Head prefect
JF-Expert Member
- Apr 16, 2013
- 225
- 105
Wakuu,
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza,nimekuwa nasumbuliwa na kushtuka kwa mapigo ya moyo kwa muda kama miezi saba na zaidi, moyo unakuwa kama unaruka mapigo, au kudunda kwa nguvu kama unakita kwa nguvu fulani mara moja au mbili kisha unaendelea na mapigo yake ya kawaida. Hali hii hudumu kwa kipindi na kupotea kisha hurudia tena.
Nikiwa kwenye kutafakari hali hii nikapatwa na hali nyingine ya kupatwa na wasiwasi ghafla,tumbo kukata, Kubanwa kifua na kushindwa kupumua, kuweweseka na kukosa control na mwili kufa ganzi. Baada ya kuwaona wataalamu nikaambiwa kitaalamu inaitwa anxiety disorder na panic attacks. Hali hii imenisumbua mpaka nimeshindwa kutekeleza majukumu yangu ipasavyo. Nimefanyiwa vipimo vya moyo(ultra sound na Eco) , ini, figo na full blood picture sijaonekana na tatizo lolote.
Madaktari wameshauri niwaone wataalamu wa maswala ya saikolojia.
Nimejaribu kupambana na hii hali, lakini bado nina mshtuko wa mapigo ya moyo yananitesa sana, pamoja na kuwa na woga usioelezeka bila sababu. Huwa nina woga na hofu ambayo siijui, kila nikitafakari kuwa naogopa nini huwa sioni ninacho ogopa, lakini naogopa. Wakati mwingine nakuwa na hofu ya kufa.
Wapi nitapata wataalamu wa saikolojia? Niko Moshi Kilimanjaro.
Kama humu wapo wanishauri hapa kwenye huu uzi au pm wakuu.
Asanteni sana.