULIAMINI unampenda na anakupenda na sio ULIDHANI....Ungedhani ungejipa muda ujiamini na huenda ndipo wengine tunapojikwaa

Tatizo ni kuwa tukishaoa vile vilivyotupa uhakika wa kupenda na kupendwa tunavitupa pembeni

Mtazamo mzuri by the way and thanks
 
Huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... na nadhani nampenda mke wangu.

Umenichekesha sana TK yaani baada ya kuwaza kwa undani bado unadhani unampenda mkeo duuuuu we kiboko nafikiri subiri talaka mkeo akiona hiyo topic
 
Huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... na nadhani nampenda mke wangu.
Tuko.
kuna tofauti kubwa kumwambia mke,"Nakupenda mke wangu"
na kumwambia,"Nadhani nakupenda mke wangu"

Hilo pia umeshawahi kuliwaza?

Hapo ulipowaza kwa undani uliwaza nini? Masuali gani ulijiuliza na kujijibu ukafikia "nadhani nampenda mke wangu"
 
Huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... na nadhani nampenda mke wangu.

Ninakushauri hii kauli mwambie shemeji yetu "nadhani nakupenda mke wangu", kama unataka kujua kwa nini kuku hanyonyeshi.
 
For me

Nampenda mke wangu. This am sure of it.

Vinginevyo usingekuwa na haja ya kumuoa. labda kama upendo uliisha baadaye.....
 
huwa tunapenda kujibu tu, ooh mi nampenda sana mke/mume wangu, kwa sababu ni mke/mumeo. Hivi umeshawahi kuliwaza kwa undani... Mi nimefanya hivyo... Na nadhani nampenda mke wangu.

kumbe hata na wewe hujaliwazia vizuri ndo maana bado unadhani unampenda mke wako,,,,, huna uhakika..... Pole aisee.

Jamani sijakurupuka. Nimefikiria sana. Ni rahisi kusema kwa mdomo au kuamini moyoni, lakini ni ngumu kuigiza kutenda. Wapo wanaoimba kila asbh na jion nakupenda na tena wanaamini hivyo lakini wanatenda sivyo. Hivi hamjawaona watu ambao hawaguswi pale wanapowaudhi wenzao. Wapo ambao hawajisikii chochote wakiwaona wake zao wamekasirika, lkn wanaimba kila saa I love You. Wapo wanaojisikia raha zaidi wakila nyama choma baa kuliko kilichopikwa na wake zao lkn wanaamini wanawapenda wake zao. Wapo wanaopeleka nyama kwa nyumba ndogo na mke anakula maharage lkn wana uhakika wanawapenda wake zao. Wapo wasiopenda hata kuandamana na wake zao njiani japo wanasema wanawapenda. Nimejaribu kujifikiria vile najisikia vibaya mke wangu akiudhiwa, ninavyopenda kumuona ana raha, ninavyojitahidi kuepuka kumuudhi, na kubwa zaidi ninavyojisikia raha ninapomwona pembeni yangu. Najua hata hivyo inawezekana vile mi nafanya, sivyo ningetakiwa kufanya. Ndio maana n
 
Back
Top Bottom