Huyu Robert Shumake ni balozi wa nchi ngapi?

Huyu Robert Shumake ni balozi wa nchi ngapi?

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,412
Reaction score
5,013
Kwa anayejua naomba kufahamisha hawa mabalozi wa heshima huwa wanapatikana vipi, maana huyu bwana Robert Shumake ambaye tunaambiwa ni balozi wetu wa heshima US, naona pia ni balozi wa Botswana at the same time (http://botswanaconsulate.org/botswana-consulate/honorary-consul-of-the-republic-of-botswanna-bio/), Hii ni halali au?..halafu vigezo huwa ni vipi mbona jamaa kama chekbob fulani hivi na mie nishazoea balozi huwa mtu mzima...Anyway naomba tujadili.

16137-RhondaWalkerandRobertShumake3.jpg


IMG_8307.JPG
 
Usishangae ukaambiwa condolezza rice ni balozi wetu pia
 
Ndiyo injiiiii yetu hii. Kila rangi zipo.na miujiza pia.
 
Kwa anayejua naomba kufahamisha hawa mabalozi wa heshima huwa wanapatikana vipi, maana huyu bwana Robert Shumake ambaye tunaambiwa ni balozi wetu wa heshima US, naona pia ni balozi wa Botswana at the same time (Mr. Robert Shumake Bio | Honorary Consul of the Republic of Botswana), Hii ni halali au?..halafu vigezo huwa ni vipi mbona jamaa kama chekbob fulani hivi na mie nishazoea balozi huwa mtu mzima...Anyway naomba tujadili.

16137-RhondaWalkerandRobertShumake3.jpg


IMG_8307.JPG
Balozi ni utambulisho wa watu wa taifa fulani katika nchi ya kigeni..., ni mwakilishi na msemaji wa mkuu wa taifa fulani ktk nchi ya kigeni... Kwa maana hiyo aidha watanzania ndio machekibob au rais wetu ndo chekbob.. maana quality unazoziona kwa balozi ni reflection ya quality ya wale anaowawakilisha.
 
Taarifa zaidi,hii ni hatari,hata taratibu za usalama hazko hv,taarifa zaid
 
Robert Shumake ni jasusi wa CIA,nyie kumbe hamuwajui wamarekani,majasusi dizani ya shumake wametapaka dunia nzima,na huwezi kuwagundua,wengine wako ubalozini wakitambulishwa kama afisa balozi,wengine wapo ktk mashirika ya misaada,wengine huja kama wakufunzi wa kijeshi,'military trainer'na wengine huja kama mapadri,CIA si ya mchezo,ndo taasisi ya serikali ya US iliyoajiri watu wengi kuliko taasisi yoyote ile.
 
Robert Shumake ni jasusi wa CIA,nyie kumbe hamuwajui wamarekani,majasusi dizani ya shumake wametapaka dunia nzima,na huwezi kuwagundua,wengine wako ubalozini wakitambulishwa kama afisa balozi,wengine wapo ktk mashirika ya misaada,wengine huja kama wakufunzi wa kijeshi,'military trainer'na wengine huja kama mapadri,CIA si ya mchezo,ndo taasisi ya serikali ya US iliyoajiri watu wengi kuliko taasisi yoyote ile.

Mkuu uko sahihi 95%.
Hapa Tz wapo wageni wengi wa namna hii kutoka mataifa kadhaa ya magharibi (yaliyoendelea) kwa minajiri mbalimbali; ukichukulia kwamba Tz inatambulika kama Centre of African Politics.
Watakuja wawekezaji, wakujitolea, NGO nk. Ili mradi kila kundi linafanya kazi ya siri lilotumwa na nchi yake kwa malengo maalum.
Unategemea kwa uwekezaji wa gharama kubwa vile kwa kujenga reli na kununua train za kisasa, lini huyu bilionea atarudisha pesa yake na kupata faida kwa safari tu ya town to airpot isyozidi 500 kwa kichwa?
Unadhani katoa msaada?
Anajua afanyalo na hata waliomtuma wanajua faida ya uwekezaji huo make watakuja CIA wasiopungua 100 kwa mradi huu na oviously watafanikiwa kuiteka Africa chini ya jangwa la sahara.
Stay tuned.
 
wanaojua maana ya balozi wa heshima wanaweza wakatusaidia, mfano Emmanuel Ole Naiko ni balozi wa heshima wa Botswana hapa nchini pia Profesa Simon Mbilinyi ni balozi wa heshima wa nchi fulani siikumbuki.
 
Back
Top Bottom