I am convicied, CCM inaenda kushindwa uchaguzi

I am convicied, CCM inaenda kushindwa uchaguzi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,794
Reaction score
165,533
Naangalia kipindi cha "MADA MOTO" Channe 10 muda huu, mada ikiwa ni "VYAMA VYA SIASA NA ELIMU YETU",wageni waalikwa ni walimu na wote wanalaumu serikali ya CCM na inaonekana wanataka mabadiliko.

Mtangazaji karuhusu watazamaji wapige simu kutoa maoni yao.Kila aliepiga simu analamu serikali ya CCM na akionyesha dhahiri kutaka mabadiliko.

Nilikuwa kwenye bar moja wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku wa leo ambapo ITV walirusha mikutano ya campaign ya Lowassa na kisha ukafuata wa Magufuli.

Tulikuwa watu kama sita tukiwa tumekaa meza za jirani na ulizuka ubishi lakini watu 4 walikuwa wanaunga mkono UKAWA na watu wawili waliunga mkono CCM.

Nikikodi boda boda huwa na tabia ya kuhoji msimamo wao katika vijiwe vyao juu ya na nani wanamuunga mkono.Majibu yao yanaonyesha wengi wa waendesha boda boda katika vijiwe vyao wanaunga mkono UKAWA.

Kwenye Vyombo vya Usafiri wa Umma(Public Transport) kama vile dala dala na mabasi, wengi ni pro-UKAWA katika mijadala na mabishano ya kisiasa ndani ya vyombo hivyo.

Ukija kwenye vijiwe vya magazeti hali ni hiyo hiyo.Mtaani ndio kabisa.

Nakushauri na wewe fanya utafiti kidogo tu usio rasimi kama huu alafu uone utapata jibu gani.

Dhana ya mabadiliko mwaka huu ni dhana inayopata nguvu kila kukicha huku ikichagizwa na kauli maarufu "tumechoka"-hii ni hatari sana kwa chama tawala.

Jambo lingine ninaloliona laweza kutokea mwaka huu ni kuwa,kwa wale wasio na vyama na wale ambao walikuwa hawajafanya maamuzi, wanaweza kabisa kuwa infuluenced na msimano wa wengi na pia miongoni mwao kuna watakofuataa mkumbo-yote haya ni faida kwa UKAWA na hasara kwa upande wa pili.
 
CCM walipaswa kushindwa siku nyingi sana
shida ni kuwa upinzani haukuwa ready..
na hata now upinzani wakishinda basi 2020 ccm wanarudi
hiyo mess ya kutimiza ahadi na kujipanga itakuwa ngumu kufanikisha na set up haiwasaidii
 
Utafiti wangu ni kama wa kwako katika maeneo kadhaa uliyoyataja na matokeo ni kama ya kwako!

Indeed the country is now ripe for change!

And the first step is ccm out
 
CCM walipaswa kushindwa siku nyingi sana
shida ni kuwa upinzani haukuwa ready..
na hata now upinzani wakishinda basi 2020 ccm wanarudi
hiyo mess ya kutimiza ahadi na kujipanga itakuwa ngumu kufanikisha na set up haiwasaidii

Too negative the Boss!
 
Ndio maana wale wa maoni feki wamepata kigugumizi kutoa maoni ya tafiti zao. Wanasoma upepo kwanza hoping it will blow their way
 
CCM walipaswa kushindwa siku nyingi sana
shida ni kuwa upinzani haukuwa ready..
na hata now upinzani wakishinda basi 2020 ccm wanarudi
hiyo mess ya kutimiza ahadi na kujipanga itakuwa ngumu kufanikisha na set up haiwasaidii
Boss ndugu yangu mara nyingi naona una comments nzuri na zenye mshiko. Hii hapa mkuu naomba ni kupinge kidogo. CCM ikitoka sasa hivi sahau kabisa kwamba itarudi kwani sasa hivi imebakiza mamluki wachache wenye kutegemea ruzuku pasipo kutoa jasho kitu ambacho vyama pinzani vitakuja kudhitibiwa watu wa namna hiyo ndani ya Serikali. Take my words.
 
umejiridhisha kwa kiasi gani kuwa hao wote wana vichinjio?..sisi huku kitaa kama huna kitambulisho basi huna right ya kujadili mchakato wa uchaguzi/kampeni
 
umejiridhisha kwa kiasi gani kuwa hao wote wana vichinjio?..sisi huku kitaa kama huna kitambulisho basi huna right ya kujadili mchakato wa uchaguzi/kampeni
Hilo swali nimewauliza sana hasa vijana wa boda boda na kwakweli wanakwambia safari hii tumejiandikisha.
 
Mtoa mada uko sahh mi pia nilijarb na naendelea kufanya ka utaft kadg ila mpaka sasa Tuache ushabik ukawa wanaongoza
 
Utafiti wako ni kweli kabisa hata Mimi huoji watu tofauti tofauti kuanzia boda boda tena hao wanaipigia ukawa campaign kwenye daladala unakuta MTU mmoja au wawili magufuli madereva daladala na makonda nao wapiga campaign mtaani ndo usiseme. Watu wamechoka kiasi kwamba wanadai hata ukawa wangeweka jiwe wangelipigia kura
 
mkuu maccm hata ukiwambia haya mambo hayasikii. Lakini hata mimi nilishafanya tafiti zangu kama zako.

Na majibu yalitoka kama ya kwako. Kila maali ni lowassa. Watoto lowassa. Wazee lowassa. Vijana lowassa.

Huyu kamanda atashinda kwa mshindo mkubwa sana. Ataushangaza uma na ccm kwa ujumla.
 
umejiridhisha kwa kiasi gani kuwa hao wote wana vichinjio?..sisi huku kitaa kama huna kitambulisho basi huna right ya kujadili mchakato wa uchaguzi/kampeni

mkuu watu wanavichinjio. Mimi nilikomaa siku 3 nzima asubui mpaka jioni. Mpaka nikapata. Vijana ni wengi sana wamejiandikisha.

Ccm wakae tayari safari hii hawavhomoki. Wakina Lizabon.tata madiba.simiyu yetu.rich pol.getamycine.

Watafute kazi ya kufanya. Maana kichaka chao kinatiwa moto 25 oct. Wajiandae kutafuta ajira za kufanya. Maana chama kinacho walea kimefika mwisho.
 
mkuu maccm hata ukiwambia haya mambo hayasikii. Lakini hata mimi nilishafanya tafiti zangu kama zako.

Na majibu yalitoka kama ya kwako. Kila maali ni lowassa. Watoto lowassa. Wazee lowassa. Vijana lowassa.

Huyu kamanda atashinda kwa mshindo mkubwa sana. Ataushangaza uma na ccm kwa ujumla.
You are very right.

Kila mahali hivi sasa mijini na vijijini, kinababa na kinamama, vijana na wazee, wanaongelea kutaka mabadiliko through Edward Lowassa na Chadema pamoja na Ukawa.

Kitu pekee kilichobaki kwa wanaccm kwa sasa ni kujiandaa kisaikolojia ili waweze kukabidhi nchi kwa amani kwa Ukawa ifikapo Oktoba 25 ya mwaka huu.
 
CCM walipaswa kushindwa siku nyingi sana
shida ni kuwa upinzani haukuwa ready..
na hata now upinzani wakishinda basi 2020 ccm wanarudi
hiyo mess ya kutimiza ahadi na kujipanga itakuwa ngumu kufanikisha na set up haiwasaidii
YOu are very right...

Shida ni moja... watanzania ni wanafiki, kwahiyo hiyo mess inaweza kuwa kubwa zaidi CCM kwasbabu hawajazoea kuwa wapinzani,

My best case scenario ni wholesale political fracas with new alliances and coalitions plus brand new rivalries and drama... We may witness kuzaliwa kwa siasa na itikadi za agenda na msimu, which is not a bad thing
 
Katika ma group yangu ya whatssps ambayo ni kama 7 hivyo
8in 10 ukawa
2 in 10 ccm
Ur right pia bodaboda na vijana wengi 80%ukawa
 
CCM walipaswa kushindwa siku nyingi sana
shida ni kuwa upinzani haukuwa ready..
na hata now upinzani wakishinda basi 2020 ccm wanarudi
hiyo mess ya kutimiza ahadi na kujipanga itakuwa ngumu kufanikisha na set up haiwasaidii

CCM wakishindwa mwaka huu, they are a goner and they know it!

tumia hata microscope uwatafute KANU, UNIP, etc wako wapi leo hii.

know what I mean??

Nlipanda gari za kuchangia jioni noah ikazuka iyo mada dereva kidogo atolewe kwenye gari yake mana gari nzima ukawa kasoro dereva malalamiko juu ya chama tawala kweli mabadiliko hayaepukiki
 
Itategemea na kasi yao watakayoingia nayo.
Tuwape mda.
Wanaweza kujiongezea mda kama wataanza vizuri ikiwa watafanikiwa kushika nchi.
Ingawa bado kuna mambo mengi wao kwa wao wanapaswa kukaa nayo sawa kama upinzani.

Back
Top Bottom