Kwenye maisha ya familia nyumba ni muhimu sana. Naona shemeji yako anaishi maisha ya ndoa, hafikirii maisha ya familia.
Nyumba inaweza ikawa si kipaumbele kwa baadhi ya watu, hasa nchi za ng'ambo kama ulaya na marekani, wao akipata apartment kazi kamaliza. lakini kwa nchi zetu za kiafrika ni tofauti, hata kama umepanga nyumba nzuri kiasi gani, bado utaonekana huna maisha. Hata kama unapenda maisha ya kupanga jenga nyumba yako tu uendelee na kupanga, heshima itakuja.
Mwambie dada yako ajenge nyumba ya gharama yeyote aiwezayo (nikiamini kiwanja wanacho). Ikiwezekana ajenge hata bila kumshirikisha mumewe maana hakuna ushirikiano. Kama itamuwia vigumu mwambie awashirikishe nduguze (akina wewe), akajenge hata kwao maana huko mbele hajui nini kitatokea, pengine mumewe hana mpango wa kuishi nae hadi dahari.