Mfumo wa kutoa haki mahakamani unaipendelea Serikali maana rais ndo anateua majaji wote. Haiwezekani waalimu wakaishtaki Serikali kwa kudhulumiwa malipo ya stahili zao, wakatendewa haki.
rais ndo anateuwa mkurugenzi wa mashtaka, wakuu wa TAKUKURU kama apendavyo yeye,je huu sio mfumo mbaya?
Haiwezekani uchaguzi ukawa wa haki wakati mwenyekiti wa ccm ndo (Rais) anateuwa watendaji wa Tume ya uchaguzi, huu sio mfumo mbaya katika vyama vingi?
Fedha ya nchi inaibiwa Benki kuu bila vyombo vya dola kujua na kuzuia wizi huo. Je mfumo wetu wa ulinzi wa mali za umma uko vizuri? Fedha zinaweza kutolewa benki kwa mabilioni in CASH kweli hili linawezekana? Hii ni tanzania tu
Inawezekana vipi GAVANA wetu aende nje ya nchi apate matatizo ya kiafya afariki na kuzikwa huko huko nje ya nchi bila kushuhudia mazishi yake na yeyote kati ya viongozi, kweli mfumo wa kuenzi watumishi wa umma uko sawa? Tukisema tuna matatizo ya kimfumo nani anabisha?
Matatizo ni mengi chungu mzima, kuanzia ugawaji wa madawa katika mahospitali, ugawaji wa maji taka na safi, vifaa vya elimu kila kitu ni hovyo sana. MABADILIKO NI MUHIMU NDUGU YANGU, AMKA!!