Iran kuzindua Kombora la hypersonic hivi karibuni

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Iran: Kombora la Hypersonic litazinduliwa hivi karibuni

May 30, 2023 02:38 UTC

[https://media]

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH, amesisitiza kuwa: Kombora la balistiki la Hypersonic la Iran litazinduliwa hivi karibuni.

Mafanikio ya viwanda vya silaha vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan katika kuunda makombora ya balistiki katika miaka ya karibuni yamekuwa ya kustaajabisha.

Kombora la Khorramshahr 4 lililopewa jina la "Khaibar lilizinduliwa rasmi siku kadhaa zilizopita kama bidhaa mpya kabisa ya makombora yaliyoundwa na sekta ya viwanda vya Wizara ya Ulinzi ya Iran kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kukombolewa mji wa Khorramshahr tarehe 3 Khordad.

[https://media]Kombora la Khaibar

Kombora la Khaibar linaloendeshwa kwa kioevu, ni toleo jipya zaidi katika kizazi cha kombora la Khorramshahr, na lina uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 2000 na kubeba kichwa chenye uzito wa kilo 1500. Kombora hilo mbali na kuwa na sifa za kimkakati lina sifa pia za kitaktiki.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumatatu alisema mbele ya hadhara ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia kuwa: Majaribio ya kombora la Hypersonic yamefanyika na kwamba kombora hilo linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh kwa mara ya kwanza katika mwaka uliopita wa Kiirani yaani 1401, alitangaza habari ya kuundwa kombora la balistiki la Hypersonic.

Wakati huo Brigedia Jenerali Hajizadeh alieleza kuwa, kombora hilo jipya la balestiki la Hypersonic lililoundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran, mbali na kuwa na uwezo wa kupenya kwenye mifumo ya kisasa ya kutungua makombora, lakini lina uwezo mkubwa wa kupiga shabaha kwa usahihi mkubwa.

Alisema kuwa, kombora hilo lina kasi kubwa na uwezo wa aina yake, na kwamba hakuna teknolojia yoyote duniani inayoweza kulitungua hata katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa imejiunga na nchi chache duniani zenye teknolojia ya kutengeneza makombora ya aina hiyo ya Hypersonic yenye kasi zaidi ya sauti; ambazo ni Russia, China, Korea Kaskazini na Marekani.
 
Naona kuna kila dalili haya makombora yakafanyiwa majaribio kwenye vita mojawapo inayoendelea hapa duniani.
 
Human anazidi kujiongezea nafas ya kutoweka duniani in future nawashaur watengeneze kubwa za kupiga bara zima at once
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom