I am just being curious | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I am just being curious

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nzi, Jul 14, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,850
  Likes Received: 4,518
  Trophy Points: 280
  Salaam wanaJF!

  Katika siku za hivi karibuni television ya TBC1 imekua na kipindi kiitwacho Enzi Hizo; kipindi ambacho kinarushwa wakati wa taarifa ya habari ya saa 2 za usiku. Toka nimeanza kukiona kipindi hicho matukio mbalimbali ya Mwalimu yamekua yakionyeshwa kama namna za kusheherekea miaka 50 ya kupewa bendera na wakoloni.

  Kuna kitu ambacho nimekiona; matukio ambayo yamekua yakionyeshwa hususani kuhusu ziara za viongozi kwenda nje ya nchi yamekua yakigusia ziara za Mwalimu tu!! (mtanisamehe kama kuna ziara za AHM, BM au JMK zimeshawahi kuonyeshwa!!)

  Sasa katika kipindi hiki ambacho muungwana JMK amekua akilalamikiwa kutokana na yeye kua na safari zisizoisha na zisizo na tija za kwenda nchi za nje. Je, tabia hii ya kuonyesha ziara za Mwalimu tu ni mbinu ya muungwana na watu wake kujustify safari zake za nje?

  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...