I love u but i have no feeling with you

DIKASHWA

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
376
953
Hello MMU members,

Mwenzenu nimekuja hapa mbele yenu kuomba ushauri sababu nipo njia panda sijui nifanyeje nahisi maoni na mawazo yenu yanaweza kuniondoa au kunisaidia kwenye huu mkwamo.

Awali ya yote mimi naishi Mtwara kwa sasa ndipo napofanyia kazi lakini origin yangu ni Shinyanga, nilitokea kumpenda binti mmoja miaka kama kumi iliyopita by then tulikuwa sekondari na nilikuwa namtangulia madarasa kadhaa sikuweza fanikiwa kuwa naye kwa kipindi kile sababu alikataa kuwa kwenye mahusiano.

Kweli niliumia sana kwa kukataliwa ombi langu but still niliendelea kumpenda na alinivutia kila nilipokutana naye kwenye makorido ya shule. Baadae kila mtu aliendelea na mishe zake za shule tukawa tumepotezana na bad enough sikuweza kuwa na mawasiliano yake.

But daima nilimkumbuka sana na pamoja na miaka mingi kupita still nilimpenda na nilimuwaza ijapokuwa hatuonani na nilijua yeye hakunipenda. Facebook zilipokuja nilijaribu kumtafuta but sikufanikiwa coz majina niliyokuwa naandika zinatokea sura za watu wengine but miezi kama minne iliyopita niliona sura yake FB na alikuwa anatumia jina jingine nilimwomba urafiki akakubali.

Tulifanya chatting kuulizana tulipo na hali zetu za maisha in general yeye alinambia yupo kwao Shinyanga na baadae tukaamia wasap nikaanza kupasha tena kiporo, kipindi hiki hakukataa alikubari moja kwa moja na alionekana yuko very concerned na mimi.

Nilijaribu kumwuliza mahusiano yake yaliyopita but alinambia hayuko kwenye good terms na huyo mtu wake although wako wote kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitano hivyo alinambia nikimhakikishia nampenda ataquit coz nilimpenda kutoka moyoni nilimwambia she can do so but afanye handover ya kueleweka kwa mtu wake hasije akamsumbua.

Alikubali na alienda kumwambia huyo jamaa kuwa ameamua kuachana naye na amepumzika from relationship but jamaa aliwaka na alikataa kata kata kwamba huyu hawezi kumpotezea muda kiasi hicho na alishachezwa machale ya kunyang’anywa tonge mdomoni. Jamaa nasikia alibembeleza but huyu msichana alikataa kurudi na alisisitiza msimamo wake wa kutaka kuishi singo. But inaonekana jamaa alishachezwa na machale kabla coz muda mwingi nilimkeep bize sana huyu mdada kwenye maongezi ya simu.

Tuliendelea kuongea na tukakubaliana nimtumie nauli aje hapa Mtwara ili tujuane zaidi msichana huyo bila ajizi alikubali na mimi nilituma nauli. Alifanya arrangement na akaweza kufika huku Mtwara ninakoishi nilifurahi sana kuonana naye nilimhug na kukiss I was so happy ki ukweli coz nilijua ndoto yangu ya kuwa na huyu binti inaelekea kutimia.

Taratibu zote za kupokea wageni hasa wapenzi nadhani zinajulikana but huyu dada hakuonekana kunisupport nikajua may be amechoka na safari ngoja kwanza apumzike but siku iliyofuatia nilipojalibu alikataa na alinambia anajihisi kunipenda that’ Y katoka kule alipotoka but hana feelings kabisa za kufanya nilijaribu kumrudisha but alisema hajisikii kabisa. Nimejaribu kumwuliza but hajui na anasema ananipenda sana na nimvumilie hadi pale hali yake itakapotengamaa, binafsi nimemwelewa but nina maswali najiuliza.

Je kipi kimempata, Is it psychological problem or spiritual problem? Au bado mahusiano yake ya nyuma yanamsumbua kiasi kwamba anajifeel guilted kuwa na mtu mwingine?

Je ni kweli ananipenda au ndo hivo ananifariji? But me nampenda sana?
Je atakuwa amejiadaa kuwa hampendi huyo jamaa kumbe still feeling kaziacha?

Je nifanye nini kumsaidia na mimi kujisaidia pia. She loves me but she has no feeling with me?
 
She loves me but she has no feeling with me
kwanza hakuna kitu kama hicho duniani kabla ya love zinaanza feelings kwanza ndo inakuja love na love ni kitendo cha kumzoea mtu yani asipokuwa karibu na yy au ww unakuwa unammiss hyo ndo love ndo maana unaweza kumpenda mtu yeyote hata mama au baba yako bali feelings hizo ndo unaangukia ktk mapenzi bt ktk swala la mapenzi huwa zinaanza feelings ndo inakuja love so ww unapotuambia she loves you bt she has no feelings with you ni kama unataka kutuambia unaweza kwenda peponi bila ya kupitia njia ya mauti ni jambo amblo aliwezekani hata kidogo kama hana feelings na www basi hakupendi
 
Nimeyanukuu maneno yake sio mimi niliyeongea hivo me mwenyewe nilishangaa coz sijawahi kuexperience kitu kama hicho thats y nashangaa
 
hapo unapoteza mda tu brother huyo wala hakupendi kakimbia shida shinyanga hana lolote ukiendelea kushangaa utahudumia sana ila mzigo hupati ng'o!!!
hahahah ningejua hayo hata nisingelogwa kumtumia nauli yangu
 
Nimeyanukuu maneno yake sio mimi niliyeongea hivo me mwenyewe nilishangaa coz sijawahi kuexperience kitu kama hicho thats y nashangaa
basi hajui maana ya fellings au love kuna huwezekano akajua feelings ni sex tu ndo maana anasema anakupenda bt hana feelings na ww
 
basi hajui maana ya fellings au love kuna huwezekano akajua feelings ni sex tu ndo maana anasema anakupenda bt hana feelings na ww
sio kwamba me ndo sijui maana ya hayo maneno coz feelings ndo zinazotutofautisha kati ya mama dada na mpenzi
 
ukweli hakupendi kabisaaa.. ila alikuja mtwara kuangalia una nini ili ajiweke hapo , kwa hiyo vitu ndiyo vingemshiaka ila kwa kuwa hakupendi na akakutana na huna chochote kapuku tu ,, akaona azuge hana hisia ... HUPENDWI NA KAMA UNAMTAKA TAFUTA HELA UTAMUWEKA NYAVUNI
 
it's more of an ivestment plan than a problem on her side. Keshakuona wewe penda penda maana umeng'ang'ania toka shule. Keshajua kwako atavuna na huba ataipata kwa huyo mpenzi. Asikudanganye mtu mwanamke akidhamiria kuacha hata uwe king'ang'anizi vipi utapigwa chini tu so huyo jamaa yake hana mpango wa kuacha nae. Huyo jamaa wa miaka mitano yupo na ataendelea kuwepo, wewe utaitwa baby, utahudumia na baadae utaona status imebadilika fb kuwa married lakini si na wewe.
Get a hint and move on dude, mpe nauli arudi kwao na wewe uendelee na maisha yako.
 
ukweli hakupendi kabisaaa.. ila alikuja mtwara kuangalia una nini ili ajiweke hapo , kwa hiyo vitu ndiyo vingemshiaka ila kwa kuwa hakupendi na akakutana na huna chochote kapuku tu ,, akaona azuge hana hisia ... HUPENDWI NA KAMA UNAMTAKA TAFUTA HELA UTAMUWEKA NYAVUNI

Nafikiri hivyo pia. Labda atueleze hali yake kiuchumi ikoje ili tujaribu kufanya forensic. Bidada alienda Mtwara kikazi zaidi. Huyu demu anamchezea akili jamaa.
 
Back
Top Bottom