Thadei Ole Mushi
UPINZANI NA SIASA NYEPESI
Na Thade Ole Mushi
Wamekosa cha kuzungumza, wamekosa cha kuwaambia wananchi, ahadi zao hazijakamilika, wameamua kufanya siasa Nyepesi.
Eti kwanini Makamu wa Rais aje kuaga miili badala ya Rais.
Hii kwa sasa ndio kick yao, ndio sera yao, ndio mazungumzo yao nk.
Acheni kutumia msiba wa Arusha kisiasa. Mama Samia ana hadhi inayokaribiana kabisa na rais kasomeni katiba ya nchi.
Cheo cha Urais ni Taasisi, Rais ameshafuata taratibu zote za kutoa pole, Rais kashaonesha ni kiwango gani ameguswa na msiba huu. Taasisi ya Urais inaona mama Samia anatosha kuiwakilisha Ofisi ya Rais.
Kwenye tetemeko Kagera Ofisi ya Rais ilimtuma Waziri Mkuu na alitosha kabisa kwa shughuli ile. Watu wapo kwenye majonzi nyie mnaleta siasa. Katiba yetu inatambua hadhi ya makamu wa Rais.
SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS
Ibara ya 47.
Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
Kwa sera zenu hizi Ikulu mtaikuta kuzimu....
Ole Mushi.
-------
Huyu anayejiita mhandisi Tadei Ole Mushi ni majanga , I suppose he is the most foolish creature to exist in the planet
Eti siasa nyepesi wapinzani wameshindwa kutimiza ahadi ni hapo tu kadhihirisha upumbavu wake kama mhandisi.
Wa kutimiza ahadi ni wale waliopewa dhamana ya kuongoza wapinzani ni watchdog tu kazi yao ni kuhakikisha yale yote ambayo waliopewa dhamana waliahidi kutekeleza yanatekelezwa, wapinzani watatekelezaji ahadi wakati hazina hawana ? Huyu mhandisi Thadei Ole Mushi VIPI? Ni lazima atakuwa na cheti fake.
Siasa ni siasa tu hakuna siasa nzito au siasa nyepesi. Mhandisi umenisikitisha sana it seems you have your brain on your knee