I hate my wife

Usaliti mnaanzaga nyie wakimalizia wanawake ndo wanaonekana wabaya
Wakati mwingi sio usaliti kama wengi mnavyochukulia,ni maudhi madogo madogo ambayo huwa hayavumiliki kirahisi,nadhani kama uko kwenye ndoa utakuwa unanielewa nazungumzia kitu gani.
 
usiache mke wako wa ndoa,
Hebu Jaribu kumpenda kama ulivyompenda Enzi za Uchumba Uone kama hajabadilika Mkuu,
Love can save it all,
huko nje utapotea,
Usiende Mkuu.
 
Ebu tuambie mkeo kakufanya nini kwanza mpk umchukie ivyo kingine ao wanawake zako usiwafiche kuhusu kuoa uwa mnaona aibu au
Hili ndio swala la msing what made you be angry at her huo ndio mwanzo wa yote mengne yote ni matokeo tu
 
hata sijakuelewa,unamchukiaje na bado unaishi naye mwisho wake nini,samehe tu
 
Hivi like kiapo cha "KWA SHIDA NA RAHA" huwa linatolewa kwa kiingereza?
Halafu huyo unayesema hujui uanzie wapi kumwambia kama umeoa, mbona ni rahisi sana! Vaa Pete yako ya ndoa, maongezi yenu yatakuwa hivi:
demu: Umeoa?
wewe: Ndiyo.
Demu: Mbona hukuwahi kunieleza?
Wewe: Nlidhani ningekueleza ningekupoteza, Nakupenda sana na sipo tayari kukupoteza.
Demu: Una muda gani ndani ya ndoa?
Wewe: Miaka mingi!
Tens unamjibu ukiwa mkali, maana huna cha kupoteza!
 
We kama ulimfumania,piga chini.hakuna masuala ya kuwekana vikao na mapadri au shehe.
 
tatizo lako mkuu unaonekana ulifanya kosa kuoa kabla hauja mchunguza vizuri tabia zake na anakuchukuliaje kwenye suala zima la mahusiano na kingine vijana wengi tunakulupuka kuoa tukiwa na umli mdogo mi msini shauli kuoa mi nawaza umilionea na ingawa ukisha oa ndo tiketi ya kupotea
 
Ila mm naona kama huo ni utoto na ulimbukeni wala sio ujanja

Ila mm naona kama huo ni utoto na ulimbukeni wala sio ujanja
Mkuu hapa nimejifunza kitu

 
Duuh pole sana kaka kama una imani kweli funga siku 7 huku ukiwa unaamka usiku wa manane unasali kwa imani mlilie Mungu shida zako zote nakuapia kila kitu chako kitakaa sawa na akili yako itatulia.
 
Ni vizur mleta uz ungekua waz yaliyokusibu au nn mkeo aliyekufanyia ili upate ushaur ambao utaweza kukusaidia, mana Ata kushaur ngumu chanzo hakijulikani
 
Ndoa bwana siku Maji yanajaa, siku Maji yanakupwa basi ndio maisha.
 
Nyie Mnadhani Kuna Kubwa Zaidi Ya Uzinzi? Unafikiria Namna Unavyomjali Lakini Anawapelekea Wengine. Inaumiza Kweli. Pole Ndugu
 
Nikupe pole tu Mkuu...

Ila usiendelee kujihusisha na hao wengine ambao huna mpango nao kuepuka kuwaumiza na kufanya mambo kua magumu zaidi.

Unahitaji muda wa kutulia na kujipanga upya kifikra
 
"Marriage is so overrated" Simkumbuki mtoa kauli. Ndiyo maana nimesitisha hili zoezi aisee. Nina marafiki karibu watatu wote wanalia matatizo makubwa kwenye ndoa. Jamani mwatutisha siye! Kuna nini huko kwenye ndoa? Mbona vilio na kusaga meno kila kona?
 
Wanawake sijui tulikosea wapi jamani,,,,yaani unampenda mtu kwa moyo wote kumbe yeye anakuchukulia for granted namna hii? seriously?....Pole sana Mkuu kwa unayopitia, ila zungumza na mkeo wa uwazi na siyo kucheat.
 
Pole sana mkuu, ila kwetu tunasema, anayemchukia mke wake anajichukia mwenyewe. All the best in repairing your relationship
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…