I can see our future so bright if we change our minds.


Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
559
Points
1,000
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
559 1,000
Kwa mzalendo yeyote yule hamu yake kubwa ni kuona Taifa lake likipiga hatua. Mabadiliko haya sio mabadiliko ya mali tu bali total transformation of human being.

Binadamu akibadilika kiakili na kiroho.

Ukiniuliza mimi mabadiliko haya mawili yaani ya kiakili na kiroho ni muhimu zaidi ya material transformation.

Kwasababu mabadiliko ya kiakili na kiroho ndio yanayopelekea mabadiliko mengine.

Kama binadamu wote tungekuwa na hekima na maarifa ya kutosha matatizo mengi ambayo tunakabiliana nayo katika dunia hii tusingekuwa nayo.


Mabadiliko ya binadamu ya kiakili ni muhimu. Kama Taifa hili lingekuwa na viongozi mature enough kukaa pamoja na kuamua baadae ya Taifa hili tungekuwa tumeendelea zaidi.

Tatizo tunafikiria maendeleo ya ki mali zaidi kuliko maendeleo ya kiakili ya watu wetu ambayo ingesaidia ku transform jamii yetu.

Ni muhimu sana kuangalia upya jambo hili. Elimu yetu hatotusaidia chochote kama haitazalisha watu wenye fikra sahihi na wazalendo.

Dhumuni la Taifa hili kuwasomesha watu wake ni maendeleo ya Taifa hili. Tujiulize watu wetu wanatumia akili zao ipasavyo kwa maendeleo ya Taifa hili?

Tusijidanganye wale wenye hekima na akili ndio wenye kuendelea na walio wapumbavu lazima watabaki nyuma. Watu wetu hawafikirii hata wale miongoni mwao wanajiita wasomi.


We can only measure your education by positive impact you brings in society.


Hili Taifa linahitaji watu watakao badilisha maisha ya watu wengine. Tunahitaji watu wetu wabadilishe mitazamo yao kuhusu Taifa hili, tuje kwa pamoja na tulijenge Taifa letu. Nina uhakika kama tutazikusanya akili zetu kwa pamoja na kufikiri juu ya ujenzi wa Taifa hili tutafika sehemu fulani.

Jambo la muhimu sana ni fikra za watu wetu ni jinsi gani tutazibadilisha na kuleta uzalendo na wajibu kwa Taifa hili. Jinsi gani tutawafanya watu wetu walipende Taifa hili na kuleta matumaini kwa watu wote. Kuwafanya watu wetu wote watambue wana share katika Taifa hili na wajibu wa kulijenga. Ni muhimu kuangalia fikra za watu wetu wote. Kama tutakuwa na watu wenye hekima na maarifa watafanya maamuzi ya busara ambayo yataleta positive impact katika jamii yetu. Adui mkubwa wa binadamu ni ignorance ni muhimu sana kupambana nae. Ni hatari kuliko kitu chochote ni afadhali uishi kwenye nyumba ya matope lakini uwe na akili.

Maono yetu lazima iwe ni jinsi gani tutalijenga Taifa hili sio ubinafsi ambao hautasaidia Taifa hili. Ni lazima tutambue tuna kitu cha kujenga kwa faida ya wote. Lazima tutambue tuna wajibu binafsi lakini kuna wajibu kwa jamii na kwa Taifa. Ndugu zangu mataifa hujengwa kwa conscious effort hayakui kama uyoga au kujengwa kwa mazoea. Mataifa yanajengwa na watu wanaofikiri na wenye busara.


Ili tujenge Taifa hili lazima tujenge upya mahusiano yetu na uaminifu miongoni mwetu. Tuna Taifa ambalo limegawanyika vipande vipande na lisilo kuwa na discipline. Huu ni ukweli na hatuwezi kukataa ukweli huu. Ni lazima tulete upya ORDER katika Taifa hili kama tunataka kuendelea. Tutengeneze vijana wenye maarifa na uelewa. Ni lazima tujenge Taifa la watu wenye kufikiri kama tunataka kutoka hapa tulipo. Ni lazima tujenge Taifa la watu wanaowajibika kwa familia na kwa Taifa. Ni lazima tujenge Taifa la watu wanao value familia na kulea watoto katika misingi ya maadili imara.

Vitu vinavyoendelea katika Taifa hili haviwezi kulifanya Taifa hili li move forward. Ubinafsi hauwezi kufanya Taifa hili lisonge mbele. Umoja katika wajibu utafanya Taifa hili lisonge mbele. Furaha yetu kama taifa itatokana tu na mafanikio ya pamoja kama nchi. Umoja wetu tu ndio utaleta furaha ya pamoja. Katika Taifa hili ni muhimu tukaheshimiana. Tunahitaji maridhiano ya kitaifa. Ni muhimu kuleta akili zetu pamoja katika ujenzi wa Taifa hili.

Sijawahi kumuona mpumbavu mkubwa kama mtu anayeliibia Taifa lake mwenyewe. Maendeleo ya mtu hayatokani na wizi that is self deception. Maendeleo ya kweli yanatokana na bidii na maarifa yake. Huwezi kujipongeza kwa mali inayotokana na wizi. Bali mtu anayefanya kazi kwa bidii kupata anachotaka ana cha kujipongeza na kujisifu. Ana kila namna ya kufurahia maendeleo yake. Mtu mwizi ni mtu aliyeshindwa kutumia akili zake na nguvu zake kuleta mabadiliko binafsi. Ni mtu asiye na thamani.

Kwahiyo wajibu wa kwanza kwetu ni kubadilisha fikra za watu wetu. Ni hatua ya kwanza na muhimu kwa Taifa hili kusonga mbele. Ubora wa Taifa lolote lile duniani unatokana na ubora wa mawazo ya watu wao. Kama sisi ni maskini mawazo yetu sio bora sana hivyo inatubidi tutie juhudi.


Ni muhimu kutambua maendeleo yetu kama watanzania ni jukumu letu wenyewe sio jukumu la Taifa lolote lile. Ni juhudi zetu ambazo zitatukomboa. Sio juhudi za wawekezaji wala Taifa lolote la kigeni. Kwahiyo ni lazima tuamke sasa. Tumaini langu ni kwamba kizazi hiki kitaibua viongozi ambao wataleta imani ya wananchi kwa Taifa lao na kwa viongozi wao.

Kwamba kitaibua changamoto mashuleni, kutia juhudi katika kutafuta maarifa na uelewa ili kwa pamoja tujenge Taifa hili. Ni muhimu kutambua heshima ya Taifa hili ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Ni lazima tujenge heshima hiyo miongoni mwa mataifa. Ndugu zangu ni lazima tufikirie kuhusu mambo haya ninayoandika ni muhimu kwa mustakabali wetu.


Nitasema na nitaendelea kusema Taifa hili linauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama Taifa lolote lile i can see possibility it is clear in my mind without any doubt. All we need to do is to change. To change our thinking. Tuwe wamoja na wenye kushirikiana. Tuweke mbele Taifa letu na kulipenda. I can see the future is so bright. I can see in my imagination cheering the unity of the Nation, progress and good fortune. God bless Tanzania.
 

Forum statistics

Threads 1,294,734
Members 498,025
Posts 31,186,322
Top