love has no boundaries... follow your heart
Umewahi kuwa narafiki yako wakaribu mno mnaye share nae mambo kibao(best friend)? mmekuwa pamoja,sekondari, chuo pamoja...anakujua mwanzo mwisho, viwanja vyako vyote na fujo zote nk
But here comes, alilazwa nikawa naenda kumcheck daily hospital na hapo ndipo nilioanza kumjua sister wake alikua anaishi Arusha kwa kwa mama yake, alikuwa anamleta chakula kila siku, she is so hot, cute.
At the begining ilikuwa sister kweli lakini taratibu tukaanza kujenga kakitu.........namtamani na yeye pia amenidondokea kimtindo, simu haziishi, sms usiseme tena za kiuchokozi.........I cant stop thinking about her
Mshikaji amepona sister haishi simu na sms,ofkozi hata mimi napiga na sms kwa sana tu lakini mshikaji hajui kinachoendelea
Aliniomba mchango wa birthday ya rafiki yake nikampa na sasa amekomalia jumamosi ijayo twende wote kwenye sherehe hiyo kigamboni.......amesisitiza kweli nisimuangushe, najua lazima nitaharibu tu
Natamani kumwambia najua na yeye anataka kusikia hivyo lakini kila nikimfikiria mshkaji nguvu yote inaniishia
MAONI YAKO MUHIMU
err, yeah it has, inaitwa relationships (yaani ndugu zako, rafiki zako, etc)
hamna kitu kibaya kama kumpenda dadake na rafiki yako especially kama mko close ki hivo unavyosema. think about it, ukija ukabreak up na huyu mdogo wake na mtu or u hurt her, unafikiri kakake, your friend atakuelewaje?? kama ni kupenda utampenda wengi tu, stay away from ur friends sister kama kweli unadhamini urafiki wake, t can only end badly
Not a good idea at all! Mkimbie kabisaaa! Nimepoteza best friend kwa njia hii. He was a great friend, wa shida na raha! Akampenda mdogo wangu na kuniambia kistaarabu. They dated 4 yrs. Lakini hawakuwa na furaha. He was insecure, wakitofautiana kidogo tu anauliza 'King' anasemaje? Did u tell her?' In the end my young sis was very unhappy but the guy wanted to marry her (nahisi kulinda urafiki). Mwisho waliachana, na urafiki wetu ulipungua sana. Hata harusi ya jamaa nilichanga ila kadi sikupewa!
I beg u! Don't do that! Nenda na rafiki yako kwenye besdei (how old ar u lakini? Mnachangishana besdei bash?)
Wakuu maneno yenu yamenigusa sana.......I cant afford to lose my friend
Lakini pia I cant ignore the fact im in love with her sister
Nafikiri ni bora kumpotezea ingawa najua i will let her down.................thats life