Huyu sio tapeli kweli ?

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,551
1,776
Wasalamu wajumbe
Kuna huyu jamaa mwenye namba 0652 174 472 amenipigia anasema anauza Mac Bro Hard Disk 500, RAM GB16 , Processor 2.7GHZ. 12, Display Retina anauza 300,000 (laki 3) !!!!!!!

Ajabu anasema yuko Ludewa mkoa wa njombe nimtumie nusu kwanza ! Hapa sio kupigwa mchana kweupe kabisa ?? !!

Kuna Mac Book ya pesa hiyo kweli ? Nimejaribu kucheck hiyo namba Google inaokena ni tapeli wa Kupatana , sasa natafuta uhakika zaidi.
 
Matapeli mbona rahisi sana kuwafahamu...
1. Hakuna Mac Pro ya pesa hiyo hata Ram ikiwa 1gb

2. Mwambie una ndugu yako Ludewa kesho anakuja na pesa kuufuata mzigo... Akikujibu njoo nikupe pesa
 
Matapeli mbona rahisi sana kuwafahamu...
1. Hakuna Mac Pro ya pesa hiyo hata Ram ikiwa 1gb

2. Mwambie una ndugu yako Ludewa kesho anakuja na pesa kuufuata mzigo... Akikujibu njoo nikupe pesa
Anakwambia njoo ila akitokea mteja anauza.. Unakwenda hatokei anasema ameshauza..
 
Wasalamu wajumbe
Kuna huyu jamaa mwenye namba 0652 174 472 amenipigia anasema anauza Mac Bro Hard Disk 500, RAM GB16 , Processor 2.7GHZ. 12, Display Retina anauza 300,000 (laki 3) !!!!!!!

Ajabu anasema yuko Ludewa mkoa wa njombe nimtumie nusu kwanza ! Hapa sio kupigwa mchana kweupe kabisa ?? !!

Kuna Mac Book ya pesa hiyo kweli ? Nimejaribu kucheck hiyo namba Google inaokena ni tapeli wa Kupatana , sasa natafuta uhakika zaidi.
Ludewa ya njombe au kuna mtaa unaitwa ludewa huko dar? Maeneo na bidhaa yenyewe vinatia shaka upatikanaj wake, ni sawa na mtu kukuambia anauza sato akiwa mtwara
 
Inawezekana kwa bei hiyo, lakini kama ina iCloud ikiwa on. Maana ikiwa hivyo hata bure anaweza kukupa tu. Kuna maswali ya msingi ya kumuuliza
1. Ni MacBook Pro ya mwaka gani?
2. Je, haina iCloud - iCloud ipo on or off
3. Battery yake inakaa masaa mangapi?
4. Ni inch ngapi?
Kwa kifupi muulize maswali mengi uwezavyo, kama atakujibu kwa ufasaha tafuta namna akutumie picha yake pia. Kimsingi, mwingine unakuta ameipiga kwa mtu
 
Achana nae niliongea nae wiki iliopita niliona tangazo lake kupatana nikampigia simu alikua na hiyo macpro na iPhone 6+ cha ajabu kila kimoja ni laki3 nikampigia simu akaniambia yupo iringa kama naitaka simu niwahi asubuh na mapema kutuma hela sababu kuna mtu anaitaka mi nikampotezea sababu hata kiwanda cha iPhone chenyewe hakiwezi kuuza iPhone 6+ laki3
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom